Abu Bakr al-Baghdadi: Tunachokijua kuhusu uvamizi wa Marekani na mauaji yake Syria


Rais Trump akivihutubia vyombo vya habari kufutia kifo cha Baghdadi
Rais Donald Trump ametangaza kwamba kiongozi aliyekuwa akijificha wa kundi la Islamic State , Abu Bakr al Baghdad alijiuwa mwenyewe wakati wa uvamizi wa kikosi maalum cha Marekani nchini Syria.
Hiki ndicho tunachojua kuhusu operesheni hiyo.

Ni wapi na lini ilitekelezwa?

Katika tangazo la runinga , bwana Trump alitangaza kwamba gaidi huyo nambari moja duniani amefariki wakati wa uvamizi hatari wa usiku kaskazini magharibi mwa Syria na vikosi maalum vya Marekani.
Marekani ilikuwa imetoa kitita cha dola milioni 25 kwa habari kuhusu alipo Abu bakr al BaghdadiHaki miliki ya picha
Image caption
Rais alisema kwamba ndege aina ya helikopta iliokisafirisha kikosi hicho maalum iliondoka kutoka eneo ambalo halikutajwa baada mwendo wa saa kumi na moja saa za Marekani siku ya Jumamosi, wakati yeye na viongozi wengine walikusanyika katika chumba cha Ikulu ya Whitehouse.
Ndege zilisafiri kwa muda wa saa moja na dakika 10 kutoka maeneo tofauti, hiuku opetresheni ya ardhini ikifanyika kwa muda wa saa mbili, aliongezea.
Maafisa waliambia vyombo vya habari nchini Marekani kwamba mapema siku ya Jumapili nchini Syria, vikosi maalum vya Marekani vililenga eneo moja la kijiji cha Barisha mkoani Idlib takriban kilomita 5 kusini mwa mpaka wa Uturuki.
Eneo alilokuwa kiongozi huyo wa Islamic State Syria
Presentational white space
Idlib ndio ngome ya mwisho ya upinzani dhidi ya serikali ya Bashar al Asad.
Inatawaliwa na muungano wa wapiganaji wa Jihad ambao unakinzana na Kundi la Islamic State , lakini mamia ya wapiganaji wa IS wanaaminika kupiga kambi katika eneo hilo.
Jeshi la Syria linaloungwa mkono na Syria lipo mashariki, magharibi na kusini.

Jinsi uvamizi huo ulivyofanyika

Bwana Trump alisema kwamba vitengo vya ujasusi nchini Marekani vilimchunguza Baghdad kwa wiki kadhaa kabla ya operesheni na kwamba walijua eneo hilo lilikuwa na mahandaki kadhaa, huku mengi yakiwa na mwisho wake.
Siku ya Jumamosi , rais aliamrisha ujumbe uliohusisha kundi moja la wanajeshi maalum , ndege nane na meli nyingine nyingi.
Picha zikimuonyesha rais donld Trump na viongozi wengine wa kisiasa na kijeshi wakiwa katika chumba kimoja cha Ikulu ya Whitehouse
Ndege hizo zilipaa juu ya anga ya Uturuki, mbali na maeneo yanayodhibitiwa na majeshi ya Syria pamoja na yale ya Urusi.
Urusi ilishirikiana na kufungua nga yake kwa operesheni hiyo ya Marekani licha ya kutoambiwa kile kilichokuwa kikijiri kulingana na rais Trump.
''Operesheni hiyo ya kuingia na kutoka ilikuwa hatari mno. Kulikuwa na wakati ambapo tungekabiliwa vilivyo'' , alisema .
''Ndege zetu zilipaa chini chini lakini kwa mwendo wa kasi''.
Huku ndege hizo zikikaribia katika nyumba hiyo zilishambuliwa lakini Trump anasema mashambulizi hayo yalimalizwa haraka.
Mkaazi mmoja wa Barisha anasema kwamba ndege hizo za Marekani zilishambulia nyumba mbili na kuiharibu kabisa mojaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMkaazi mmoja wa Barisha anasema kwamba ndege hizo za Marekani zilishambulia nyumba mbili na kuiharibu kabisa moja
Mwanakiji mmoja kutoka eneo la Barisha aliambia BBC kulikuwa na mashambulizi kutoka kwa helikopta hizo kwa zaidi ya dakika 30 kabla ya vikosi vya ardhini kuingia eneo hilo, akiongezea kwamba ndege hizo zilishambulia nyumba mbili na kuiharibu kabisa mojawapo.
Baada ya ndege hizo kutua , wanajeshi hao maalum walilipua mashimo katika kuta ya nyumba hizo ili kukwepa kuingia ndani kupitia mlango wa mbele uliowekwa vilipuzi na baadaye kuanza kuondoa vifusi kulingana na Trump.

Unaweza pia kusoma:

Rais huyo alisema kwamba Baghdad alifariki baada ya kutorokea katika handaki lililo na mwisho, akilia na kupiga kelele.
Hakuna uthibtisho huru wa mauaji ya BaghdadiHaki miliki ya pichaAFP
Image captionHakuna uthibtisho huru wa mauaji ya Baghdadi
Watoto 11 waliondolewa katika nyumba hiyo bila majeraha kufikia wakati huo, huku watu wakisalimu amri na wengine kupigwa risasi.
''Aliyekuwa amesalia alikuwa Baghdadi pekee katika handaki pamoja na watoto watatu'', aliongezea.
''Alifika mwisho wa handaki , huku mbwa wetu wakimfukuza . Alikuwa ameweka vilipuzi katika nguo yake ya ndani na akajilipua na watoto hao watatu''.
''Mwili wake ulikatwakatwa na mlipuko huo huku handaki hilo likiuangukia'' , aliongezea.
Picha na kanda za video kuhusu kilichotokea baada ya uvamizi huo wa Marekani zilionyesha vifusi vya jengo lililoharibiwa pamoja na gari lililochomeka likiwa na mashimo chungu nzima ya risasi.

Kwa nini Marekani ina hakika Baghdadi amefariki?

Bwana Trump amesema kuwa matokeo ya vipimo vya mabaki ya mtu aliyejilipua katika handaki hilo yalionyesha kwamba alikuwa Baghdadi.
Ilichukua takriban muda wa dakika 15 baada ya kufariki.
''Vipimo hivyo vilifanywa na wataalam waliosafiri na vikosi hivyo maalum na walikuwa na sampuli ya vinasaba vya Baghdadi'', aliongezea.
Wataalam hao pia walibeba vipande vya mabaki ya mwili wake katika ndege hizo, kulingana na Trump. Hakujakuwa na uthibitisho huru kuhusu kifo cha Baghdad. Wafuasi wa IS wamekuwa wakionyana kuhusu kuamini tangazo hilo la Marekani.

Je kuna majeraha mengine?

Rais huyo alisema: hakuna hata mwanajeshi ama afisa mmoja wa Marekani aliyeuawa katika operesheni hoyo, huku idadi kubwa ya wapiganaji wa Baghdadi na washirika wao wakifariki naye.
Chombo cha habari cha Jihadi mjini Idlib lkimesema kwamba basi la raia lilishambuliwaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionChombo cha habari cha Jihadi mjini Idlib lkimesema kwamba basi la raia lilishambuliwa
Wake wawili wa Baghdadi ni miongoni mwa waliokufa
Bwana Trump anasema kwamba wanawake hao walipatikana wakiwa wamevalia fulana za ndani zilizowekwa vilipuzi ambavyo havikulipuliwa.
Mbwa wa Marekani alijeruhiwa katika handaki hilo mahala ambapo Baghdadi alifariki , kulingana na Trump .
Haijajulikani iwapo wafuasi wa IS ama watoto waliokamatwa walijeruhiwa.
Bwana Trump alisema kwamba wapiganaji hao kwa sasa wanazuiliwa huku watoto hao wakiwekwa chini ya usimamizi wa mtu ambaye hakutajwa.

Kwa nini Baghdadi alijificha Idlib?

Mji wa Barisha upo mamia ya kilomita kutoka eneo la jangwa lililo mashambani katika mpaka wa Syria na Iraq ambapo Baghdadi aliaminika kujificha.
Bwana Trump alisema kwamba, Baghdadi alikuwa Idlib kwa kuwa alikuwa na lengo la kujenga upya jeshi lake la wapiganaji wa IS baada ya vikosi vya Kikurdi vinvyoongozwa na Marekani kuteka ngome zake za mwisho zilizosalia karibu na kijiji cha Baghuz kilicho mashariki mwa Syria mwezi Machi.
''Hiyo ndio sababu iliomfanya kusalia katika eneo hilo'', rais huyo aliongezea. Hilo ndio eneo muhimu unapozungumzia kujenga upya kundi hilo.
Anasema kwamba ripoti muhimu za kijasusi kuhusu mipango ya siku zijazo ya Baghdadi ilipatikana wakati wa shambulio hilo na kwamba Marekani itamsaka yeyote yule atakayemrithi.
''Tunawajua watakaomrithi. Na tayari tumeanza kuwaaangazia''.

Je Abu Bakr al-Baghdadi ni nani?

Alizaliwa 1971 katika eneo la Samarra nchini Iraq.
Akiwa angali mtoto alidaiwa kupenda sama kusoma Quran na kufuata sheria za kidini, akiwalaumu ndugu zake wasiofutwa vizuri dini ya Kiislamu.
Lakini ilikuwa wakati ambapo alikuwa anafuzu kupata Stashahada ya somo la Quran katika chuo kikuu cha Saddam Husein , ndio wakati alijihusisha na msimamo mkali wa kundi hilo.
Mwisho wa mwaka 2000 alikuwa ameanzisha kundi linalofuata sunna na aliendelea hadi kushirikishwa na kundi la al-qaeda nchini Iraq ambapo kundi la Islamic state lilibuniwa.
Tangu 2014 amesalia mkimya kwa muda mrefu huku kukiwa na uvumi wa kifo chake ambao haujathibitishwa.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

HILI NDILO BIFU KUBWA KATI YA RIHANA NA NICK MINAJ.