SULUHU YA WANAUME KUBORESHA MBEGU ZA UZAZI HII HAPA USIKOSE! LINDA NDOA YAKO SASA


Tomato pureeHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Chakula chenye nyanya nyingi kinaweza kumsaidia mwanaume kutoa mbegu za kiume zenye ubora, utafiti umebainisha.
Afya ya wanaume ambao hunywa vijiko viwili vya nyanya ambayo imesagwa kwa siku wamebainika kuwa na shahawa ambazo ni bora zaidi.
Tatizo la uzazi kwa wanaume limeathiri karibu nusu ya idadi ya wapenzi wanaoishindwa kupata watoto.
Mtaalamu wa masuala ya uzazi anasema kuwa kuna uhitaji wa tafiti nyingi zaidi kuhusisha wanaume ili kujua tatizo lao la kushindwa kuzalisha.
Wataalamu wa afya wamewashauri wanaume wenye matatizo ya uzazi kwa sasa kula chakula bora kwa afya na kuvaa nguo za ndani ambazo hazibani.
Utafiti umeshauri pia wanaume wanapaswa kupunguza msongo wa mawazo wawezavyo na kushiriki tendo la ndoa na wenza wao kila mara wanapokuwa karibu na wapenzi wao.
Lakini wazo la kutumia chakula aina fulani cha virutubisho limekiwa likisisitizwa sana kwa muda sasa.
Nyanya ni chakula ambacho kina vitamini E na madini ya zink jambo ambalo limekuwa likiwekewa mkazo katika tafiti zilizopita ni kuwa na uwezo wa kuzuia seli ambazo zinaweza kusababisha uharibifu katika mwili.
Chakula hicho kimekuwa kikihusishwa na faida za kiafya pamoja na kupunguza hatari za kupata ugonjwa wa moyo au saratani.
Cooked tomatoesHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Wataalam wanasema kuwa kuna watu wanaotumia tiba lishe kwa sababu kutumia tu nyanya kwenye chakula inawia vigumu kutambua kwa uhakika kama kila mwanaume amepata .
Wanaume wanahitajika kula nyanya kilo mbili zilizopikwa kila siku ili kupata ujazo sawa na tiba lishe ya nyanya.
Presentational grey line
Katika jaribio la wiki 12, ambapo kampuni inayotengeneza tiba lishe ilichagua wanaume 60 kunywa tiba lishe gramu 14 kwa siku au vidonge.
mbegu zao za kiume zilifanyiwa jaribio la kwanza katika wiki ya sita na mwishoni mwa utafiti.
Licha ya utofauti wa manii zao lakini zilionyeshwa namna gani shahawa zinatoka kwa kasi zilikuwa juu kwa wale waliokula tiba mbadala wa nyanya.
Dr Liz Williams, mtaalamu wa lishe katika chuo kikuu cha Sheffield, anasema kuwa sasa kuna ushauri mdogo sana ambao anaweza kuwapa wanaume katika kutumia chakula hicho.
"Sisi tunawaambia kuwa wapunguze matumizi ya pombe na kula vizuri, ushauri ambao ni wa kawaida tu."
Aliongeza pia kuwa: "Huu ni utafiti mdogo ambao umefanywa, kuna uhitaji wa jaribio lingine kubwa, lakini matokeo haya yanatia moyo.
"Hatua inayofuata ni kurudia zoezi hilo kwa wanaume wenye matatizo ya uzazi na kuona kama nyanya inaweza kuboresha shahawa za wanaume na kusaidia wapenzi kupata watoto au tiba sahihi ya uzazi."

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA