MAPENZI YALIYO CHIPUKA GEREZANI, SASA NI WANANDOA!


Waswahili husema 'Mapenzi ni kama Nyasi na humea popote',
Mwandishi wa BBC scolar kisanga alisafiri hadi mkoani Kilimanjaro nchini humo na kuhudhuria ndoa ya kipekee iliyofanyika mwishoni mwa juma baina ya wapenzi wawili hao wawili waliokutana wakiwa gerezani wakitumikia vifungo vyao.
Lakini wawili hawa Walikutana vipi ilihali wafungwa wa kiume na wa kike hufungwa Magereza tofauti?
Rose Male ambaye kwa sasa anafahamika kama (Jamila) alihukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa tuhuma za mauaji na kutumikia kifungo hicho kwa miaka sita na baadae kujulikana hakua na hatia.
jamila
Mohamed Ulotu ambaye kwa sasa ni ndiye mume wa Jamila ,yeye alihukumiwa kifungo cha miaka 30, alitumikia na kukimaliza kifungo chake na baade kukata rufaa katika mahakama ya Afrika ya haki za binaadamu na kushinda rufaa hiyo na sasa anategemea kulipwa fidia na serikali ya taifa hilo la Afrika Mashariki
Lakini swali la kujiuliza ni walikutana vipi ilihali wanawake na wanaume hufungwa magereza tofauti?
''Tulikutana katika idara ya afya, wafungwa tuliofungwa muda mrefu hua tunapata uongozi, hivyo wakati napeleka wagonjwa hospital na kuwahudumia wengine ndio nikaonana na Jamila ,wakati huo alikuwa mahabusu na tulianza kuongea nikawa nampa moyo kwamba haki yake ataipata, lakini sikujua kama tungefikia hapa'' alisema Mohamed.
Hata hivyo Mohamed aliwahi kutoka Gerezani mwezi Julai mwaka 2017 huku mkewe (Rose Male) ambaye kwa sasa ni Jamila aliendelea kukaa mahabusu na baadae ndio alipohukumiwa kunyongwa hadi kufa.
''Mimi nilimaliza kutumikia kifungo changu nikatoka ambapo nilikaa miaka 20 yaani sawa na miaka 30 kwani kwa sharia za kimagereza moja ya kumi ya kifungo huondolewa hivyo ikabaki miaka 20 na nikatumikia yote na nikiwa uraiani nilihangaikia rufaa yangu wakati huo pia nilikua nafuatilia kuhusu kesi ya Rose (Jamila)'' Alisema Mohamed.
Miezi mitano baada ya Mohamed kutoka Mkewe Rose Male (Jamila) nae alishinda Rufaa yake na kurejea uraiani.
''Siku nilipoambiwa nipo Huru nimeshinda rufaa yeye (Mohamed) alikua mtu wa kwanza kabisa Kuja na ndio siku aliyonitamkia kwamba ananipenda lakini nilimwambia haukua wakati wake,Nilienda nyumbani na tukaendelea kuwasilina na baadae nikamruhusu akaja kujitambulisha'' alisimulia Jamila.
M
Wawili hao kila mmoja anasema amekua mwenye furaha kwani ametimiza haja ya moyo na kusema alitamani kuoa/kuolewa mtu aliyepitia gerezani kwani wamekumbana na mengi na kuona kila mmoja alimtahili mwenzie.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA