Alichoamua Kingwendu baada ya mkewe KUBAKWA akiwa amelewa


Muigizaji wa filamu za Kiswahili, mchekeshaji Kingwendu yuko katika wakati mgumu baada ya mkewe kubakwa na jirani yake wakati akiwa amelewa pombe.
 
Baada  ya  jitihada  nyingi  za  kumtafuta Kingwendu, hatimaye  mwandishi  alifanikiwa  kumpata  na  kukiri  kuwa  alizipata habari hizo wakati ambapo yuko safarini na majirani walimueleza kilichotokea kuwa mkewe na jirani huyo aliyembaka mida ya saa tano usiku wote walikuwa wamelewa.
 
”Kama ulivyosikia hiyo habari, mimi nilikuwa sipo ndo nimerudi juzi, nataka nianze kufuatilia sheria sema sasa hivi nimefiwa na dada yangu tunapeleka msiba kijijini na baada ya hapo ninapumzika halafu ninasafiri Nairobi, nikirudi Nairobi tarehe tano kuanzia tarehe sita ndo naanza kufuatilia.” Amesema Kingwendu.
kingwendu
 
Mchekeshajihuyo ameumizwa na kitendo hicho na ameamua kufuata taratibu za kisheria ili haki itendeke.
 
“Kutokana na kitendo alichokifanya na mimi nimejisikia vibaya, inanibidi nimtafute huyu bwana nimpate ili nimpeleke mahakamani, mke wangu bado niko naye, sema huyu jamaa aliyefanya unyamaa huu yupo jirani. Mke wangu alikuwa amelewa na jamaa naye alikuwa amelewa. Mke wangu sijui alikuwa anatoka wapi saa tano usiku ndo akakutana na huyo jamaa, majirani ndio walivyoniambia hivyo, walinipigia simu wakati nipo Shinyanga huko.”  Amesema Kingwendu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA