Meghan Markle: ''Nilionywa kuhusu kufunga ndoa na mwanamfalme Harry''


Meghan, Harry and Prince WilliamHaki miliki ya pichaAFP
Mwanamfalme William wa Uingereza ana wasiwasi kuhusu nduguye baada ya kuzungumzia kuhusu afya yake ya kiakili katika kipindi kimoja cha runinga , kulingana na chanzo cha Jumba la Kensington.
William amedaiwa kutumai kwamba nduguye mwanamfalme Harry ne Mkewe wako katika hali nzuri baada ya kuambia chombo cha habari cha ITV kwamba wanakabiliwa na shinikizo.
Chanzo hicho kimesema kwamba kuna uwezekano kwamba wanandoa hao walikuwa katika eneo dhaifu.
''Jumba la Kensington halikuwa na maoni yoyote kuhusu filamu hiyo ya ITV , ambayo ilienda hewani siku ya Jumapili''.
Kipindi hicho kilifuatilia ziara ya wanandoa hao walipokuwa kusini mwa Afrika mapema mwezi huu.
Katika mahojiano, wanandoa hao walisema kwamba wanakabiliwa na shinikizo la mara kwa mara la kuchunguzwa na vyombo vya habari vya Uingereza.
Chanzo hicho cha jumba hilo kilipinga madai kwamba mwanamfalme Harry alikasirishwa na nduguye baada ya makala hayo kwenda hewani siku ya Jumapili.
Hatua hiyo inajiri baada ya mwanamfalme Harry kukiri kwamba yeye na William wana ''siku nzuri'' na ''siku mbaya''.
Alipoulizwa kuhusu ripoti za vyombo vya habari kuhusu mgogoro kati ya ndugu hao, William alisema mambo mengine hutokea na hiyo husababisha familia kuwa na shinikizo kama hali ilivyo.
Aliongezea: Sisi ni ndugu na tutaendelea kuwa ndugu. Kwa sasa tuko njia panda lakini nitamsaidia kwa vyovyote vile kwa sababu najua atakuwepo kunisaidia pia yeye.
Presentational grey line

Uchanganuzi wa Jonny Dymond

Mapema leo vyanzo viliambia BBC kwamba Mwanamfalme William alikuwa amekasirishwa na nduguye kuhusu mahojiano aliofanya.
Chanzo chengine katika Jumba la kifalme la Kensington kilisema kuwa huo sio uelewa wake wa tabia ya mwanamfalme Harry. Badala yake afisa huyo alitiiliwa shaka na tabia ya wanandoa hao.
Mahojiano hayo yalibaini watu wawili waliokuwa katika shinikizo kali , shinikizo ambayo walikuwa wamejiandaa kutangaza kwamba Harry anakabiliwa na tatizo la kiakili, anahisi kufuatwa na kivuli cha mamake, Diana, Bintimfalme wa Wales katika maisha yake.
Vibaya zaidi ni kwamba historia inajirejelea - kwanza vyombo vya habari vilimuingilia mamake, na sasa anafikiria mkewe analengwa. William anauona ulimwengu tofauti.
Wakati mmoja pia yeye aliviona vyombo vya habari kama vinavyoingilia watu na vyenye nguvu sana.
Ni mojawapo ya sababu kwa nini ndugu hao wawili wameenda njia panda. Lakini swala kuu sasa ni hofu iliopo kwa Harry na Meghan- Wanaonekana kuwa peke yao.
Presentational grey line

Hali sio shwari sana

Meghan mwenye umri wa miaka 38 alisema katika makala hiyo kwamba kuingiliana na masiha ya kifalme imekuwa vigumu kwake.
'' Nilipokutana na mume wangu tulikuwa na furaha kwa sababu nilikuwa na furaha tele'', alisema. ''Lakini marafiki zangu wa Uingereza walinishauri, 'Nina hakika ni mtu mzuri lakini magazeti ya Uingereza yatakuharibia maisha yako''.
Harry na Meghan Marcle
Alipoulizwa kuhusu mwanahabari wa ITV Tom Bradby iwapo ilikuwa sawa kusema kwamba hakuwa salama, bintimfalme huyo alisema : Ndio.
Mwanamfalme Harry , 35 alielezea afya yake ya akili na jinsi anavyokabiliana na shinikizo ya maisha yake kama kitu kinachohitaji kuchukuliwa hatua ya haraka.
Alisema: Nilifikiri kwamba sitajumuishwa lakini mara tu kila kitu kikaanza na hiki ni kitu ambacho ninahitaji kukiangazia.
Mojawapo ya kazi hii ni kuonyesha kwamba una ujasiri, lakini kwangiu na mke wangu kuna mengi yanayoniumiza moyo hususan iwapo mengi yanayosemwa sio ya kweli.
Ndugu hao wa Ufalme wa Uingereza kwa pamoja walifanya kampeni ili kusaidia kuanzisha mazungumzo kuhusu afya ya kiakili.
Mwaka 2017, waliongoza mchango wa hisani ambao walianzisha kukabiliana na unyanyapaa katika afya ya akili.
Mwanamfalme William, Binti mfalme Katherine na mwanamfalme Harry katika kuongoza mchango wa watu wanaokabiliwa na afya ya kiakiliHaki miliki ya pichaPA MEDIA
Mnamo mwezi Mei mwaka huu, wanawafalme hao pamoja na wake zao walishirikiana kuanzisha ujumbe wa simu kwa wale wanaokabiliwa na tatizo la afya ya kiakili
Matamshi ya mwanamfalme Harry kuhusu shinikizo ya vyombo vya habari yanajiri huku yeye ne mkewe wakitafuta njia za kuvichukulia hatua vyombo vya habari huku Meghan akilishtaki gazeti la The Mail Jumapili kuhusu madai kwamba lilichapisha mojawapo ya barua zake za siri.
Naye mwanamfalme Harry aliwasilisha kesi katika mahakama kuu dhidi ya wamiliki wa gazeti la The Sun , News of The World na lile la Daily Mirror, kuhusiana na madai ya kudukua simu yake kuanzia muongo mmoja uliopita.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA

HILI NDILO BIFU KUBWA KATI YA RIHANA NA NICK MINAJ.