SONG JIANG, MHALIFU WA UCHINA ALIYEJIFICHA PANGONI KWA MIAKA 17 ANASWA HATIMAYE!


Baada ya miaka 17 Song alibainiwa na ndege isiyokuwa na rubani (drone)Haki miliki ya pichaYONGSHAN POLICE
Image captionBaada ya miaka 17 Song alibainiwa na ndege isiyokuwa na rubani (drone)
Polisi nchini Uchina wamemkamata mhalifu ambaye amekuwa akijificha kwa miaka 17, baada ya kutumia ndege zisizokuwa na rubani kubaini pango alimokuwa akijificha.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 63 ,kwa kwa majina Song Jiang amekuwa akitafutwa na polisi baada ya kutoroka jela ambapo alifungwa kwa kufanya biashara haramu ya kuwasafirisha wanawake na watoto, lakini aliweza kutoroka kutoka kwenye kambi ya jela mwaka 2002.
Amekuwa akiishi ndani ya pango dogo na kukata mawasiliano ya aina yoyote na binadamu kwa miaka mingi.

Unaweza pia kusoma:

Polisi katika mji wa Yongshan walipokea taarifa kuhusu ni wapi alipo Song mwezi Septemba , kulingana na maelezo yao katika akaunti yao ya mtandao wa kijamii wa WeChat.
Taarifa hizo ziliwapeleka hadi katika eneo la milima iliyopo nyuma ya mji anakotoka katika jimbo la Yunnan lililopo kusini mashariki mwa Uchina.
Ndege isiyokuwa na rubani ( Drone) ilibaini pango kwenye eneo la milima yenye mteremko mkaliHaki miliki ya pichaYONGSHAN POLICE
Image captionNdege isiyokuwa na rubani ( Drone) ilibaini pango kwenye eneo la milima yenye mteremko mkali
Baada ya kushindwa kumpata katika msako wa kawaida , maafisa walituma ndege zisizokuwa na rubani za ziada ili kuwasaidia maafisa katika msako huo.
Hatimae ndege hizo zilibaini chuma chenye rangi ya kwenye eneo la mtelemko mkali pamoja na taka zilizokuwa kando ya makazi yaliyopo karibu na eneo hilo.
Pando lilikuwa na ukubwa wa mita 2 za mrabaHaki miliki ya pichaYONGSHAN POLICE
Image captionPando lilikuwa na ukubwa wa mita 2 za mraba
Ndipo polisi walipoamua kutembea kwa miguu hadi katika eneo hilo na kumpata song ndani ya pango dogo ambamo amekuwa akiishi kwa miaka.
Kwa mujibu wa polisi , mwanamme huyo amekuwa akiishi kwa kujificha binadamu kwa muda mrefu kiasi kwamba ilikuwa ni vigumu kwakekuwasiliana na maafisa usalama.
Vyombo vya habari vya taifa vimesema kuwa Song alitumia chupa za plastiki kuteka maji kutoka mtoni, na matawi ya miti kama kuni za kuwasha moto.
Baada ya kukamatwa amerudishwa tena gerezani.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

HILI NDILO BIFU KUBWA KATI YA RIHANA NA NICK MINAJ.