PATA VISA VYA DAKTARI ALIYESAIDIA CIA KUKAMATWA KWA OSAMA BIN LADEN HATIMAYE KUUAWA!
Daktari wa PakistanI ambaye aliisaidia Marekani kumpata kiongozi wa kundi la al-Qaeda Osama Bin laden amekata rufaa dhidi ya hukumu yake jela.
Ni mara ya kwanza ambapo kesi ya Shakil Afridi inasikilizwa katika mahakama ya wazi.
Jaji aliahirisha kesi hiyo hadi tarehe 22 mwezi Oktoba kufuatia ombi la waendesha mashtaka.
- Tanzania na Kenya zaongoza kwa idadi ya mabilionea
- Matumaini baada ya gari lililozama kivuko cha Likoni kuonekana
- Polisi apigwa mawe hadi kufa
Kinachodaiwa kufanywa na Daktari Afridi kilikuwa aibu kubwa kwa Pakistani. Lakini yeye mwenyewe anadai ya kwamba alinyimwa haki yake wakati wa kusilikilizwa kwa kesi hiyo ambapo alihukumiwa mika 33 jela.
Hakushtakiwa rasmi kwa jukumu lake katika operesheni hiyo ya mwaka 2011 ya kumsaka na kumuua mtu aliyekuwa akitafutwa sana duniani.
Kufungwa kwake jela kulisababisha hisia kali hatua iliosababisha Marekani kufutilia mbali msaada wake kwa Pakistan wa takriban dola milioni 33 - ikiwa ni dola milioni moja kila mwaka kwa hukumu yake katika mahakama ya Peshawar.
Rais wa Marekani Donald Trump aliahidi katika uchaguzi wa 2016 kwamba atamwachilia huru Afridi baada ya dakika mbili iwapo atachaguliwa - lakini hilo halijafanyika.
Huku daktari huyo akionekana kuwa shujaa Marekani, nchini Pakistani anaonekana kama msaliti ambaye alililetea aibu kwa taifa hilo.
Makomando wa jeshi la wanamaji la Marekani walisafiri kwa helikopta kutoka Afghanistani mpaka Pakistani na kumuua aliyepanga njama za mashambulizi ya Septemba 11 na kuondoka na mwili wake bila kuzuiwa.
Na hatua hiyo ilizua maswali mengi ya iwapo jeshi la Pakistani lilikuwa linajua iwapo Bin Laden alikuwa nchini humo. Pakistani imesalia kuwa mshirika asiyeaminika katika vita vya Marekani dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu.
Lakini je, Shakil Afridi ni nani?
Dkt Afridi alikuwa daktari mkuu katika hospitali ya wilaya ya Khyber na akiwa mkuu wa huduma za afya alikuwa amesimamia baadhi ya mipango kadhaa ya chanjo zinazofadhiliwa na Marekani.
Kama mfanyakazi wa serikali , alianzisha mpango wa chanjo ya Homa ya Ini (Hepatitis B), ikiwemo katika mji wa Abbottabad ili kubaini iwapo waliokuwa wakiishi katika eneo hilo ni ndugu za bin Laden.
Inadhaniwa kwamba mfanyakazi mmoja wa Dkt Afridi alitembelea nyumba ya akina Osama bin laden na kuchukua vipimo vya damu - lakini haijulikani iwapo hilo lilisaidia Marekani kumpata Osama.
Dkt Afridi alikamatwa mnamo tarehe 23 mwezi Mei 2011 siku chache tu baada ya Bin laden kuuawa. Alidaiwa kuwa na miaka 40 wakati huo.
Ni mambo machache yanayojulikana kuhusu maisha yake, mbali na kwamba alitoka katika familia maskini na kufuzu katika chuo cha matibabu cha Khyber 1990.
Familia yake imekuwa ikiishi katika maficho tangu kukamatwa kwake , ikihofia shambulio la kijeshi.
Mkewe ni msomi kutoka Abbotabad ambaye alikuwa mwalimu mkuu wa Shule ya serikali kabla ya kwenda mafichoni. Wawili hao wana watoto watatu - wavulana wawili na msichana mmoja - watoto wawili wakiwa watu wazima kufikia sasa.
Mwezi Januari 2012 , maafisa wa Marekani walikiri hadharani kwamba Dkt Afridi alikuwa akikifanyia kazi kikosi cha Ujususi cha Marekani. Lakini haijulikani jukumu lake lilikuwa ni lipi katika CIA.
Hakusema lolote kuhusu jukumu lake wakati kesi yake ilipokuwa ikisikizwa na tume ya Abbottabad kuhusu mauaji hayo.
- Marekani yatangaza $1m kwa mwanawe Bin Laden
- Aliyekuwa mlinzi wa Osama Bin Laden afukuzwa kutoka Ujerumani
Dkt Afridi hakujua ni nani aliyekuwa akilengwa katika operesheni hiyo wakati alipoajiriwa na CIA kulingana na uchunguzi wa Pakistan.
Je alihukumiwa na nani?
Ijapokuwa awali alikuwa ameshtakiwa kwa kutekeleza uhaini, Dkt Afridi alifungwa mwezi Mei 2012, baada ya kupatikana na makosa ya kufadhili kundi la Lashkar-e-Islam, kundi la wapiganaji lililopigwa marufuku.
Alihukumiwa kifungo cha miaka 33 jela kwa madai ya kushirikiana na kundi hilo na mahakama moja ya kikabila, ijapokuwa hukumu hiyo ilipunguzwa na kufikia miaka 23 baada ya kukata rufaa.
Daktari huyo pia alishutumiwa kwa kutoa msaada wa dharura kwa wapiganaji hao na kuyaruhusu makundi kama hayo katika hospitali ya serikali aliokuwa akisimamia.
Familia yake imekana mashtaka hayo na mawakili wake wanasema kwamba fedha alizotoa ni kikombozi cha dola 6,375 ili kumwachilia baada ya kutekwa 2008.
Kutoka seli yake jela 2012 alidaiwa kuambia shirika la habari la Fox News kwamba alikuwa ametekwa na kuteswa na majasusi wa Pakistan.
Mwaka mmoja baadaye alifanikiwa kupeleka barua alioandilka kwa mkono kwa wakili wake akisema kwamba amenyimwa haki
Kwa nini basi hakushtakiwa na mashtaka ya kuisaidia Marekani?
Hilo haliko wazi, lakini swala hilo la Bin Laden lilikuwa pigo kubwa kwa Pakistan.
Ijapokuwa maafisa walikasirishwa na kile walichokiona kama ukiukaji wa haki ya uhuru wa taifa hilo, huduma ya ujasusi ililazimika kukiri hadharani hawakujua kwamba mwanzilishi huyo wa kundi la al - Qaeda alikuwa akiishi kwa siri katika eneo hilo katika nyumba ya ghorofa tatu ambayo ilikuwa imezibwa na kuta ndefu kwa miaka kadhaa.
Kwa nini kesi hiyo inasikizwa mahakamani wakati huu?
Kufikia sasa , mchakato mzima wa kesi yake umeanzishwa chini ya usimamizi wa sheria za uhalifu za Uingereza , ambazo zilitawala maeneo ya kikabila karibu na mpaka na Afghanistan hadi mwaka uliopita.
Mahakam za kikabila zilisimamiwa na maafisa wa utawala, zikisaidiwa na baraza la wazee wa kikabila na hawakuwa wakifuata sheria inavyohitajika.
Hiyo ilionekana kuwa njia rahisi ya kukabiliana na Afridi, ikiwa sio swala la kufanyika hadharani
Lakini kuunganishwa kwa maeneo ya kikabila na mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa mwaka uliopita kunamaanisha kwamba kesi hizo zimerudishwa katika mahakama za kawaida.
Katika siku ya kusikilizwa kwa kesi yake hukumu yake inaweza kupunguzwa ama kuongezwa , kwa kuwa waendesha mashtaka watahoji.
Tangu alipohamishwa mwaka uliopita kutoka jela ya Peshwar hadi Punjab, kumekuwa na madai kwamba huenda akaachiliwa, ikiwezekana kupitia kubadilishana wafungwa na Aafia Siddiqui , mtu aliyedaiwa kuwa mshirika wa al - Qaeda ambaye kwa sasa yuko jela Marekani.i.
Maoni
Chapisha Maoni