Marubani wa Southwest Airlines: Walikuwa wakichukua filamu za moja kwa moja kutoka katika choo cha ndege hiyo
Mfanyakazi wa kampuni ya ndege ya Southwest Airlines amewasilisha kesi mahakamani akiwashutumu marubani wawili kwa kuficha kamera katika choo cha ndege hiyo na kuwachukua picha za moja kwa moja abiria ambao walikuwa wakienda kujisaidia.
Renee Steinaker anadai kwamba aliwapata marubani hao wakati wa safari ya ndege ya mwaka 2017 kutoka Pittsburgh hadi Phoenix.
Rubani Terry Graham alimtaka kukaa katika chumba cha rubani na rubani mwenza Ryan Rusell, wakati alipotumia choo hicho, mashtaka hayo yanasema.
- Jinsi Abu Bakr al-Baghdadi alivyouawa
- Je ni kweli supu ya Pweza ni zaidi ya supu ya kawaida?
- 'Selfie iliyombaini mtoto aliyeibiwa'
Rubani na kampuni ya ndege ya South West Arlines wamekana kwamba kulikuwa na kamera iliyokuwa ikiwachukua abiria na wafanyakazi waliokwenda msalani.
Kampuni hiyo imesema kwamba kisa hicho kilikuwa cha kushangaza.
Bi Steinaker anadai kwamba bwana Russell alimuonya kutosema kitu kuhusu kamera hiyo ambayo alisema ilikuwa mkakati wa usalama.
Mfanyakazi huyo aliripoti kisa hicho kwa kampuni hiyo, lakini anadai msimamizi mmoja alimuagiza kutomwambia mtu yeyote kilichotokea.
Marubani hao hawakuitwa na kampuni hiyo ya ndege na wanaendelea na kazi yao kawaida kulingana na mashtaka hayo.
''Madai yaliowasilishwa ni ya kikatili'', wakili anayemwakilisha bi Steinaker aliiambia BBC.
Je kampuni hiyo na marubani wake wamesema nini?
Katika taarifa kampuni ya ndege ya Southwest Airlines iliambia BBC kwamba kampuni hiyo haiweki kamera katika vyoo vya ndege.
Awali , kampuni hiyo ya ndege ya Marekani ilikataa kutoa tamko kuhusu kesi hiyo .
Lakini katika taarifa nyingine , ilisema imechunguza madai hayo na kupata kwamba hakukuwa hata na kamera moja katika choo.
Southwest itapinga mashtaka hayo , ilisema.
''Wakati kisa hicho kilipotokea siku mbili zilizopita, tulichunguza madai hayo na kuangazia hali hiyo na wafanyakazi waliohusika''.
Kisa hicho kimedaiwa kutokea wakati wa safari ya 2017 kutoka Pittsburgh hadi Phoenix
"Tunaweza kuthibitisha kutoka kwa uchunguzi wetu kwamba hakukuwa na kamera chooni, kisa hicho hakifai na kwamba kampuni hiyo haiwezi kukikubali''.
BBC imeomba tamko kutoka kwa mawakili wanowawakilisha marubani hao.
Katika majibu yao yalioandikwa kwa walalamishi bwana Russell na bi Graham walikiri kwamba kulikuwa na kipakatalishi katika chumba hicho cha marubani lakini walikana madai mengine yoyote, CNN iliripoti.
Je mashtaka hayo yanasemaje?
Saa mbili kabla ya safari ya ndege kuanza mnamo tarehe 27 Februari 2017, bi Graham alimuomba bi Stainaker kusalia katika chumba hicho cha marubani huku yeye akienda chooni , yalisema malalamishi hayo.
Kulingana na sera ya kampuni hiyo ya ndege wafanyakazi wawili wanafaa kuwepo katika chumba hicho cha ndege kila mara.
Bwana Russell alikiri kwamba kamera ilikuwa ikichukua watu moja kwa moja , huku akiwa na wasiwasi katika uso wake, kabla ya kumshauri bi Stainaker kutoambia mtu yeyote na kwamba ulikuwa mkakati wa kiusalama, yamesema malalamishi.
Kamera hizo zilikuwa na siri kubwa zikiwa zimewekwa katika kila ndege aina ya 737-800 , ilidaiwa kwamba bwana Graham alimwambia mfanyakazi mmoja wa ndege.
Na kufuatia maelezo ya bwana Russell, bi Stainaker alipiga picha ya kipakatalishi hicho na simu yake, yalisema mashtaka hayo.
Wakati bi Stainaker alipolalama, msimamizi mmoja alimwambia kunyamaza kuhusu suala hilo , na kwamba iwapo itajulikana hakuna mtu atakayesafiri kwa kutumia kampuni hiyo ya ndege.
Mashtaka hayo ya Bi Steinaker yanataka alipwe $50,000 kama fidia kutoka kwa kampuni ya Southwest Airlines pamoja na marubani.
Bwana Goldman alisema mteja wake alikua amedhurika na suala hiyo ambalo lilimsababishia dhiki kali.
Mashtaka hayo yaliwasilishwa katika kaunti ya Maricopa , jimbo la Arizona, lakini imehamishwa katika mahakama ya wilaya mjini Arizona.
Hakuna tarehe ya kusikilizwa kwa keshi hiyo imewekwa kufikia sasa.
Maoni
Chapisha Maoni