Je tunachokiona ni mwisho wa uhusiano wa karibu kati ya Israel na Marekani?


Benjamin Netanyahu alifanya uhusiano wake na netanyahu kuwa ajenda muhimu katika kampeni zake za uchaguziHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBenjamin Netanyahu alifanya uhusiano wake na netanyahu kuwa ajenda muhimu katika kampeni zake za uchaguzi
Kulikuwa na kioja wakati wa sherehe ya kuapishwa kwa wabunge wapya nchini Israeli wiki iliyopita.
Ni miezi mitano pekee iliyopita tangu wabunge wapya kuapishwa na kufuatia mkwamo baada ya uchaguzi mwengine ambao haukukamilika - pengine watalazimika kuapishwa upya.
Na kuongezea hilo, hotuba ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu ilidaiwa kuwa mbaya na hivyo basi haikuwafurahisha wengi.
Alionya kuhusu kupigana na Iran mbali na changamoto za kiusalama wakidai kuwa hotuba hiyo haifanani na hotuba za awali zinazokumbukwa tangu siku za vita vya Yom Kippur mwaka 1973.
Maneno yake kulingana na wengi yalionekana na wachanganuzi wengi kama kampeni inayolenga kudhihirisha ni kwa nini anafaa kuongoza taifa hilo licha ya kwamba alishindwa kupata wingi wa kura.
''Wanawake kwa waume, ninawapatia tishio kubwa la Iran'', aliandika mwandishi wa gazeti la Ma'ariv Ben Caspit akimkejeli Netanyahu kuhusu tishio lake la usalama.
Lakini hotuba hiyo pia ilisaidia kuchochea hofu siku ya mkesha wa vita vya Yom Kippur, siku ya Wayahudi inayoadhimishwa kila mwaka ambapo miaka 46 Israel ilikabiliwa na shambulio kutoka kwa Umoja wa majeshi ya mataifa ya Kiarabu.
Je huu ndio mwisho wa uhusiano wa karibu kati ya Israel na Marekani
Katikati ya hofu hiyo ni sera ya rais Donald Trump katika eneo la mashariki ya kati , ambayo inafuatiwa na maswali kuhusu uhusiano wake wa karibu na benjamin Netanyahu.
Waziri huyo mkuu ameufanya uhusiano wake na Trump kama ajenda yake kuu katika kampeni yake ya uchaguzi, akidai kwamba umefanikiwa katika njia muhimu.
Chini ya utawala wake uongozi wa rais Trump umebadilisha sera ya muda mrefu ukitambua Israel kama mmiliki wa haki wa milima ya Golan mbali na kuuhamisha ubalozi wa Marekani hadi Jerusalem.
Hususan bwana Netanyahu anauona uamuzi wa Trump kujiondoa katika mkataba wa kinyuklia wa Iran na kuwa mkali dhidi ya taifa hilo la Kiislamu kama hatua muhimu ya kuilinda Israel dhidi ya uwezo wa Iran unaozidi kupanuka katika eneo hilo.
Chochote bila uungwaji mkono kutoka pande zote mbili sio jambo la kawaida, hivyobasi majibu ya rais Trump katika uchaguzi huo wa Septemba yalionekana kama onyo .
Alisema kwamba ushindani katika uchaguzi huo ulikuwa wa karibu mno na kusisitiza kwamba uhusiano muhimu kati ya Marekani na Israel upo katika mikono ya raia wa Israel na sio mtu binafsi.
'Trump anachukia walioshindwa', ndio kichwa cha habari kilichotamatisha hususan marafiki ambao hawawezi kushinda licha ya msaada wake, walisema.
Je amani kati ya Israel na Palestina itapatikana?
Hapo huenda amepita mipaka , lakini swala hilo linaangazia udhoofu wa bwana Netanyahu ambaye alishindwa kubuni serikali mara mbili.
Katika vita vya miungano ya kisiasa nchini Israel, anajaribu kushikilia wadhfa wake hatua ambayo inaweza kumpatia uwezo wa kukabiliana na mashtaka ya ufisadi yanayomkabili.
Muhimu ni kwamba ajenda kuu ya bwana Netanyahu - Sera ya Iran tayari ilikuwa imeyumbishwa na hatua ya Iran kufuata njia ya kidiplomasia na taifa hilo la Kiislamu.
Pia ilipata pigo kufuatia hatua ya rais Trump kutofungua kucha zake ili kujibu shambulio la Iran dhidi ya hifadhi za mafuta nchini Saudia.
Waisraeli wamekuwa wakisonga mbele kwa nguvu zaidi na waziwazi dhidi ya washirika wa Iran katika mipaka yake kwa lengo la kukomesha kuongezeka kwa makombora ya Iran karibu na mpaka huo.
Lakini shambulio hilo la Saudi lilitoa onyo kwamba iwapo Iran inaweza kuishambulia Saudia moja kwa moja na makombora, basi vilevile inaweza kufanya kama hivyo dhidi ya Israel.
Na Je Israel inaweza kukabiliana na tishio kama hilo bila usaidizi wa Marekani ambaye waanamini amekuwa mwandani wao?
Pigo ambalo Iran iltoa kwa hifadhi za mafuta za Saudia linamaanisha kwamba makombora ambayo yalirushwa kutoka Iran, shambulio ambalo halikujibiwa kivyovyote na utawala wa rais Trump ,linaashiria kuanguka kwa fundisho la usalama ambalo limekuwa likishinikizwa na Netanyahu , ambaye alitegemea maamuzi yake yote kutoka kwa rais Trump ambaye anamtaja kuwa rafiki mkubwa zaidi wa Israel, aliandika Shimon Shiffer katika eneo la Yedhioth Ahronoth.
Onyo hilo limesababishwa na hatua ya Marekani kuondoa vikosi vyake kaskazini mashariki mwa Syria ili kutoa fursa kwa jeshi la Uturuki , hatua inayowacha bila mtetezi wapiganaji wa Kikurdi ambao wamekuwa washirika wakuu wa Marekani.
Kwa mara nyengine uamuzi huo umetoa wasiwasi kuhusu hatua ambazo Marekani inaweza kuchukua ili kuwalinda washirika wake.
''Trump amekuwa mshirika asiyeaminika kwa Israel'', alisema Shiffer.
Ukweli ni kwamba hakuna jinsi ambavyo Marekani inaweza kupunguza usaidizi wake wowote kwa usalama wa Israel.
Lakini baada ya miaka mitatu ya kushirikiana na utawala wa rais Trump , Israel sasa imeanza kuona ukweli kuhusu rais asiyeaminika ambaye hapendelei kutumia uwezo wa jeshi la Marekani, na anaogopa kuhusishwa katika mzozo wa mashariki ya kati, na yeye kama bwana Netanyahu anakabiliwa na vita vya kisiasa nchini mwake ambavyo lazima akabiliane navyo ili kusalia uongozini.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

HILI NDILO BIFU KUBWA KATI YA RIHANA NA NICK MINAJ.