WEMA Atangangaza Dau La Milioni Atakayemuona Mbwa wake
BEAUTIFUL Onyinye, Wema Sepetu ametangaza dau la shilingi milioni moja kwa yeyote atakayefanikisha kupatikana kwa mbwa wake aitwae Vanila aliyepotea hivi karibuni.
Akielezea ishu hiyo, Wema alisema mbwa huyo alikuwa na mwenzake akiishi nao nyumbani kwake Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambapo juzikati alikorofishana na mwenzake aitwae Thiona na kuamua kutokomea kusikojulikana.
Msanii huyo alisema anaomba yeyote atakayemuona Vanila wake awasiliane naye au atoe taarifa kituo chochote cha polisi kilicho karibu naye na atakabidhiwa pesa zake taslimu.
Maoni
Chapisha Maoni