BRAZIL KUMEKUCHA! Dunga ndiye kocha mpya, je! atafanya nini copa America 2015 huko Chile?

Dunga ndiye kocha wa Brazil
Shirikisho la soka la Brazil CBF limemtangaza aliyekuwa mchezaji wa Brazil Dunga kuwa kocha wa timu ya taifa kwa mara ya pili.
Dunga aliyeiongoza Brazil kutwaa kombe la dunia la mwaka wa 1994 aliwahi pia kuwa kocha katika mwaka wa 2006 hadi 2011.
Dunga amechukua pahala pake Luiz Felipe Scolari, ambaye alijiuzulu kufuatia kimbunga cha mabao 7-1 ambayo timu hiyo ililazwa na Ujerumani katika hatua ya nusu fainali .
Dunga ndiye kocha wa Brazil
Sadfa ni kuwa Kocha huyo mwenye umri wa miaka 50 naye alifutwa kazi baada ya selecao kubanduliwa nje ya kombe la dunia la mwaka wa 2010 katika hatua ya robo fainali.
Carlos Alberto Parreira ndiye aliyechukua pahala pake lakini hata naye haku dumu Scolari alipotajwa kuwa Kocha.
Scolari mwenye umri wa miaka 65 aliiongoza Brazil katika semi fainali za kombe la dunia ambapo timu hiyo ilipata kichapo kibaya cha mabao masaba kwa moja dhidi ya mabingwa wa kombe la Dunia Ujerumani.
Dunga ndiye kocha wa Brazil
Dunga amewapiku mkufunzi wa kilabu ya Corinthians Tite,Mkufunzi wa kilabu ya Sau Paulo Muriciy Ramalho na Vanderlei Luxembourg ambaye aliwahi kuifunza timu hiyo kutoka mwaka 1998 hadi mwaka 2000.
Wakati huohuo kocha wa Argentina Alejandro Sabella, 59, amesema kuwa atatangaza hatima yake juma lijalo baada ya kushindwa bao moja kwa nunge na Ujerumani katika fainali ya kombe la dunia huko Brazil mapema mwezi huu .
Wachezaji wanamtaka kocha Sabella kuiongoza timu hiyo katika kipute cha kuwania ubingwa wa mataifa ya Amerika ya Kusini yaani 2015 Copa America mashindano yatakayoandaliwa huko Chile.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

HILI NDILO BIFU KUBWA KATI YA RIHANA NA NICK MINAJ.