HILI NDILO TUNDU WATUHUMIWA WA UJANGILI WALIPO TOROKEA
Tundu lililotobolewa na Mahabusu hao. na kutoroka. |
Watuhumiwa watatu wa kesi za ujangili pamoja na
mauaji wametoroka mahabusu katika kituo cha polisi wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu,
mara baada ya kutolewa mahakamani kusikiliza kesi zinazowakabili.
Tukio hilo lilitokea terehe 19/02/2016 majira ya
usiku, ambapo ilielezwa kuwa walitoroka wakati mvua ikinyesha muda huo, huku
wakichimba ukuta kwa kutumia kitu chenye ncha kali kutoboa ukuta wa mahabusu
hiyo.
Akidhibitisha kutokea kwa tukio hilo Kaimu Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani
hapa Audax Majaliwa, alisema kuwa kutokana na tukio hilo askari saba
wanashikiliwa.
Majaliwa alisema kuwa watuhumiwa hao kabla ya
kutenda tukio hilo, terehe 01/02/2016 walifikishwa katika mahakama ya wilaya ya
Meatu ili kusikiliza kesi zinazowakabili.
Aliwataja watuhumiwa hao waliotoroka kuwa ni Chiluli
Sitta (28) mkazi wa kijiji cha Mwasangula kata ya Itinje wilayani humo, ambaye
alikuwa akikabiliwa na kesi a mauaji.
Wengine ni Msanja Ndangule (45) pamoja na Paschal
Masanja ambao ni Baba na mtoto wake, wote wakazi wa kijiji cha Sapa kata ya
Itinje wilayani humo ambao walikuwa wakikabiliwa na kesi ya ujangili.
Alisema katika mahabusu hiyo walikuwemo jumla ya
watuhumiwa sita, ambapo watatu ndiyo walitoroka na wengine wawili walibaki,
ambao ndiyo walitoa taarifa kwa askari kuwa wenzao wametoroka kwa kuchimba
ukuta.
“ jambo la kushangaza kwa nini wengine walibaki?
Na hao waliotoroka wanatoka kata moja…tunahofu hapa kuwa kulikuwepo na
njama…lakini wale waliobaki walieleza kuwa waliona dalili mapema kwa wenzao
kuwa wako kwenye mipango mikubwa” Alisema Majaliwa
askari
saba wanashikiliwa ili kusaidia uchunguzi wa tukio hilo ambao ni G 8371 PC Adam, F
9840 DC Hussen, D 5582 Copro Piter ambaye alikuwa Kiongozi wa zamu ziku ya
tukio, G 4806 PC John, G 8602 PC Yassin, H 8410 PC Hery Pamoja na WP 1125
Adija.
Alisema kuwa baada ya hatua hizo kwa askari hao,
taratibu nyingine za kushtakiwa kijeshi zitaendelea mara baada ya uchunguzi
kukamilika.
Maoni
Chapisha Maoni