Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2016

Je, Tundu Lissu Anajijenga ili Kugombea Urais 2020?

Picha
Hii ni kama strategy ya ukawa kujenga mgombea wake kwa mwaka 2020, baada ya kuone appointment ya Katibu mkuu kukosa mwito ndani na nje ya muunganiko huo. Kauli na matendo ya Lisu yanaonyesha muelekeo wa kujijenga kisiasa kwa lengo la kugombea nafasi hiyo. Ikumbukwe kwamba bado kuna pingamizi za ndani kwa ndani ukawa kama Lowasa atasimama kwa tiketi hiyo ifikapo uchaguzi mkuu, hii ni kutokana na yeye kuzidi kupungua ushawisi ukilinganisha na kipindi cha uchaguzi wa 2020. Saikolojia ya mwanadamu unaonyesha kwamba mtu anayekipinga kitu flani sana either anakipenda sana au anahisi kama aliyenacho hastahili kuwa nacho isipokua yeye. Saikolojia hii ndogo inapelekea wengi wetu kuanza kunyanyua kope za macho na kujiuliza nia halisi ya Lisu baada ya kuona na kusikia haya aliyoyafanya hivi karibuni. Je huu ndio mwanzo wa safari ya kugombea nafasi hiyo 2020, na mwendelezo wa matukio toka kwa mwanasiasa huyo?

Suluhisho Rahisi Kwa Wanaodhani Wamepungukiwa Nguvu, Wanaosumbuka Kurudia Tendo au Kuwahi Kufika

Picha
Inavyoonekana siku hizi japo kweli kuna tatizo la upungufu wa nguvu za kiume haswa kwa mazingira ya mijini, Lakini hili tatizo linaonekana kukuzwa kuliko lilivyo hadi imepelekea woga mkubwa kwa baadhi ya wengi wetu. Kwa kuanzia yafuatayo yaweza kusaidia kuboresha kulifurahia tendo la ndoa zaidi na kwa muda zaidi. Kuuweka Mwili vizuri: Ni wazi kuwa tendo hili linachagiwa sana na mzunguko mzuri wa damu. Mwili ukiwa kwenye hali nzuri kiafya na tendo huwa linaenda ipasavyo. Na mwili ukiwa dhoofu basi tegemea tukio dhoofu pia. Hivyo ukitaka kuwa na matokeo mazuri kwenye ndoa yako, jitahidi sana kujiweka vizuri kwa kula sahihi na kufanya mazoezi mepesi mepesi tu kwa wale wanaoweza kuutumia muda vizuri wapiti pite Gym walau siku mbili na kuendelea kwa wiki. Kufahamu kuwa kupumzika kwa uume baada ya baada kufika mara ya kwanza sio tatizo. Kwa wanaume walio wengi, baada ya mshindo wa kwanza hupumzika kidogo kabla ya kuendelea na awamu nyingine. Japo kuna am

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya June 30, Ikiwemo ya Magufuli Kamnasa Mwizi wa Mil 7 Kila Dakika.

Picha
SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya June 30, Ikiwemo ya Magufuli Kamnasa Mwizi wa Mil 7 Kila Dakika

Hifadhi Kubwa zaidi ya Gesi ya Helium yagunduliwa Tanzania

Picha
Tanzania ni miongoni mwa mataifa chache duniani yaliyojaliwa kuwa na rasilimali na madini mengi. Na baada ya kugunduliwa kwa gesi asili huko Mtwara na dhahabu sasa watafiti kutoka Uingereza wamegundua hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi adimu zaidi ya Helium nchini Tanzania. Watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford na kile cha Durham kwa ushirikiano na wataalumu wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban futi bilioni 54 za gesi hiyo ya barafu kama inavyofahamika. Ugunduzi huo umefanyika katika eneo la bonde la ufa la Tanzania. Katika taarifa kwa wanahabri huko Japan, watafiti hao wanasema kuwa uhaba wa gesi hiyo kote duniani ulikuwa umesababisha taharuki haswa kwa madaktari ambao wanatumia gesi hiyo adimu kuendesha mashine za utabibu zijulikanazo kama MRI scanners, mbali na kutumika katika mitambo ya kinyuklia miongoni mwa sekta zingine nyingi za kawi na teknolojia. Kabla ugunduzi huo watafiti walikuwa wamebashiri ukosefu wa gesi hiyo baridi i

VIDEO: Goli la mechi ya Yanga vs TP Mazembe June 28 2016, Full Time 0-1

Picha
June 28 2016 klabu ya Dar es Salaam Young Africans ilicheza mchezo wake wa pili wa Kundi A wa Kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, katika mchezo huo Yanga ilifungwa goli 1-0, goli amble lilifungwa na Merveille Bope dakika ya 74.

FFU Jela Miaka 30 kwa Kubaka Mwanafunzi, Pia Atalipa Faini ya Milioni 15 na Viboko 12 Seebait.com 2016

Picha
ASKARI wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Raphael Makongojo (25) aliyembaka aliyekuwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Korogwe amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela. Pia Makongojo amepewa adhabu kali, ikiwemo viboko 12 pamoja na kuamriwa kutoa faini ya Sh milioni 15 mara atakapomaliza kifungo chake. Hukumu hiyo iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya ya Arusha ndani ya chumba cha faragha (chemba) ambako waandishi hawakuruhusiwa kusikiliza hukumu, lakini baadaye waliambiwa kwa sharti la hakimu wala waendesha mashtaka kutajwa majina yao kwa sababu kesi hiyo iliendeshwa faragha. Awali kesi hiyo ilianza kwa mshitakiwa kusomewa maelezo yake ya awali akituhumiwa kumbaka mwanafunzi wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Korogwe ambaye hivi sasa amemaliza masomo. Awali askari huyo alishushwa pamoja na mahabusu wenzake mahakamani hapo, lakini kwa kuwa kesi inayomkabili ni ya ubakaji hivyo inasikilizwa ndani ya chumba cha faragh

Utajiri wa Diamond Umefikia Shilingi Bilioni 8.6

Picha
Kumekuwepo na tetesi nyingi kuhusu utajiri wa Diamond umefikia kiasi gani. Hilo ni swali ambalo hajawahi kulijibu kwa uhakika zaidi ya kutoa tu hints na kuwaacha wanaouliza kubaki na majibu yao wenyewe vichwani. Lakini kupitia kipindi maalum cha kituo cha runinga cha E!TV, E Vip kilichorushwa Jumapili ya June 26, tunaweza kusema walau kwa uhakika staa huyo ana utajiri mkubwa kiasi gani. Diamond ana utajiri wa dola milioni 4 za Kimarekani ambao kwa shilingi ya Tanzania ni zaidi ya bilioni 8.6. Si kitu kinachoshangaza tena kwa Diamond kutokana na hatua aliyofikia akiwa msanii anayelipwa fedha nyingi zaidi Tanzania kwa sasa. Fedha zake nyingi zinatokana na show zake zisizokauka za ndani na nje ya nchi, mikataba ya ubalozi na matangazo kutoka makampuni kama Vodacom, Cocacola, DSTV na Red Gold. Hivi karibuni alipata deal jingine la kutangaza huduma ya taxi ya Uber. Pia amekuwa akiingiza fedha nyingi kupitia biashara ya nyimbo zake hasa miito ya simu, ma

Atakayempachika Mimba Mwanafunzi Kifungo cha Miaka 30 Jela

Picha
BUNGE limepitisha kwa kauli moja Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Namba 2 ya mwaka 2016 ambayo pamoja na mambo mengine, imeongeza adhabu kwa watu wanaowapa mimba au kuoa ama kuolewa na mwanafunzi, sasa watafungwa jela miaka 30. Sheria hiyo ilipitishwa jana bungeni mjini Dodoma baada ya Muswada kuwasilishwa Juni 24, mwaka huu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) ambao baadhi ya wabunge walipata fursa ya kuuchangia. Muswada huo ulilenga kufanya marekebisho katika sheria 21 kwa lengo la kuondoa mapungufu yaliyobainika wakati wa utekelezaji wa sheria hizo na umepitishwa kuwa sheria. Sheria zilizopendekezwa kurekebishwa na sheria hiyo ni pamoja na ya Kudhibiti Utakatishaji wa Fedha Haramu; Kudhibiti Usafirishaji Haramu wa Binadamu; Kanuni za Madai; Usajili wa Makandarasi; Elimu; Ajira na Mahusiano Kazini na Sheria ya Taasisi za Kazi. Muswada huo uliowasilishwa bungeni na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju unatamka adhabu ya kifungo c

Utafiti Umeonyesha Kumbe Marubani wa Ndege Huwa Wanapitiwa na Usingizi Wakiwa Angani Wakiendesha Ndege

Picha
Between 43% & 54% of pilots surveyed in the U.K.,Norway, and Sweden admitted to have fallen asleep while flying a passenger plane. One third of them stated that when they woke up, they discovered that their co-pilots had also fallen asleep.

Ugonjwa Usiofahamika Ulioibuka mkoani Dodoma Na Kuwaathiri watu 32 Wafahamika

Picha
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amesema ugonjwa usiofahamika ulioibuka mkoani Dodoma, unatokana na sumukuvu inayopatikana kwenye nafaka. Akizungumza jijini, Dar es Salaam jana, Ummy alitolea ufafanuzi kuhusu ugonjwa huo na kuongeza ndani ya wiki moja, kumekuwa na ongezeko la wagonjwa 11 na kufanya jumla ya wagonjwa kufikia 32, ingawa idadi ya vifo haijaongezeka. Alisema majibu kuhusu ugonjwa huo yanatokana na uchunguzi wa awali uliofanywa na Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) na kwamba serikali imechukua nafaka kadhaa zinazopatikana mkoani Dodoma ili kuzipeleka Atlanta, Marekani kwa uchunguzi zaidi. “Tulitoa taarifa ya kuwepo kwa ugonjwa huo Juni 19 mwaka huu ambao ulipatikana wilaya za Chemba na Kondoa, kulikokuwa na wagonjwa 21 na vifo saba, hata hivyo mpaka kufikia juzi wagonjwa waliokumbwa na ugonjwa huo wameongezeka na kufikia 32 na idadi ya vifo imebakia saba,” alisema Ummy. Alisema katik

Majina ya Wakuu wa Wilaya wapya walioteuliwa na Rais Magufuli Leo Haya Hapa

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya mabadiliko madogo katika safu ya wakuu wa mikoa na amewateua wakuu wa wilaya 139. Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika mabadiliko hayo Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Bi. Zainab R. Telack kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Bi. Zainab R. Telack anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Anna Kilango Malecela ambaye uteuzi wake ulitenguliwa. Rais Magufuli pia amemteua Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma. Dkt. Binilith Satano Mahenge anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabit Mwambungu ambaye amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es salaam ambako atapangiwa majukumu mengine. Aidha, Rais Magufuli amemteua Dkt. Charles F. Mlingwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara. Dkt. Charles F. Mlingwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na B

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya June 24, Ikiwemo ya Magufuli Vitani na Ukawa...

Picha
SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya June 24, Ikiwemo ya Magufuli Vitani na Ukawa...