Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2015

MAHUJAJI WA 5 KUTOKEA TANZANIA WATHIBITISHWA KUFA HUKO MAKKA

Picha
WATU wasiopungua 700 wamekufa, huku wengine 816 wakijeruhiwa jana jirani na mji Mtakatifu wa Makka walikokwenda kuhiji ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa moja ya nguzo muhimu katika Imani ya dini ya Kiislamu.Kwa mujibu wa Baraza la Taasisi na Jumuiya za Kiiislam nchini, kati ya mahujaji 2,000,000 waliokwenda Saudi Arabia mwaka huu, 1,500 wanatoka Tanzania.Kwa mujibu wa taarifa ya Sheikh Abu Bakari Zuberi Mufti wa Tanzania,  kwa vyombo vya habari amesema tayari wamethibitisha kutokea vifo vya watu watano waliotokea Tanzania miongoni mwao mmoja ni raia wa Kenya na wengine  wanne ni Watanzania.Amesema Watanzania waliotambuliwa hadi jana usiku wametajwa kuwa ni, Mwanaisha Hassan Juma, Mkungwe Suleiman Hemedi na Sefu Saidi Kitimla. Mwanamke mwingine mmoja Mtanzania jina halijaweza kupatikana hadi Alhamisi usiku wakati wakiandaa taarifa hii ambapo raia wa Kenya ametambuliwa kwa jina la Fatuma Mohammed Jama.Kuna taarifa ya mahujaji wanawake wawili ambao hadi Septemba 24

PENZI KWA FLORA ,NAMSHANGAA SANA MBASHA

Picha
Mwimbaji wa muziki wa Injili nchini, Emmanuel Mbasha. MWIMBAJI wa muziki wa Injili nchini, Emmanuel Mbasha ameshinda kesi yake ya ubakaji iliyokuwa ikimkabili, aliyotuhumiwa kumfanyia kitendo hicho msichana aliyekuwa akiwasaidia kazi za ndani ya nyumba yake na aliyekuwa mkewe, Flora Mbasha.Emmanuel Mbasha alidaiwa kufanya kitendo hicho mara mbili kwa msichana huyo, kitu ambacho ni kinyume cha sheria za nchi.   Aliyekuwa mke wa Emmanuel Mbasha, Flora Mbasha. Hata hivyo, baada ya takriban mwaka mmoja na ushee, wa kusikiliza pande mbili, Jamhuri iliyomshtaki na kuwasikiliza mashahidi, hatimaye, mahakama imejiridhisha pasipo shaka kuwa kijana huyo hana hatia! Kwa kuwa mahakama ndicho chombo kinachotafsiri sheria, ni vyema nikimpongeza Mbasha kwa matokeo hayo, kwani vinginevyo alikuwa anakabiliwa na kifungo kisichopungua miaka 30 jela. Kwa umri wake, kama ingethibitika, bila shaka tungemsahau, maana muda huo ni mr

BREAKING NEWS: ALIYEKUWA WAZIRI WA UTUMISI CELINA KOMBANI AMEFARIKI DUNIA

Picha
Habari zilizotufikia jioni hii zinasema kwamba Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Ompeashi Kombani (pichani), amefariki dunia leo huko India alikokuwa akipata matibabu ya saratani. Alikuwa na umri wa miaka 56. Taarifa kutoka ofisi za Bunge zimethibitisha kifo hicho na kueleza kwamba mwili wa marehemu unategemewa kuwasili Dar es salaam siku ya Jumatatu, ambapo Bunge na Serikali zitasimamia maandalizi yote ya maziko na kumsafirisha kwa mazishi nyumbani kwa marehemu huko Mahenge ambako alikuwa Mbunge wa jimbo la Ulanga Mashariki.

LOWASSA ATIKISA SHINYANGA LEO KWENYE HARAKATI ZA KUELEKEA IKULU

Picha
ahama Shinyanga katika viwanja vya Stendi mpya, toka asubuhi Kahama ilisimama kwa muda leo wakimsubiri Mhe. Edward Ngoyai Lowassa, Jumatatu 14/09/2015 Edward Ngoyai Lowassa na James Lembeli wakikabidhiwa mkuki,upinde,mshale na usinga na wazee wa Kahama kuonyesha wao ni viongozi - Kahama leo Jumatatu 14/9/2015 Mama Regina Lowasa Ndani ya Solwa,Shinyanga Leo.

RATIBA YA LOWASSA MTIHANI KWA DK MAGUFULI

Picha
Ratiba za kampeni za wagombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaoonekana kuchuana vikali, Edward Lowassa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kuungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na Dk. John Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), zimeibua mgongano. Hali hiyo imelalamikiwa na CCM ambayo imeitupia lawama Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kwamba imeshirikiana na Chadema kupanga njama hizo. Kufuatia hali hiyo, jana Nec iliingilia kati na kuitisha kikao cha kupitia upya ratiba za kampeni za vyama. Kampeni za vyama ambavyo vinashiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu unaotarajia kufanyika Oktoba 25, zilianza rasmi Agosti 22, mwaka huu baada ya Nec kufanya uteuzi wa wagombea. Kwa mujibu wa taratibu na sheria, kabla ya kampeni kuanza vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi hutakiwa kuwasilisha ratiba zao Nec na baadaye tume hiyo hupanga ratiba ya nchi nzima kujum

ANGALIA NAFASI ZA KAZI NSSF MWISHO WA KUTUMA MAOMBI TAR 14 SEPTEMBA 2015

Picha
VACANCIES RE-ADVERTISEMENT Refer to the Advertisements that appeared on the Guardian and Daily News papers dated 31st August, 2015. The date of submission has changed to 14th September, 2015. Submit your application and relevant documents to Director General, National Social Security Fund P.O.BOX 1322, DAR ES SALAAM, e-mail This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. The National Social Security Fund (NSSF) which is the leading provider of social security services in Tanzania is hereby inviting applications from suitably qualified, dynamic and motivated Tanzanians to immediately fill vacant positions currently existing in the Fund.  BOFYA HAPA KU APPLY 

TUHUMA ZA KUTUMIWA NA CCM, LIPUMBA AANZA KUJISAFISHA, SOMA HAPA ALICHOSEMA

Picha
Mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Wananchi CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema wanaodhani wanatumika CCM wamekosa mwelekeo kwani alikuwa kinara wa kuitaka itoke madarakani. Profesa Lipumba aliyekuwa mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), alijiengua kwenye wadhifa huo kwa kile alichodai nafsi yake itamhukumu kwa kumkaribisha kundini, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa. Lowassa aliyejiunga na Ukawa Julai 28, amepitishwa na vyama vya Chadema, NLD, CUF na NCCR-Mageuzi kuwania kiti cha urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25. Akizungumza juzi usiku kwenye mahojiano maalumu na Kituo cha Televisheni cha Azam, Profesa Lipumba alisema wanaosema wanatumika hawana hoja kwa kuwa walipambana kuitoa CCM madarakani. “Hivi inaingia akilini kweli? Unapambana kuitoa CCM madarakani halafu hao hao uliokuwa unawapiga, wakutumie kuitetea?,” alihoji Profesa Lipumba. Akizungumzia msimamo wake, Profesa Lipumba alisema dhamira yake inamsuta kuendelea kubaki ndani