Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Rais wa TFF aachiwa huru, aanza kurejesha mamilioni aliyohujumu



on Rais wa TFF aachiwa huru, aanza kurejesha mamilioni aliyohujumu
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru aliyekuwa makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura kwa masharti ya kutokufanya makosa yoyote kwa kipindi cha miezi 12 nakulipa zaidi ya Shilingi milioni 100 kwa awamu tano ambapo leo amelipa Tsh. 20,249,531
Mnamo Oktoba 02, Michael Wambura alieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu kuwa ameandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kwa ajili ya kuomba msamaha na kukiri makosa yake.
Wambura alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza, Februari 11, mwaka huu, akikabiliwa na mashtaka 17 yakiwemo ya kutakatisha fedha zaidi ya Sh 100milioni, katika kesi ya uhujumu uchumi namba 10/2019.
Hatua hiyo ni kufuatia ombi la Rais Magufuli mnamo Septemba 22, 2019 akiwa Ikulu jijini Dar es salaam wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni alimpa siku 7 Mkuu wa Mashtaka (DPP) Biswalo Mganga kwenda kuwasikiliza watuhumiwa wa makosa ya uhujumu uchumi waliopo rumande ili kwa wale walio tayari kutubu na kulipa fedha walizo hujumu na waachiwe huru.
Ambapo Septemba 30, Rais Magufuli amepokea taarifa kuwa jumla ya washtakiwa 467 wapo tayari kurudisha jumla ya shilingi Bilioni 107.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA