Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2016

Lema Amjibu Waziri Mwigulu. Asema Yupo Tayari Kufa Akipigania Haki Operation Ukuta

Picha
Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini amemjibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba kuwa Arusha tumejiandaa vyema kwa ajili ya Operesheni UKUTA, na kwamba Mwigulu siyo wa kwanza duniani kutoa lugha za vitisho duniani. Lema amesema kuwa tumejiandaa kufa ama kuuawa na Jeshi la Polisi wakipigania haki na kuikumbusha serikali kuacha kuvunja katiba ya nchi ambayo Rais na viongozi wote waliapa kuilinda. Mh Lema ameyasema hayo kumjibu Mwigulu Nchemba aliyesema anawaonya chadema wasitingishe kiberiti, kwamba viberiti vingine vimejaa gesi. Lema amesema kuwa kauli za hovyo zinazotolewa na serikali zinaweza kuingiza nchi kwenye machafuko. Amesema Farao Mungu alimfanya moyo wake uwe mgumu ili Apate kujitukuza mbele ya wana Israel, na kinachoonekana hivi sasa ni kwamba Mungu ameufanya moyo wa Magufuli kuwa mgumu ili Tanzania ili iweze kukombolewa. Lema amesema kuwa hatumjaribu mtu bali wakati wa kuandamana bali tunatetea utaw

Soma Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Katika Magazeti na Mitandaoni leo 18 Aug 2016

Picha
Hapa Chini Nimekuwekea Nafasi za kazi Mbali Mbali zilizotangazwa leo katika Magazeti na Mitandaoni, Bonyeza Links Job Opportunities at Acacia Mining, Application Deadline: 26 Aug 2016 Job Opportunity at Sun Share, Application Deadline: 24 Aug 2016 Job Opportunity at Serengeti Breweries Limited (SBL), Serengeti Breweries Limited (SBL) Job Opportunity at Tanzania Postal Bank (TPB), Application Deadline: 25 Aug 2016 Job Opportunity at Four Seasons Hotels and Resorts, Application Deadline: 22 Aug 2016 Job Opportunity at 7Skyee Consultancy Private Limited, General Manager - Treasury Job Opportunity at 7Skyee Consultancy Private Limited, General Manager (Accounts) Nafasi Zingine Unaweza Kutembelea:  WWW.AJIRAYAKO.COM

Ni Kosa Kumwangalia Mwanamke Kwa Sekunde 14 Nchini India

Picha
Watumiaji wa mitandao ya kijamii wamelalamika kuhusu tamko la afisa mmoja aliyesema kuwa ni kinyume na sheria kumuangalia mwanamke kwa zaidi ya sekunde 14 katika jimbo la Kerala nchini India. Hakuna sheria kama hiyo nchini India lakini afisa huyo Rishiraj Singh ambaye ni kamshna amesema kuwa kumuangalia mwanamke kwa mda mrefu kunaweza kukutia mashakani. Watu mitandaoni wanauliza itakuwaje iwapo mwanamume atafunga jicho mara moja na kulifungua akimwangalia mwanamke wakiongezea kuwa huenda bei ya miwani ya kujilinda dhidi ya jua ikapanda. Lakini wengine wanasema kuwa bwana Signh amezua hoja nzuri sana kuhusu usalama wa wanawake. ”Mtu anaweza kushtakiwa kwa kumuangalia mwanamke kwa sekunde 14”,alisema bwana Singh katika eneo la Kochi siku ya Jumamosi. Tamko hilo lililofanywa katika kanda ya video limesambaa katika jimbo hilo na kuzua ucheshi miongoni mwa mitandao ya kijamii. Source:BBC

Mwanamke Akikujibu Hivi Achana nae Haraka Sana Ujue Hakuna Kitu Hapo....

Picha
Wanawake wa uswahilini wa siku hizi wamekuwa na swagger ya aina moja wanapotongozwa.utasikia "MIMI NAWAOGOPA WANAUME",ukiuliza wewe ni bikra kwani? Atajibu hapana,ukiuliza kwa nini unawaogopa wanaume wakati we sio bikra atakujibu" NISHATENDWA SANA".ndugu yangu nakushauri,kama ukijibiwa hivo basi ondoka fasta ujue hapo hakuna mwanamke kabisa,kwa sababu haiwezekani mtu atendwe yeye tu na kila mwanaume,ujue huyo ana mapungufu ambayo hata wewe hutaweza kuvumilia ,mapungufu ambayo hata wewe utamtenda tu na mwisho wa siku utamuongezea idadi ya wanaume waliomtenda.ila mara nyingi wanawake wanaojibu hivo au wanaotendwa hivo unakuta ni hawajatulia kabisa(vicheche).

Wenye Akaunti ‘Feki’ Mitandaoni kukiona - TCRA

Picha
MAMLAKA ya Udhibiti wa Mawasiliano hapa Nchini (TCRA) imewaonya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaojisajili katika mitandao hiyo kwa kutumia majina na taarifa za uongo, anaandika Charles William. James Kilaba Kaimu Mkurugenzi wa TCRA amesema, vitendo vya watu kujisajili katika mitandao ya kijamii kwa kutumia majina na taarifa zisizo sahihi, ni kosa kisheria na kwamba wanaofanya hivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria. Kilaba ameyasema hayo leo, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuongeza ufahamu kuhusu matumizi sahihi na salama ya mitandao ambayo inasimamiwa na Kitengo cha dharura cha kuitikia matukio ya usalama kwenye mitandao hapa nchini (TZ-CERT). “Tumeamua kuzindua kampeni hii ili kuwasaidia wananchi kuepuka makosa ya kimtandao na kuepuka kufanyiwa utapeli au wizi mitandaoni kwa sababu matukio mengi ambayo yamekuwa yakiripotiwa au kulalamikiwa yanazuilika kwa watu kupewa elimu ya matumizi sahihi ya mitandao,” amesema Kilaba. Kampeni hiyo

Magufuli: Nataka Kutengeneza Tanzania Mpya

Picha
RAIS John Magufuli amewaambia wananchi wa Sengerema mkoani Mwanza na Watanzania kwa ujumla kuwa wana deni kubwa kwake baada ya kumchagua kwa kura nyingi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, lakini akawaahidi kuwa hatawaangusha na anataka kutengeneza Tanzania mpya. “Nataka niwaeleze deni limebaki kwetu, nyie mmemaliza kazi yenu. Deni ni ahadi nataka niwaahidi kama nilivyokuja kuwaomba kura sitawaangusha, nataka kutengeneza Tanzania mpya,” alisisitiza Rais Magufuli huku akiwataka wananchi kuendelea kuiamini serikali yake, kwa kuwa iko pamoja nao. Aidha, Rais Magufuli alisisitiza suala la watendaji wa serikali, kuacha kuwanyanyasa wananchi wanyonge, na badala yake wahangaike na mafisadi na wafanyabiashara wakubwa wanaokwepa kodi, badala ya kuwatoza ushuru wanyonge. “Kusanyeni kodi kwa wafanyabiashara wakubwa na sio kwa wananchi wanyonge,” alisema Rais Magufuli na kupiga marufuku kwa halmashauri kuwatoza ushuru wakulima wanaosafirisha mazao yao kutoka s

Sakata la Supu ya Pweza Latolewa Ufafanuzi..Utafiti Kama Kweli Inaongeza Nguvu za Kiume Bado Waendelea

Picha
Akizungumza na East Africa Radio katika kipindi cha East Africa Break Fast Prof. Kaale amesema taarifa za utafiti wa wanafunzi wa Muhimbili bado haujakamilika kwani umeishia katika hatua ya wanyama panya na majaribio kabla hayajaenda kwa binadamu lazima yafanyike kwa wanyama wenye mfumo unaofanana kwa kiasi fulani na binadamu. "Mwanafunzi alinunua pweza akamchemsha mwenyewe, akawapa panya mchuzi akawafuatilia kwa muda wa siku 29 na aliwatenga panya katika makundi mawili kundi moja likapewa maji na lingine likapewa mchuzi wa pweza na mfumo wa ‘genetics’ unafanana sana na binadamu kwa zaidi ya asilimia 95 lakini hatuwezi kusema kwamba umethibitishwa kwa binadamu bila hatua zote kukamilika" Amesema Prof. Kaale Prof. ameendelea kufafanua kwamba waliopewa supu walionekana kufanya tendo la kujamiiana mara nyingi kuliko wale waliopewa maji hivyo kisayansi huwezi kusema moja kwa moja kwamba tayari na kwa binadamu supu hiyo inaweza kufanya kazi.