NANDO amkera LULu ile mbaya; tazama picha hapo chini


MTOTO mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameibuka na kufunguka kuwa amekerwa na kitendo cha mshiriki wa Shindano la Big Brother Africa (BBA) 2013, Amir Khan Nando kujinadi kuwa aliwahi kuwa ‘mtu’ wake kitu ambacho si cha kweli.
Akizungumza na Ijumaa kwa juzikati, Lulu alikiri kuwa Nando aliwahi kumtokea na alimkubalia awe ‘my baby’ wake lakini baada ya kumshtukia kuwa hana nia nzuri, alimpotezea kabla hawajazama kwenye dimbwi la mahaba.
Mtoto mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Mtoto mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Nahisi Nando alikuwa kwanza anataka kiki kupitia mimi na ndiyo maana kila alipotaka kupiga picha na mimi, nilimkatalia coz nilishamgundua nia yake, nimemshangaa kweli alipotangaza kuwa niliwahi kuwa mpenzi wake labda alivyonitokea na kumkubalia lakini sikufanya naye chochote kinachohusu mapenzi ndiyo akaona aseme hivyo,” alisema Lulu.
Juzikati, Nando alifanya mahojiano na Global TV Online ambapo awali alidai ‘kutembea’ na Lulu lakini alipobanwa zaidi aliumauma maneno na kudai anampenda na yuko tayari kumuoa kwa sababu ana sifa za kuwa mke (wife material).
Amir Nando
Amir Nando
Ili kuyapata mahojiano kamili ya Nando, tembelea tovuti ya utaona bango la Global TV, bofya hapo na utapata majibu mengi ambayo staa huyo wa BBA alifunguka pamoja na vipindi vingine vya kusisimua.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

HILI NDILO BIFU KUBWA KATI YA RIHANA NA NICK MINAJ.