KWANINI! WANAWAKE WAJAWAZITO WANAFANYA MAZOEZI RWANDA?


Wanawake wajawazito
Image captionWanawake wajawazito wakiwa katika zoezi la kunyoosha viungo
Washiriki wa mazoezi ya kwanza ya pamoja kwa wanawake wajawawazito wameiambia BBC kuwa wanataka serikali ya Rwanda kuendeleza mpango huo.
Hii ni baada ya zaidi ya wanawake 100 wajawazito kushiriki mazoezi ya Umma ya kunyoosha viungo mjini Kigali.
Waandaaji wa mazoezi hayo wanasema kuwa lengo lao ni kubadili dhana kwamba wanawake wajawazito hawana uwezo wa kufanya hivyo.
Nelson Mukasa ambaye ni kiongozi wa shirika lisilokuwa la kiserikali lililoanzisha mpango huo anasema raia wa Rwanda wanaamini kuwa mwanamke akipata ujauzito hafai kufanya kazi yoyote.
"Watu wanastahili kujua kwamba kutofanya mazoezi ya viungo kwa mama mjamzito ni hatari kwa afya yake na ya mtoto aliye tumboni" - Bwana Mukasa anasema.
Ruth Ntukabumwe ambaye ana ujauzito wa miezi saba anasema kuwa amehudhuria awamu ya kwanza ya mazoezi na angelipendelea kuendelea na mazoezi mengine.
"Ni kitu kizuri sana, nilipofanya mazoezi, nilihisi utulivu na pia mtoto pia amechangamka tumboni jambo lililonifanya kusikia raha sana" - Ruth alisema.
Wanawake wajawazito
Image captionWanawake wajawazito wakishiriki mazoezi ya pamoja ya kutembe mjini Kigali
Faida ya mazoezi kwa mama mja mzito
Kwa mujibu wa wataalamu wa afya ya uzazi wnawake waja wazito wanaweza kufanya mazoezi
Mama mjamzito anashauriwa kufanya mazoezi ya kukimbia kwa muda usio zidi dakika thelathini lakini pia anashauriwa asikimie kwa haraka haraka, au mwendo wa mashindano.
''Usitumie nguvu kubwa katika kukimbia na hakikisha unakunywa maji ya kutosha kabla yakukimbia na baada ya kukimbia maana katika kukimbia kunakupungua maji''anasema Dkt Lucy Nduta dakatari bingwa kinamama kutoka mjini Nairobi Kenya.
Bi Lucy pia nasema kuogelea pia ni aina yazoezi litakalo kumsaidia mama mjamzito kuwa mwepesi zaidi na kupata utulivu.
''Akili itakua katika utulivu na hapa ndio matokeo ya kutokua katika msongo wa mawazo yanapatikana,''aliongeza kusema.
Mtaalamu huyo mia amesema kuwa baadhi ya kinamama wajawazito wanatabia ya kukaa kizembe nyumbani na kuruhusu hali ya kuchoka kuwatala na kua wavivu nyumbani.
Kulala na kuamka au kukaa sehemu sio njia sahihi ya moja ya kumlinda kiumbe ndani yake ila yapo manufaa makubwa sana wakati mama kijacho anafanya mazoezi yakutembea.
''Toka nje tembea,fanya hata matembezi ya jioni, wakati ambapo hakuna jua kali, na tembea barabara ambayo haina mashimo shimo na maporomoko'' ailisema Dkt Nduta
Mwanamke mjamzito
Image caption"Nimechoka kwasababu sijazoea kufanya mazoezi, lakini nimefurahia sana kujumuika na wanawake wajawazito wenzangu " - Bi Uwizeyimana anasema.
Muda mfupi baada ya kufanya mazoezi, Libérée Uwizeyimana ambaye ana mimba ya miezi minane aliiambia BBC kuwa hajawahi kufanya mazoezi akiwa mjamzito.
"Nimechoka kwasababu sijazoea kufanya mazoezi, lakini nimefurahia sana kujumuika na wanawake wajawazito wenzangu " - Bi Uwizeyimana anasema.
Bwana Mukasa amesema wana mazoezi maalum ambayo hayawezi kuwadhuru wanawake hao.
Mazoezi yasioshauriwa kwa mama mjamzito
  • Kubeba vitu vizito kama kunyanyua vyuma vyenye uzito mkubwa.
  • Kulalia tumbo kama njia ya kufanyia mazoezi.
  • Mazoezi yakusimama mda mrefu si rafiki kwa mama kijacho.
  • Epuka mazoezi yenye hatari ya wewe kudondoka kwa usalama wako na mtoto.
  • Usifanye mazoezi yakutumia sana pumzi yako fanya mazoezi kwa kiasi.
Wanaume pia wameshauriwa kushiriki michezo hiyo ili kuwapa motisha wake zao.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

HILI NDILO BIFU KUBWA KATI YA RIHANA NA NICK MINAJ.