Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai, 2016

Rais Magufuli Atoa ONYO Kali....."Mimi sijaribiwi, wasije kunijaribu. Atakayeleta vurugu atashughulikiwa bila huruma!

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Julai, 2016 ameanza ziara ya siku nne katika mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na Geita akitokea mkoani Dodoma, ambapo amezungumza na wananchi kwa lengo la kuwashukuru kwa kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana  na kueleza juhudi zinazofanywa na serikali katika kutatua kero za wananchi na kuwaletea maendeleo. Akiwa Mkoani Singida, Rais Magufuli aliyeongozana na mkewe Mama Janeth Magufuli amewasihi watanzania kufanya kazi kwa juhudi na kujiepusha na vitendo vya vurugu vinavyohamasishwa na baadhi ya wanasiasa huku akionya kuwa serikali yake haitamvumilia mtu yeyote ambaye atathubutu kuchochea vurugu ikiwemo maandamano kinyume cha sheria. “Sitaki nchi hii iwe ya vurugu, watakaoleta vurugu mimi nitawashughulikia kikamilifu bila huruma, na wasije wakanijaribu, mimi ni tofauti sana na kama wapo watu wanaowatumia wakawaeleze vizuri, mimi sijaribiwi na wala sitajaribiw

Bodi ya Mikopo yatangaza majina 1,091 ya wadaiwa Ambao Hawataki Kulipa (Awamu ya kwanza).....Bonyeza Hapa Ujitazame Kama na Wewe Jina Lako Lipo

Picha
Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB), inawaarifu wadaiwa wote ambao mpaka hivi sasa hawajaanza kulipa mikopo waliochukua kipindi wanasoma, na wenye majina yao kwenye orodha hii kwamba wamevunja mkataba kutokana na sheria ya bodi hiyo No. 9 ya 2004 (kama ilivyorekebishwa) sehemu ya 19 (1). Na wanataarifiwa kwamba, kulingana na sheria hiyo ya bodi (HESLB)  No. 9 ya 2004, Bodi imedhamiria kutenda yafuatayo:- (i) Bodi itachukua hatua za kisheria kulingana na kipengele cha 19 (a) (1) cha sheria ya bodi. (ii) Mdaiwa atapewa penati ya 5%  juu ya ile 5% iliyokua ikitozwa kabla kwa kila mwezi kwenye deni lililobakia au alilonalo. (iii) Mdaiwa ataongezewa gharama za kumtafuta alipo ili alipe deni zilizoingiwa na bodi. (iv) Mdaiwa atawekwa kwenye ‘blacklist’ na maelezo yake yatapelekwa  kitengo cha kumbukumbu ya wakopaji na hivyo kushindwa kukopa sehemu nyingine yoyote. (v) Mdaiwa atazuiliwa kupata udhamini wa Serikali au udahili wa masomo ya j

Papa Francis Aanguka Ghafla Akiongoza Misa

Picha
POLAND: Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis, ameanguka ghafla wakati akiwa anaongoza misa, baada ya kujisikia vibaya. Inadaiwa Papa husumbuliwa na tatizo la maumivu ya miguu na mgongo

Al-Shabab Washambulia Mtambo wa Mawasiliano Kenya

Picha
Washukiwa wa kundi la Al-Shabaab mapema leo Alhamisi wameshambulia na kulipua mtambo wa mawasiliano ulioko katika mji wa Fino, Lafey katika kaunti ndogo ya Mandera nchini Kenya. Afisa mkuu wa Polisi huko Lafey, Bosita Omukolongolo, amesema kuwa kisa hicho kilitokea saa nane usiku. Afisa huyo wa Polisi anasema kuwa walikabiliana vikali na wanamgambo hao, lakini hakuna maafa yaliyoripotiwa upande wa polisi waliokuwa wakiulinda mlingoti huo wenye vifaa vya kupeperusha mawasiliano. Kundi la Al- Shaabab, ambalo lina makao yake nchini Somalia, limehusika na mashambulizi ya mara kwa mara pamoja na mauaji nchini Kenya na mataifa kadhaa ya Afrika Mashariki na upembe wa Afrika.

Waziri Mkuu kuhamia Dodoma Septemba mwaka huu......Asema akishahamia, Mawaziri na Naibu Mawaziri wote wafuatie mara moja

Picha
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema atahamia Dodoma ifikapo Septemba, mwaka huu kuonyesha kuwa Serikali imedhamiria kutekeleza ahadi ilizotoa kwa wananchi. Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Jumatatu, Julai 25, 2016) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa mkoa wa Dodoma na kuwashukuru kwa ushiriki wao kwenye maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa zilizofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa, mjini Dodoma. “Jana nilimwita Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na kumwambia akamilishe matengenezo kwenye nyumba yangu kwa sababu ninataka kuhamia Dodoma ifikapo Septemba,” amesema na kushangiliwa na mamia ya wakazi wa mji wa Dodoma waliohudhuria maadhimisho hayo. Amesema tangu Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, kazi nyingi zimefanyika na wananchi wameziona na kwamba sasa hivi kazi iliyobakia ni utekelezaji wa ahadi alizotoa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli. “Wananchi kazi mmeziona na sasa tunaenda kwenye utek

Simu za Nokia kuja kivingine na mfumo wa Android Nougat

Picha
Nokia imeripotiwa kuwa kwenye mipango ya kurejea kwenye soko la smartphone na simu mpya zinazotumia mfumo mpya wa Google, Android Nougat, version 7.0. Simu hizo zinatarajiwa kuingia sokoni mwishoni mwa mwezi huu na zinatarajiwa kuzuia majina vumbi kama simu mpya za Samsung, Galaxy S7, S7 Edge na S7 Active. Zitakuwa na screen yenye ukubwa inchi 5.2.

Kaka‬ wa Rais ‪Obama‬, Malik Obama Atoa Sbabu Sita za Kumuunga Mkono ‪Donald‬ Trump

Picha
Malik Obama is disappointed with his brother President Barack Obama so much that he has opted to support Donald Trump whom he will vote for come November 8th. President Obama’s Kenyan half-brother Malik Obama has bought into Trump’s ideology “Make America Great Again” Malik has caused a storm after he publicly declared his support for Republican presidential nominee, Donald Trump. In an interview with the Post from his home in Kogelo, Siaya County, Malik said that his brother President Obama had disappointed him and that he would vote for Trump. (Malik has a dual citizenship for Kenya and US.) He cited six reasons why he will be voting Trump on November 8th. 1. Malik admires Donald Trump Malik told the Post Donald Trump speaks from his heart adding that he was deeply disappointed by Democrats. He particularly singled out his brother’s administration as the reason why he switched allegiance to Republican. 2. President Obama failed to prosecute Clint

Wanafunzi Wote Walio Vyuo Vikuu Wasio na Sifa Kuondolewa. Vyuo Kurudisha Fedha za Wanafunzi Hewa...

Picha
Waziri wa Elimu Joyce Ndalichako amesema wanafunzi wote wanaosoma vyuo vikuu wasio na sifa wataondolewa bila kujali wapo mwaka wa ngapi na hata waliopo kazini wataondolewa kwa kuwa hao ndio wanatumia njia za mkato kwenda kupata kazi japokuwa hawana sifa. Waziri amevitaka vyuo vikuu kuchukua wanafunzi walio bora ili kuweka sifa ya ubora wa vyuo vyao Na kuhusu vyuo vilivyochukua fedha ambazo hazikustahili vitalazimika kurudisha fedha hizo na kisha kuchukuliwa sheria kwa waliohusika, amesema bado wanaendelea kugundua idadi kubwa ya wanafunzi mfu walioombewa fedha tangia waanze zoezi hilo na sasa wamefikia vyuo vitatu tu.

Breaking News Wakurugenzi wote wa NSSF wamesimamishwa kazi, kupisha uchunguzi wa idara zao katika shirika hilo.

Picha
BODI ya wakurugenzi ya Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limewasimamisha kazi wakurugenzi sita na meneja watano na Mhandisi mmoja kufuatia matumizi mabaya ya ofisi na kutofuata sheria na kanuni. Kwa mujibu wa taafia iliyotolewa leo na Mkurugnezi Mkuu wa NSSF,  Profesa Godius Kahyarara imesema hatua ya kuwasimamisha kazi wakurugenzi na mamenja hao inafuatia kikao cha bodi chini ya uenyekiti wa  Prefesa Samweli Wangwe kilichokaa kuanzia Ijumaa iliyopita. “Bodi imeagiza  kusimamishwa kazi Wakurugenzi , Mameneja watano na Mhandishi mmoja ili kupisha uchunguzi ili kubaini wahusika katika tuhuma za ubadhirifu, matumizi mabaya ya ofisi na kutofuata kanuni, sheria na utatibu katika uwekezaji,  usimamizi wa miradi na manunuzi ya ardhi na ajira,” alisema Profesa Kahyarara. Aliwataja wakurugenzi hao ni Mkurugenzi wa mipango, Uwekezaji na Miradi, Yakub Kidura, Mkurugenzi wa fedha, Ludovick Mrosso, Mkurugenzi wa rasilimali watu na utawala, Chiku Matessa, Mkuru

Hichi ni Kiasi cha Pesa Kilichoingia Tangu Daraja la Kigamboni Lianze Kutumika

Picha
Tangu daraja jipya la Kigamboni lianze kutumika rasmi tarehe 19/04/2016 limekusanya jumla ya shilingi bilioni 1.3 kutokana na tozo za vyombo vya usafiri. Daraja hilo liligharimu dola za kimarekani milioni 136 ambazo ni takribani bilioni 300 kwenye ujenzi wake.

KIJANA WA KITANZANIA ATENGENEZA GARI LA KIFAHARI, ALIITA ‘KAPARATA’

Picha
 Kijana Jacob Louis 'Kaparata' (38) akimwelekeza mmiliki wa blogu ya Taifa Kwanza! jinsi alivyolitengeneza gari lake la kifahari aina ya 'Kaparata' kwa kipindi cha miezi mitatu tu. Jacob Louis 'Kaparata' akiingia kwenye gari lake alilolitengeneza mwenyewe kwa miezi mitatu. Wananchi wakipigana vikumbo kulishangaa gari la 'Kaparata' katika viwanja vya maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Saba Saba) jijini Dar es Salaam.   Na Daniel Mbega SIYO Jeep la Mmarekani wala Korando la Mkorea. Hili ni gari aina ya Kaparata ambalo limebuniwa na kutengenezwa na kijana Mtanzania, Jacob Louis ‘Kaparata’ (38), mkazi wa Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam ambaye ametumia vifaa vingi vinavyopatikana hapa hapa nchini. Waliobahatika kuliona gari hili katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa – Saba Saba wamekiri kwamba huu ni ubunifu mkubwa ambao unastahili kuungwa mkono na serikali na mamlaka nyingine. “Nimetumia vifaa vingi vinavyopatikana hapa nc

Mvutano wa CCM na CHADEMA Walitikisa Jeshi la Polisi, BAVICHA Yaandaa Zaidi ya Vijana 5000 Kuzuia Mkutano, Polisi Mara Yasema Wanacheza Ngoma ya Kitoto

Picha
Mvutano wa kisiasa baina ya vijana wa CCM na CHADEMA  kuhusu katazo la mikutano ya vyama vya siasa umezidi kukua huku jeshi la polisi likitarajiwa kutoa tamko kuhusu hali hiyo. Hali hiyo ya jino kwa jino imejitokeza  zikiwa zimebakia siku 16 kabla ya kufanyika kwa mkutano mkuu wa CCM July 23, ambao Baraza la Vijana la CHADEMA ( BAVICHA )  limesema litawasaidia polisi kuuzuia. Tayari BAVICHA limetangaza kuandaa vijana 5000 kutoka sehemu mbalimbali nchini kwenda kuzuia mkutano huo utakaotumika kumkabidhi Rais John Magufuli uenyekiti wa chama hicho. Jumatatu iliyopita, Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka aliionya Bavicha wasiende Dodoma kuzuia mkutano wa CCM kwa kuwa watatumia kila mbinu kuwazuia ili kulinda heshima ya chama chao. Shaka alisema mkutano huo utafanyika kama ulivyopangwa, hivyo Bavicha kama kweli ni vidume wa mbegu wajitokeze ili wakione cha mtema kuni. Shaka alisema UVCCM wako tayari kuidhihirishia dunia kwa kuwatia adab

Orodha ya wakurugenzi wa Halmashauri na Majiji walioteuliwa leo na Rais Magufuli

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo July 07 2016 amefanya uteuzi wa wakurugenzi wa halmashauri za majiji 5, Manispaa 21, Miji 22 na Wilaya (DC) 137 za Tanzania Bara. Uteuzi huo umetangazwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Mussa Iyombe ambapo kati ya wakurugenzi wote 185 walioteuliwa, 65 wameteuliwa kutoka orodha ya wakurugenzi wa zamani na 120 ni wakurugenzi wapya. Orodha ya wakurugenzi walioteuliwa kulingana na mikoa yao ni kama ifuatavyo; ARUSHA ⦁ Arusha Jiji – Athumani Juma Kihamia ⦁ Arusha DC – Dkt. Wilson Mahera Charles ⦁ Karatu DC – Banda Kamwande Sonoko ⦁ Longido DC – Jumaa Mohamed Mhiwapijei ⦁ Meru DC – Kazeri Christopher Japhet ⦁ Monduli DC – Stephen Anderson Ulaya ⦁ Ngorongoro DC – Raphael John Siumbu DAR ES SALAAM ⦁ Dar es salaam Jiji – Siporah Jonathan Liana ⦁ Kinondoni Manispaa – Aron Titus Kagurumj

Shela ya Harusi Aliyovaa Nancy Summary Siku ya Harusi Yake Yazua Gumzo

Picha
Shela alilovaa Miss Tanzania 2005, Nancy Abraham Sumary alipokuwa akifunga ndoa na mchumba’ke, Lucas Neghesti mwishoni mwa wiki iliyopita, limezua gumzo kutokana na ‘usimpo’ wake licha ya gharama yaku kuwa kubwa ambapo linadaiwa kununuliwa kwa shilingi milioni tano za Kitanzania.  Kwa mujibu wa chanzo chetu, kisa cha kuzua gumzo ni jinsi lilivyokuwa simpo kwa muonekano ingawa lilimpendeza na kumtoa chicha kwani wapo waliopenda namna lililofanana na lile la mdogo wake staa wa muziki Marekani, Beyonge Knowles, Solange Knowles ambalo ndiyo lilitakiwa kuwa na gharama kubwa kwani linastahili kutokana na kuwa limeshavaliwa na staa huyo wa Marekani. Hata hivyo, wapo waliomsifia kwa jinsi alivyojidizaini na kuwa bibiharusi simpo na mwenye muonekano wa kimataifa kwani kwa Watanzania wengi imekuwa ni vigumu mwanamke kufunga ndoa akiwa na nywele zake (natural) tofauti na wengine ambao hupenda matashtiti kibao. Nancy na Luca walifunga ndoa Ijumaa iliyopita amb

Lionel Messi Ahukumiwa ‘Kufungwa miezi 21 Jela’

Picha
Mchezaji nyota wa Argentina na Barcelona Lionel Messi amehukumiwa kifungo cha miezi 21 jela baada ya kupatikana na makosa ya kutumia ulaghai wakati wa ulipaji ushuru, vyombo vya habari nchini Uhispania vinaripoti. Babake, Jorge Messi, pia amehukumiwa kufungwa jela kwa kuilaghai Uhispania €4.1m (£3.2m; $4.6m) kati ya 2007 na 2009. Wakati wa kesi, waendesha mashtaka walisema maeneo salama yenye kinga dhidi ya ushuru Belize na Uruguay yaliyumiwa kuficha mapato kutokana na uuzaji wa haki za picha za mchezaji huyo. Lakini Messi amesema hakufahamu lolote kuhusu masuala yake ya kifedha.

Taasisi ya Maridhiano kutafuta muafaka kati ya UKAWA na Naibu Spika

Picha
TAASISI ya Maridhiano inatarajia kuwasilisha ujumbe kwa Spika wa Bunge Job Ndugai kuomba kuyakutanisha makundi mawili yanayosigana bungeni ili kuleta muafaka wenye tija kwa taifa. Mwenyekiti wa taasisi hiyo Sheikh Sadick Godigodi jana alisema kumeguka kwa Bunge kunakosababishwa na Kambi ya Upinzani kuona inaonewa na maamuzi ya Naibu Spika, Dk. Tulia Akson kunahitaji viongozi wa dini kuingilia kati na kupata suluhu. "Tunatarajia katika Bunge lijalo litakaloanza Septemba kuwasilisha ujumbe kwa Spika ili tupewe nafasi ya kutatua mgogoro huu kwa maana wabunge wote wanatakiwa kuwepo bungeni kuwakilisha matatizo ya wananchi," alisema Sheikh Godigodi. "Haiwezekani kundi moja likawa nje na jingine likaendelea, tunahitaji maridhiano ya pande zote mbili za muhimili huo.” Kambi ya Upinzani Bungeni ilisusia vikao vya Bunge la Bajeti kwa zaidi ya siku 70 kupinga kile kilichoita kuburuzwa na Naibu Spika katika uendeshaji wa chombo hicho cha kutunga