MELI YA MAFUTA YA IRAN YASHAMBULIWA KTK PWANI YA SAUDIA.


Wizara ya mambo ya nje ya Iran inadai kuwa meli hiyo imelengwa "mara mbili".Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWizara ya mambo ya nje ya Iran inadai kuwa meli hiyo imelengwa "mara mbili".
Mlipuko uliosababisha moto katika meli ya mafuta ya Iran umetokea karibu na pwani ya Saudi Arabia, vyombo vya habari vya Irania vinasema.
Meli hiyo inayomilikiwa na shirika la kitaifa la mafuta la Iran (NIOC), ilikuwa maili 60 sawa na (km97) kutoka bandari ya Saudia ya Jeddah.
Wizara ya mambo ya nje ya Iran inadai kuwa meli hiyo imelengwa "mara mbili".
Katika miezi ya hivi karibuni visa vya "hujama" vimetekelezwa dhidi ya meli za mafuta za Iran katika bahari nyekundu na kwamba uchunguzi unafanywa alisema msemaji wa wizara hiyo Abbas Mousavi said.
Siku ya Ijumaa vyanzo vya habari ambavyo havikuthibitishwa viliarifu vyombo vya Iran kwamba meli hiyo ililipuliwa kwa makombora ambayo "huenda" yanatoka Saudi Arabia.
Lakini NIOC baadae ilikanusha madai hayo. Ilisema kuwa milipuko miwili tofauti ilitokea katika meli hiyo ambayo ''huenda" imesababishwa na makombora.
Milipuko hiyo haijathibitishwa na taarifa kuhusu meli haijawekwa wazi.
Televisheni ya kitaifa ya Iran awali iliripoti kuwa meli hiyo imetambuliwa kama Sinopa, lakini NIOC baadae ilisema inaitwa Sabiti.
''Sabiti kwa sasa inasafiri kuelekea rasi ya Uajemi,'' Mehr alisema.
Hifadhi mbili za mafuta zimeripotiwa kuharibiwa, hali iliyosababisha mafuta kumwagika katika bahari nyekundu lakini hakuna mtu aliyejeruhiwa..
Picha zinazodaiwa kupigwa siku ya Ijumaa katika meli ya Sabiti zilioneshwa katika televisheni ya taifa ya Iran lakini hazikuonesha uharibifu wowote.
Chanzo katika kampuni ya Windward inayojishughulisha na uchambuzi wa masuala ya baharini iliambia BBC kuwa ni jambo la kawaida kwa meli za mafuta za Iran kuzima AIS ili isionekane - mara kwa mara kuepuka vikwazozo vya kimataifa na unyanyasaji kutoka kwa Saudi Arabia.
Kutokana na sababu za kiusalama meli zote huzima kifaa cha AIS zinapokaribia mfereji wa Suez.
Tukio hili la sasa linajiri wakati kumekuwa na hali ya taharuki kati ya Iran na Saudi Arabia katika siku ya hivi karibuni.
Mwezi uliopita ndege 18 zisizokua na rubani na makombora saba ya meli zilishambulia visima vya mafuta na kituo cha kusafisha mafuta nchini Saudi Arabia, shambulio ambalo Saudia iliilaumu Iran.
Maafisa wa Marekani walisema Iran ilihusika katika mashambulio dhidi ya meli mbili za mafuta katika eneo la Ghuba mwezi Juni na Julai, na pia kushambulia meli zingine nne za mafuta mwezi Mei.
Iran ilipinga madai ya kuhusika na matukio hayo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

HILI NDILO BIFU KUBWA KATI YA RIHANA NA NICK MINAJ.