Uganda: Wamiliki wa hoteli kuwasilisha taarifa za wateja polisi


Asan KasingyeHaki miliki ya picha
Image caption
Polisi nchini Uganda imetoa sera mpya ya usalama ambayo italazimu wamiliki na mameneja wa hoteli, vyumba vya wageni na maeneo mengine ya kulala kujulisha serikali kuhusu wageni wote ambao wanatumia maeneo yao.
Kulingana na sera hiyo mpya, orodha ya watu ambao wamelala kwenye hoteli yoyote, sasa itahitajika kupelekwa kwenye kituo cha polisi kilicho karibu kila asubuhi.
Asan Kasingye, afisa mwandamizi wa polisi anayesimamia polisi ya kijamii anasema orodha hizo zitawasaidia kujua kila anayeingia kwenye maeneo tofauti.
''Tunaamua kuandikisha kila mtu kwenye maeneo tofauti. Hata pia wale ambao wanalala na kutumia hoteli. Mamaneja wa hoteli hizi wanafaa kuandikisha watu wote na halafu watupe orodha hizi ili tuzitumie kwenye masuala ya usalama ," Kasingye alisema.
Kabla ya sera hiyo, wamiliki wa nyumba pekee ndiyo waliokuwa wanalazimishwa kupatia orodha ya wapangishaji wa nyumba zao. huwekwa na viongozi wa mitaa mbalimbali na nakala kupewa polisi.
Asan Kasingye, afisa mwandamizi wa polisi UgandaHaki miliki ya pichaUPD
Image caption''Tunaamua kuandikisha kila mtu kwenye maeneo tofauti. Hata pia wale ambao wanalala na kutumia hoteli.''
Polisi pia ilikuwa inafuatilia wateja wa kigeni wanaotembelea hoteli tofauti.
Lakini sasa, kila mteja ambaye jina lake litapatiwa polisi, atachunguzwa na maafisa wa upelelezi ili kujua historia yao ya uhalifu.
Hata hivyo chama la wamiliki wa hoteli nchini Uganda bado hakijajulishwa kirasmi kuhusu sera hii ya usalama, na wanasema wana mpango wa kukutana na kuzungumza kuhusu jinsi sera hii itakavyowaathiri.
''Tunahitaji kukutana kama wamiliki wa hoteli na kujaribu kuelewa sera hii. Sisi tunaunga mkono serikali kwa mambo ya usalama lakini tunachounga mkono haipaswi kuwa katika mgogoro na biashara yetu."Susan Muhwezi ni Mwenyekiti wa chama hicho alisema.
Sera hiyo mpya imezua gumzo miongoni mwa raia wa Uganda huku baadhi yao wakiunga mkono na wengine wakipinga.
Kwa miaka Zaidi ya kumi, polisi ya Uganda imekuwa ikijaribu mikakati tofauti ya usalama kukiwemo mkakati wa polisi ya kijami. Baadhi ya mikakati hiyo imefaulu, lakini ingine ikiwemo mkakati wa kundi la wananchi wanao zuia uhalifu haijafaulu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

HILI NDILO BIFU KUBWA KATI YA RIHANA NA NICK MINAJ.