Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA
Vikosi vya muungano vya Syria (SDF) vinavyoongozwa na wapiganaji wa Kikurdi vinasema majasusi waliiba nguo za ndani za Abu Bakr al-Baghdadi ambayo ilitumiwa kufanya uchunguzi wa chembe chembe za vinasaba, DNA kabla auawe.
Kamanda wa mwandamizi wa SDF Polat Can anadai kuwa wapelelezi wao walichangia kwa kiasi kikubwa juhudi za kupata maficho ya kiongozi wa kundi la Islamic State (IS) kabla ya oparesheni ya vikosi maalum vya Marekani nchini Syria.
- Serikali ya Tanzania yalaumiwa kuhusu wakimbizi wa Burundi
- Asili ya binaadamu wa leo 'yagunduliwa Botswana'
- Rais mstaafu Kenya atibiwa hospitalini, sio mara ya kwanza
Baghdadi alijilipua na kujiua mwenyewe wakati wa oparesheni ya kumsaka.
Marekani imepuuza jukumu la vikosi vya Kikurdi katika oparesheni hiyo.
Akizungumzia oparesheni hiyo Oktoba 27, Rais wa Marekani Donald Trump alisema vikosi hivyo "vilisaidia" kutoa habari lakini akaongeza hawakufanya ''jukumu lolote la kijeshi".
Bwana Can alisisitiza kuwa SDF ilichangia sehemu muhimu ya oparesheni hiyo katika ujumbe wa twitter alioandika Jumatatu.
Ujuzi wote na ufikiaji wa al-Baghdadi na kitambulisho cha mahali pake kilikuwa ni matokeo ya kazi yetu wenyewe
"mchakato wote wa kiintelijensia wa kumtafuta al-Baghdadi na utambuzi wa mahali alipokuwa umetokana na juhudi zetu wenyewe. Maafisa wetu wa intelijensia walihusika katika mawasiliano na kutoa muongozo uliochangia kufaulu kwa oparesheni hiyo hadi dakika ya mwisho," alisema.
Bwana Can aliongeza kuwa SDF imekuwa ikifanya kazi CIA kumtafuta Baghdadi tangu Mei 15, na kwamba waligundua alikuwa akijificha katika mkoa wa Idlib, mahali ambako oparesheni hiyo ilitekelezwa.
Vyanzo vya habari vinasema Bwana Can, alibaini kuwa kiongozi huyo wa IS alikuwa karibu kuhamia eneo jingine mjini Jarablus.
SDF wamekuwa washirika muhimu wa Marekani katka mapambano dhidi ya kundi la Islamic State (IS), lakini mapema mwezi huu rais Trump aliwaondoa wanajeshi wa Marekani kaskazini mwa Syria.
Wachambuzi wanasema hatua ya Marekani kuondoa wanajeshi wake iliipatia nafasi Uturuki kuanzisha mashambulio ya mpakani katika eneo hilo.
Raisi Donald Trump amethibitisha kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa Operesheni hiyo pia imefanikiwa kumuua msaidizi namba moja wa al- Baghdad
Tunafahamu nini kuhusu oparasheni hiyo?
Washirika kadhaa wa Marekani au washirika wakuu katika eneo hilo waliarifiwa kuhusu oparesheni hiyo,ikiwemo Uturuki, Iraq, vikosi vya Kikurdi kaskazini mashariki mwa Syria, na Urusi, ambayo inadhibiti anga juu ya Idlib.
Rais Trump alisema kwamba vitengo vya ujasusi nchini Marekani vilimchunguza Baghdad kwa wiki kadhaa kabla ya operesheni na kwamba walijua eneo hilo lilikuwa na mahandaki kadhaa, huku mengi yakiwa na mwisho wake.
Siku ya Jumamosi, rais aliamrisha ujumbe uliohusisha kundi moja la wanajeshi maalum, ndege nane na meli nyingine nyingi.
Ndege aina ya helikopta iliyokuwa ikisafirisha kikosi maalum cha Marekani kiliondoka kutoka eneo ambalo halikutajwa baada mwendo wa saa kumi na moja saa za Marekani siku ya Jumamosi.
Ndege hizo zilipaa juu ya anga ya Uturuki, mbali na maeneo yanayodhibitiwa na majeshi ya Syria pamoja na yale ya Urusi.
Urusi ilishirikiana na kufungua anga yake kwa operesheni hiyo ya Marekani licha ya kutoambiwa kile kilichokuwa kikijiri kulingana na rais Trump.
''Operesheni hiyo ya kuingia na kutoka ilikuwa hatari mno. Kulikuwa na wakati ambapo tungekabiliwa vilivyo'' , alisema .
''Ndege zetu zilipaa chini chini lakini kwa mwendo wa kasi''.
Huku ndege hizo zikikaribia katika nyumba hiyo zilishambuliwa lakini Trump anasema mashambulizi hayo yalimalizwa haraka.
Wanajeshi walishuka kwa mashambulio makubwa ya risasi ardhini, ripoti zilisema.
Baada ya hapo vikosi vya Marekani vilimtaka Baghdadi, ambaye alikuwa amejificha ndani ya pango kutoka nje na kujisalimisha .
Katika hutuba isiyo ya kawaida siku ya Jumapili , Rais Trump alisema Baghdadi alikufa baada ya kufika ukingoni alipokuwa akitoroka huko "akilia na kupiga mayowe wakati anafukuzwa na mbwa wa Marekani".
Baghdadi wakati huo alikuwa anatoroka akiandamana na watoto wake watatu wadogo ,lakini hatimae akajilipua kwa bomu alilokuwa amevaa baada ya kugundua kuwa amezingirwa.
Katika mlipuko huo Baghdadi na hao watoto wake wote watatu walifariki papohapo.
Rais Trump alisema japo mwili wa Baghdadi ulikuwa umechanika lakini waliweza kumtambua baada ya kuufanyia uchunguzi.
"Jambazi ambae alijitahidi sana kuwaogofya na kuwahangaisha wengine siku zake za mwisho alionekana mwenye mahangaiko,taharuki kubwa na kuchanganyikiwa ,alionekana mwenye uoga kupindukia alipogundua kikosi cha Marekani kilikuwa kinamkaribia , Rais Trump alisema.
Abu Bakr al-Baghdadi alijilipua wakati alipozingirwa na kikosi maalum cha Marekani.
Trump alisema matokeo ya uchunguzi uliofanyiwa maiti "ilitoa ishara malum, ambayo ilibaini moja kwa moja" kuwa ni Baghdadi.
Uchunguzi ulifanywa na wataalamu walioandamana na kikosi maalum katika eneo la tukio na walikuwa wamebeba sampuli ya chembe chembe za vinasaba DNA, ripoti ilisema.
Walitumia teknolojia mchanganyiko ya kutambua sura pamoja na mtambo mdogo wa kusoma matokeo ya DNA wakiwa ndani ya ndege kupata matokeo, kwa mujibu wa gazeti ya Daily Beast.
Wataalamu hao pia walibeba "kipande" cha mwili ili kuthibitisha matokeo ya uchunguzi wao.
Maoni
Chapisha Maoni