Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2016

Wema Sepetu Awashukuru Waliomtumia Salamu za Birthday

Picha
Jumatano hii ilikuwa ni siku ya kuzaliwa ya staa wa filamu Wema Sepetu ambao ndugu, jamaa pamoja na marafiki walimtakia heri na mafanikio mrembo huyo. Moja kati ya vitu ambavyo vilileta gumzo kwenye mitandao ya kijamii ni baada ya mama Diamond kum-wish malkia huyo wa filamu huku akimkaushia Zari ambaye ni mama watoto wa Diamond. Pia dada zake na Diamond walim-wish maklia huyo. Baada ya kupokea salamu za watu mbalimbali kutoka katika kila kona ya dunia malkia huyo wa filamu na yeye aliamua kuwashurudu huku akionyesha kile ambacho hakukitarajia. Wema kupitia istagram aliandika: Wow… wow… wow… daah.. sijui cha kuandika.. am just out of words… Wema mimi nitamlipa nini Mungu kwa Neema na Baraka zake anazonijalia kila siku…?? Napenda kutoa shukrani zangu za Dhati kwa mumumu wangu, My family, my management, teamkazi wale kwa kufungua dimba last Night with that amazing suprise… alafu sasa huku insta, snapchat, twitter and kila site ambazo mmepost about M

Prof. Lipumba: Sing'oki ng'o. Mimi ni Mwenyekiti halali CUF, Kikao kilichonivua uanachama ni batili

Picha
Katika mahojiano na sauti ya Amerika VOA Swahili jana jioni, Mwenyekiti aliyejiuzulu wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba amesema kuwa yeye bado ni Mwenyekiti halali na kikao kilichomvua uanachama ni batili. Akihojiwa na mwandishi wa habari mahiri Sunday Shomari, Mwenyekiti huyo aliyejiuzulu amesisitiza kuwa yeye bado ni mwenyekiti halali kwa mujibu wa katiba ya CUF na kikao kilichoongozwa na Mhe. Katani huko Unguja ni batili na yeye anaendelea na shughuli za kichama kama kawaida.

ZARI Amuumbua Hamisa Mobetto, Aanika Live Uchafu Wake na Diamond

Picha
Zile tetesi za muda mrefu kuhusu mwanamuziki Diamond Platnums pamoja model maarufu nchini, Hamisa mobeto aka Salome kuvunja amri ya sita huenda zikazaa matunda soon baada ya hivi karibuni mzazi mwenzie ,ambaye pia ni mpenzi wake wa sasa, Zari Hassan ambapo kupitia page yake ya snapchat amepost picha za hereni huku zikiwa zimeambata na ujumbe mzito, ambapo alimtaka mwenye hereni hizo cheap alizozisahau chumbani kwake akazichukue mara moja. Hata hivo kwa mujibu wa wapenda umbea mjini aka team chambua kama karanga waliweza kuzichambua hereni hizo vizuri na kubaini kuwa zilishawahi kuvaliwa na mwanamitindo maarufu nchini Hamisa Mobetto(pichani) aka SALOME. Huenda hii ikawa habari Kali kwa wiki hii, hata hivyo bado Zari hajafunguka chochote kuhusu mmliki wa hereni hizo, wala Hamisa bado hajazungumzia chochote kama ni kweli uchafu huo (kama alivyoita Zari) ni wake au sio

TCRA Yadai Haipendi Kufungia vyombo vya Habari ila Sheria Inawalazimu

Picha
Mamlaka ya Mawasiliano ya Tanzania, TCRA, imesema haifurahii kuvifungia vyombo vya habari bali inavitaka vifuate kanuni na sheria zilizopo. Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Joseph Mapunda, ameyasema hayo akiwa jijini Mbeya. “Hatufurahii vyombo kufungwa, hatufurahii vyombo kupewa adhabu,lengo kubwa ni kuvifanya vyombo viwajibike, kwa mujibu wa sheria viwajibike pia kwa wananchi,viwajibike kwa nchi,” alisema. “Tunasajili vyombo vingi ili viweze kusaidia, kuhamasisha, kuelimisha, na kuhabarisha wananchi sasa litakuwa halina maana,” aliongeza. Hivi karibuni kamati hiyo ilikifungia kwa miezi mitatu kituo cha redio cha Radio 5.

JK Afanya ‘Ukauzu’ Ughaibuni

Picha
RAIS Mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete, amekataa kuzungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani huku msaidizi wake akiwapiga vikumbo waandishi hao ili wasimsumbue ‘bosi’ wake, baada ya kutoka katika mkutano wa 71 wa Umoja wa Mataifa, anaandika Charles William. Mkutano huo ulioanza jana mjini New York, unajadili masuala mbalimbali ikiwemo vita dhidi ya ugaidi pamoja na utolewaji wa misaada zaidi kwa wakimbizi. Mkanda wa video uliopatikana leo, umemuonyesha Dk. Kikwete akitoka katika eneo la mkutano huku wandishi wa habari wakijaribu kumuhoji lakini akikataa na kuendelea kutembea, akiondoka katika eneo hilo. Baada ya Dk. Kikwete kukataa kuhojiwa alionekana akiwatupia maneno waandishi hao. Hata hivyo maneno hayo hayakuweza kunaswa na vinasa sauti vya wandishi hao huku msaidizi wake akiwazuia waandishi hao ili wasiendelee kumsogelea. Haikujulikana mara moja, kwanini Dk. Kikwete alikataa kuzungumza na wandishi wa habari katika eneo la nje ya mkut

MATOKEO YAMPA KIBURI GUARDIOLA, AINGIA MTAANI NA KUJIACHIA NA MKEWE

Picha
  Sasa ulitaka afanye mini? Maana Kocha wa Man City, Pep Guardiola mambo yanamuendea vizuri naye ameamaua kujiachia kiana. jana asubuhi  alionekana akiwa  katikati ya mitaa ya  jiji la Manchester akijiachia na mkewe Cristina Serra. Pamoja na mkewe, Guardiola, kocha wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich aliongoza na kocha wa viungo ambaye ni memba wa benchi lake, Lorenzo Buenaventura. Mwendo wa kikosi cha Man City chini yake unaonyesha uko safi na tayari ameanza kupewa nafasi ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England

Polisi Marekani Yamkamata Mshukiwa wa Shambulio

Picha
Mtu aliyekuwa akitafutwa kuhusiana na mashambulio ya mabomu katika miji ya New York na New Jersey amekamatwa baada ya kushambuliana na polisi kwa risasi. Ahmed Khan Rahami, mwenye umri wa miaka 28 ni raia wa Marekani mwenye asili ya Afghan. Alijeruhiwa katika mapambano hayo yaliyosababishwa kukamatwa kwake karibu na nyumba yake kwenye mji wa New Jersey. Katika operesheni ya kumkamata mtuhumiwa huyo polisi wawili pia walijeruhiwa. Meya wa mji wa New York, Bill de Blasio amesema kuna kila sababu kuamini kwamba shambulio hilo lilikuwa ni ugaidi. Kwa upande wake Rais Barack Obama amewataka watu kuwa watulivu na kuongeza kuwa kila mtu ana mchango katika kuondoa hali hiyo.

ZITTO, Kafulila Wamtwisha Mzigo wa Escrow Rais Magufuli

Picha
Wakati Baraza la Usuluhishi la Benki ya Dunia likitoa hukumu ya kutaka Tanesco kuilipa Benki ya Standard Chartered-Hong Kong (SCB-HK) Sh320 bilioni, wanasiasa wawili walioibua sakata hilo bungeni wamechachamaa wakimtaka Rais John Magufuli awafikishe mahakamani wote waliohusika katika sakata la escrow. Katika hukumu hiyo, Baraza hilo limeitaka Tanesco kulipa mamilioni hayo ya fedha baada ya mgogoro wa muda mrefu kati yake na Kampuni ya Independent Power Tanzania Ltd (IPTL). Uamuzi huo umekuja wakati Serikali ilisharuhusu kufanyika kwa malipo ya Sh306 bilioni kutoka katika akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa imefunguliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa ajili ya sakata hilo kwenda kwa kampuni ya Pan Africa Power Solutions (T) Ltd (PAP). Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji alisema katika shauri hilo, shirika hilo liliwakilishwa na mawakili binafsi kutoka kampuni ya uwakili ya Rweyongeza na ndiyo itakayotoa taarifa kuhusu hukumu hiyo. Maoni y

TAARIFA RASMI KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA IKULU LEO

Picha
Tweet Tweet ? ? at 6:43 PM Email This

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili ya Septemba 18

Picha
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili ya Septemba 18

RAIS Magufuli: Tetemeko Halijaletwa na Serikali, Watu Wafanye Kazi

Picha
Mkuu Anasema waathirika wasikae tu huko wanangoja hela za serikali kwa sbb wanasikia zimechangwa,waanze kujisaidia kwanza wao na serikali itawasaidia pale waliposhindwa. Mkuu anasema mtu ukuta umedondoka, anataka asubiri serikali ndio imtengenezee! Watu wajue tetemeko ni janga la asili halijaletwa na CCM. Waanze kwa kujenga wenyewe kuta zilizodondoka sio wasubiri serikali, sababu maisha yanendelea na watu wanatakiwa wafanye kazi kwa kujenga nyumba zao na sio kila kitu serikali itafanya. Na wale wanasiasa wanaotaka kutumia janga hili kujinufaisha kisiasa mkuu anasema waache mara moja....Na kasema wote wanaotumia janga hili kukusanya misaada kwa njia ya kitapeli, basi wakamatwe mara moja.

Matembezi Dar yakusanya Sh1.5 bilioni za waathirika wa tetemeko Kagera

Picha
TAKRIBANI shilingi bilioni 1.5 zimechangwa kufuatia matembezi ya hisani yaliyopewa jina la “Walk for Kagera” yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kusaidia wahanga wa Tetemeko la Ardhi lililotokea tarehe 10 septemba mwaka huu mjini Bukoba Mkoani Kagera. Akizungumza mara baada ya matembezi hayo Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe Ally Hassan Mwinyi aliwashukuru wadau mbalimbali waliojitokeza na kushiriki matembezi hayo ya hisani. “Nawapongeza sana wadau wote mlioshiriki katika matembezi haya, mmeonyesha mshikamano mkubwa kwa umoja wenu mmeweza kuchangisha jumla ya shilingi 1,502,680,000 hii inatia faraja sana muendelee na moyo huo” Alisema Mzee Mwinyi. Kwa upande wake Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Kagera kuwa Serikali inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha wahanga wa tetemeko hilo wanapatiwa huduma stahiki na kwa wakati. Balozi Kijazi aliongeza kuwa kutokana na kuguswa na tatizo hilo Serikal

KUTOKA BUNGENI: Rais Magufuli Kuhamia Dodoma Rasmi Mwaka 2020

Picha
Leo Septemba 16, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisoma hotuba ya kuahirisha mkutano wa nne kwa Bunge la 11 uliodumu kwa muda wa wiki mbili, amesoma ratiba ya serikali kuhamia Dodoma. “Ili kufanikisha azma ya Serikali kuhamia Dodoma, tayari imeandaliwa ratiba itakayowezesha Serikali kuhamia Dodoma kwa awamu, kuanzia mwezi Septemba, 2016 hadi mwaka 2020, bila ya kuathiri bajeti yetu ya mwaka 2016/2017 kama ifuatavyo”– 1. Septemba 2016 – Februari 2017. Waziri Mkuu na Mawaziri wote, Makatibu Wakuu wote, Manaibu Makatibu Wakuu wote watahamia Dodoma katika Awamu ya Kwanza. Aidha, kila Wizara itatakiwa kuhamisha Watumishi wa Idara moja au mbili, na wakati huo huo kuendelea kuweka utaratibu wa kupeleka Watumishi wa Idara nyingine kuhamia Dodoma; 2. Machi 2017 – Agosti 2017. Kipindi hiki kitawapa fursa watendaji wa wizara mbalimbali kuweka katika Bajeti zao za mwaka 2017/2018 gharama za kuendelea kuhamisha watumishi wake kuja Dodoma. 3. Septemba 20

Malawi Yadai Kuishtaki Tanzania Kwenye Umoja wa Afrika(AU)

Picha
Foreign Affairs and International Cooperation minister Francis Katsaira said Tanzania has released a new Lake Malawi map which shows the east African country has taken a chunk of Lake Malawi, which is potentially rich in oil and gas.. “We have already reported them to the African Union and very soon we will be reporting them to Comesa and Sadc,” he said. Kasaira said Tanzanian authorities have threatened to beat up and arrest Malawians who will disregard the new map. The old map, drawn up by Germany and Britain gives the whole Lake Malawi, except a small part to Malawi. Tanzania has taken much interest in the lake after oil was discovered in the lake popularly known as lake of stars. Katsaira said both Malawi and Tanzania were supposed not to interfere with the Lake Malawi issue as the matter was with the African Union and a mediation team. He therefore said the government is waiting for a response from Tanzsnia on the proposal fo

Namanga: Edward Lowassa asimamishwa na wananchi wamweleze ugumu wa maisha

Picha
Mh Edward Lowassa Mjumbe wa kamati kuu wa chama Cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA ) na Chama kikuu cha Upinzani TANZANIA na Waziri Mkuu mstaafu amesimamishwa na Wananchi wa Namanga Mpakani mwa Tanzania na Kenya .  Wananchi wamemueleza Ugumu na ukali wa Maisha walionayo ikiwa ni pamoja na kudorora kwa mzunguko wa fedha mpakani hapo leo hii akiwa safarini Toka Nairobi Kenya alipokwenda kuhudhuria mazishi ya Marehemu Ole Ntimama.

Gavana BOT Afichua Siri ya Kilio Cha Fedha Kupotea Mtaani

Picha
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu jana alitolea ufafanuzi hali ya kiuchumi nchini huku akieleza siri ya kilio kinachovuma cha fedha kupotea mtaani na nyingine zikidaiwa kufichwa. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Profesa Ndulu alisema kuwa kwakuwa taasisi hiyo ndiyo inayofahamu fedha zote zilizopo benki na zilizopo mtaani, inafahamu kuwa hakuna fedha iliyopotea bali fedha zimepotea kwa watu waliokuwa wanazipata kwa njia ya udanganyifu kwakuwa sasa Serikali imebana mianya hiyo. “Hakuna fedha iliyopotea, Serikali imebana shughuli za watu na ‘mission town’ sasa shughuli zote zinafanywa na Serikali. Hivyo, kwao fedha zimepotea, lakini kwetu hazijapotea,” alisema Profesa Ndulu. Hata hivyo, Profesa Ndulu alikiri kupungua kwa fedha katika mabenki nchini hali iliyopelekea kupunguza kasi ya utoaji mikopo kwa wananchi. Alisema hali hiyo ilitokana na kuhamishwa fedha za mashirika ya umma na taasisi kutoka benki z