BI HARUSI AFA MAJI, SELFIE YAMPONZA NA KUTELEZA KWENYE MAPOROMOKO!


Bwawa la Amaravathi Dam, wilaya ya Coimbatore, Tamil Nadu, India
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionJimbo la Tamil Nadu lina mabwawa mengi ambayo huvutia wageni wengi
Wanandoa wawili wapya na watu wengine watatu wa familia yake walikufa maji katika bwawa moja la maji baada ya kujaribu kupiga picha ya selfie, kulingana na maafisa wa polisi kutoka jimbo la kusini mwa India la Tamil Nadu.
Waliokufa ni miongoni mwa watu sita walioshikana mikono na kusimama katika kina cha maji marefu karibu na bwawa la Pambar kabla ya mmoja wao kuteleza, na kujaribu kumuokoa mwengine.
Mume wa mwanamke huyo aliweza kumuokoa dadake lakini wengine wakafa maji. India ina idadi kubwa ya watu wanaofariki kutoka na vifo vya selfie.
India iliripoti vifo vya watu 259 kati ya 2011 na 2017 kulingana na utafiti uliofanywa na shirika la maabara ya tiba nchini Marekani. Inafuatiwa na Urusi, Marekani na Pakistan
Katika jimbo la Tamil Nadu siku ya Jumapili . Wanandoa hao wachanga , kutoka eneo la Bargur katika eneo la Krishnagiri, walikuwa wakiwatembelea watu wa familia yao katika eneo la Uthangarai pamoja na dadake bwana harusi , kulingana na gazeti la Hindu.
Watatu hao waliingia katika maji hayo pamoja na vijana watatu wa familia moja , kabla ya mmoja wao mvulana mwenye umri wa miaka 14 kuteleza na kuwashika dada zake wawili mmoja wao akiwa na miaka 18 na mwengine wa miaka 19, pamoja na wanandoa hao wawili na dadake bwana harusi
Dada huyo alivutwa na nduguye lakini wengine wanne wakapotea ndani ya maji. Maafisa wa polisi wanasema kwamba miili yao baadaye ilipatikana na uchunguzi kufanywa.
Ni kisa cha hivi karibuni miongoni mwa msururu wa vile vya kupiga selfie nchini India. Wataalam walionya kwamba watu wanafanya hatari ili kuwafurahisha watu wa familia zao katika mitandao ya kijamii.
Katika jimbo la Haryana mnamo mwezi Mei , vijana watatu waliokuwa wakipiga picha za selfie katika reli waliruka kutoka katika njia ya barabara hiyo ya treni walipoona gari hilo likikaribia walikokuwa, kabla ya kuuawa na treni nyengie iliokuwa inajiri kutoka upande mwengine wa reli.
Mwaka 2017, Jimbo la India la Karnataka lilizindua kampeni ya kuwaonya watu kwamba selfie zinaweza kuua baada ya kifo cha wanafunzi wanne.
Mwaka huohuo, mtu mmoja alifariki katika eneo la Odisha wakati ndovu ambaye aliuwa akipiga selfie naye alimkamata na kumpiga na chini.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

HILI NDILO BIFU KUBWA KATI YA RIHANA NA NICK MINAJ.