MBWANA SAMATA AMEFUNIKA; CHEKI HARUSI YAKE NA MPENZI WAKE NEIMA MGANGE!


SAMATTAHaki miliki ya pichaSAMATTA/INSTAGRAM
Image captionSamatta na mkewe baada ya kufunga ndoa
Ni likizo ya kimataifa na wachezaji wenzake wengi wapo katika zamu ya kimataifa lakini nahodha wa timu ya Taifa Stars na KRK Genk Mbwana Samatta alikuwa na mipango mingine kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania.
Mshambuliaji huyo matata alitumia wakati wake mzuri wa likizo hiyo siku ya Alhamisi kufunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi Neima Mgange.
Sherehe ya harusi yake iliofanyika katika kijiji cha kijichi mjini Dar es Salaam ilihudhuriwa na wachezaji wenzake wa Taifa Stars akiwemo Himid Mao na Thomas Ulimwengu kulingaa na gazeti hilo.
Ilikuwa sherehe ya kufana miongoni mwa watu wa familia ya Mgange walipokutana na mshambuliaji huyo ambaye ndiye mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kushiriki katika ligi ya mabingwa Ulaya.
Maelezo kuhusu uhusiano wa Mbwana na Neima yalikuwa ya siri kubwa na ni watu wa familia zote mbili pekee waliokuwa wakielewa kilichokuwa kikiendelea hadi siku ya Alhamisi.
Mshambuliaji huyo hakushirikishwa katika mechi ya kimataifa ambayo Taifa Stars inacheza dhidi ya Uganda wikendi hii.
Alikuwa akiugua jeraha lakini akashirikishwa katika kikosi cha timu ya Genk kilichopoteza 6-2 dhidi ya klabu ya Salzbourg kutoka Austria katika michuano ya kombe la mataifa bingwa Ulaya.
Pia aliisaidia Tanzania katika michuano ya kimakundi ya kufuzu kwa kombe la dunia Qatar 2022.

Kwanini Mbwana Samatta ananganganiwa na klabu England

Mbwana Ally Samatta huchezea KRC Genk ya UbelgijiHaki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionMbwana Ally Samatta huchezea KRC Genk ya Ubelgiji
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Ally Samatta anang'ang'aniwa na klabu tatu za England, taarifa za vyombo vya habari nchini Uingereza zinasema.
Tetesi zinasema nyota huyo anatafutwa na West Ham United, Everton na Burnley.
Samatta, 25, maarufu kwa Watanzania kama Samagoal ameng'aa sana akichezea klabu ya KRC Genk nchini Ubelgiji.
Amefungia klabu hiyo mabao 11 katika mechi 16 ambazo amewachezea msimu huu, nusu ya mabao hayo akiyafunga barani Ulaya.
Taarifa za kumhusisha Samatta na klabu ya Everton zimetoka kwa mtandao wa hitc.com, mmoja wa mitandao ambayo imeibukia kuwa maarufu kwa taarifa za wachezaji na kuhama kwao.

Kwa nini anahusishwa na Everton?

Samatta, mwenye kimo cha futi 5 inchi 11, amefunga mabao sita katika ligi ndogo ya klabu barani Ulaya, Europa League, na ni hapo ameanza kuonekana na klabu za England.
Mnamo 23 Agosti 2018 Samatta, alifunga 'hat-trick' dhidi ya Brøndby IF katika Europa League kwenye mechi ambayo walishinda 5-2.
Everton wametatizika kumpata mshambuliaji wa kutegemewa tangu nyota wao Romelu Lukaku alipowaacha na kuhamia Manchester United kwa £75 mwaka 2017.
Wamekumbwa na ukame wa mabao msimu huu na zaidi wamesaidiwa na mawinga au viungo wa kati badala ya washambuliaji wao ambao wameonekana butu.
Ndio maana si ajabu wanavutiwa na mchezaji ambaye ameibuka stadi wa kutikisa nyavu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA