Wasiwasi kuhusu mabomu 50 ya kinyuklia ya Marekani yaliyofichwa Uturuki


Kambi ya kijeshi ya Incirlik inaendeshwa kwa pamoja na marekani na UturukiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Ulikuwa ujumbe wa twitter , lakini lilikuwa kama tangazo la kutangaza vita vya kiuchumi.
Ujumbe ulioandikwa na rais wa Marekani Donald Trump tarehe 7 mwezi Oktoba ulishirikisha vitisho vya moja kwa moja vya kuangamiza kabisa uchumi wa Uturuki iwapo taifa hilo litavuka mpaka na kuendelea kupigana dhidi ya Wakurdi katika mpaka wake.
Akinukuliwa rais huyo wa Marekani alionekana kutaka kudhibiti operesheni ya uvamizi huo ambao umepingwa na rais wa Uturuki Reccep Tayyip Erdogan katika eneo la Kaskazini mwa Syria ili kuteka eneo ambalo halikuwa na vikosi vya Kikurdi ambavyo vinaonekana kuwa hatari na serikali ya Ankara.
Kufikia wakati huo , kizuizi pekee cha hatua ya Uturuki kuvamia eneo hilo ni uwepo wa wanajeshi wa Marekani ambao Trump alitangaza kuondoka kwake.
Kama ilivyothibitishwa na Pentagon , mashambulizi yaliotekelezwa na Uturuki yalikuwa yakianguka mita 100 karibu na kambi yake ya kijeshi.
Suala hili lilizua wasiwasi kuhusu kudorora kwa uhusiano kati ya Uturuki na Washington ambapo ilijibu kwa kuiwekea vikwazo vya kiuchumi.
Sio kuhusu uhusiano wowote, Uturuki ipo katika eneo la kijiografia ambapo inalifanya taifa hilo kuwa daraja kati ya mashariki ya Ulaya, mashariki ya kati na katikati ya Asia.
Eneo la Bosphorus linaifanya Uturuki kuwa eneo zuri la kimkakatiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Uturuki ni mshirika rasmi wa Marekani kuhusu masuala ya ulinzi, ambapo jeshi la pili kubwa zaidi katika muungano wa Nato mbali na kwamba taifa hilo linahifadhi mabomu 50 ya kinyuklia ya Marekani ambayo yamehifadhiwa katika kambi moja ya wanahewa katika eneo la Incirlik, umbali wa kilomita 100 kutoka katika mpaka na Syria.
Baada ya mashambulizi yalioagizwa na Erdogan, utawala wa Trump ulianza kuweka mipango ya kusafirisha silaha hizo ambazo kulingana na maafisa wakuu wa Marekani walionukuliwa na gazeti la 'The New York Times' zimekuwa chini ya uhifadhi wa Erdogan.
Lakini mabomu hayo yaliingiaje Uturuki?

Urithi wa vita baridi.

Uwepo wa mabomu hayo ya kinyuklia katika ardhi ya Uturuki imekuwa siri kubwa kwa zaidi ya muongo mmoja.
Kwa mujibu wa Jeffery Lewis, profesa wa uthibiti wa silaha katika taasisi ya mafunzo ya kimataifa ya Middlebury mjini California, kuna mataifa mengine ambayo yapo katika hali kama hiyo, kama vile Ujerumani , Itali, Ubelgiji na Uholanzi.
kami ya kijeshi ya ya wanahewa ya Ujerumani pia inahifadhi mabomu ya kinyuklia aina ya B61Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Mojawapo ya makubaliano yalioafikiwa kati yake na Usovieti kutatua mzozo huo wa makombora ya 1962, Moscow iliamua kupeleka makombora yake nchini Cuba huku Marekani ikiondoa makombora yake kutoka Uturuki.
Marekani iliondoa makombora yake lakini imekuwa ikihifadhi mabomu yake ya Kinyuklia nchini Uturuki ili kutumika na taifa hilo pamoja na washirika wa Nato.
Ni takriban mabomu 50 aina ya B61, yalio na uwezo wa kubeba mzigo wa kinyuklia wenye kati ya tani 300 na kilotani 170 ikiwa ni ukubwa wa zaidi ya mara 11 ya bomu lililofanya uharibifu mkubwa katika mji wa Hiroshima.
Hatahivyo ni wanajeshi wa Marekani pekee walio na uwezo wa kuyatumia kwa kuwa Syria haina vifaa vinavyoweza kurusha mabomu hayo.
Lakini kutokana na hofu iliopo kwa sasa na Uturuki, hatari kubwa ni kuweka mabomu hayo katika eneo hilo la Incirlik na itamaanisha nini kuyaondoa.?

Ishara na tishio

Kulingana na maafisa hao wakuu wa Marekani waliohojiwa na 'New York Times', hali ya mabomu hayo inashirikisha tatizo la kwamba kuyaondoa katika eneo la Incirlik kutamaliza uhusiano kati ya Marekani na Uturuki.
Lakini kuyaacha kunaweza kukuza hatari ya kinyuklia ambayo inapaswa kuwa ilisuluhishwa miaka iliyopita.
Ndege za kivita za Awacs zimetumia kambi ya Incirlik katika operesheni zake za mashariki ya katiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Hii sio mara ya kwanza kwa masuala hayo kujadiliwa, ijapokuwa hakujakuwa na haraka yoyote.
Tangu mwisho wa vita baridi , hatma ya aina hiyo ya mabomu ya kinyuklia imekuwa ikijadiliwa katika Nato lakini wanachama kadhaa ikiwemo Uturuki imepinga kuondolewa kwake kwa kuwa ni ishara ya hakikisho la Marekani kuwalinda washirika wake.
Wachanganuzi wengine pia walizungumzia hatari ya kuondolewa kwake, ikiwa kama sababu ya Uturuki kutengeza silaha zake za kinyuklia , wazo ambalo Erdogan alitoa ishara aliposema katika mkutano wa hadhara wa chama chake kwamba haikubaliki kwamba taifa lake halina silaha hiyo.
Alisema kwamba hakuna taifa lililoendelea ambalo halina silaha ya kinyuklia.
Wataalama kama vile Ankit panda, mchunguzi mkuu wa shirikisho la wanasayansi wa Marekani FAS anaamini hakuna umuhimu wowote wa kuweka silaha hizo nchini Uturuki.
Ushirikiano huo wa Uturuki na Marekani hautaokolewa na uwepo wa mabomu ya Marekani katika ardhi ya Uturuki, Panda aliandika katika gazeti la New Republic.
Mabomu hayo yanaweza kuondolewa, Uturuki ikaendelea kusalia kama mwanachama wa Nato anayevumiliwa.
Na ni jukumu la Uturuki katika muungano wa Nato ambalo lipo katikati ya mjadala huo.
Wakosoaji wa Erdogan wanamtuhumu Erdogan kwa kuwa diktetaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
''Serikali ya Uturuki imebadilika, Rais Erdogan amekuwa dikteta na kwamba sera yake ya kigeni inaunga mkono Urusi.
Amebadilika kutoka kuwa mshirika wa Marekani na kuchukua msimamo wa kadri na hata misimamo mengine ikiwa kinyume na maslahi ya usalama wa Marekani'', anasema Lewis.
Ushirikiano unaoonekana kati ya Moscow na Ankara ni thibitisho tosha hususan hatua ya Erdogan kununua mfumo wa ulinzi wa Urusi aina ya S-400, ambao uliifanya Marekani kuiondoa Uturuki katika mpango wake wa utengenezaji silaha pamoja na ununuzi wa ndege za Marekani aina ya F-35.
''Iwapo Uturuki ingewasilisha ombi la kuwa mwanachama wa Nato, ombi hilo halingefanikiwa'', aliandika Max Boot , mchanganuzi anayelifanyia kazi baraza la uhusiano wa kimataifa la Marekani CFR.
Mtaalamu huyo anaelezea kwamba kwa sasa shirika hilo linahitaji wanachama kuwa na mfumo wa kidemokrasia, kutafuta suluhu kwa njia za amani, kuonyesha hakikisho la kufuata sheria, haki za kibinadamu, soko la kiuchumi mbali na mahitaji mengine.
''Uturuki licha ya kuwa na soko la kiuchumi haliwezi kuafikia masharti hayo mengine'', aliongezea.

Je mabomu hayo yako salama?

Hii sio mara ya kwanza kwamba Marekani ina hofu kuhusu usalama wa mabomu yake ya kitonoradi nchini Uturuki.
Mwaka 2016, wakati wa jaribio la mapinduzi dhidi ya Erdogan, kambi hiyo iliopo Incirlik ilitumika na baadhi ya washirika katika njama, ikiwemo jenerali ambaye aliomba ulinzi wa Marekani ambao alinyimwa.
Ndani ya kambi hiyo ya incirlik kuna mabomu hayo ya ya kinyuklia ya B61Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Baadae wanajeshi walio watiifu walikatiza umeme katika kambi hiyo kabla ya kufanya operesheni ya kuwazuia wanajeshi waasi waliokuwemo.
Tukio hili linaelezea umbali wa Ankara na Washington, tangu Uturuki ilalamike kwamba Marekani ilikuwa na mkono katika mapinduzi hayo, mbali na hatua ya Marekani kukataa kumrudisha Fetullah Gulen , kiongozi wa dini anayedaiwa kuanzisha mapinduzi hayo.
Muhubiri wa Kiislamu Fetullah Gulen ameshutumiwa na Uturuki kwa kufanya jaribio la mapinduzi nchini humoHaki miliki ya pichaAFP
Jaffery Lewis anaelezea kwamba silaha hizo zipo katika sakafu ya jumba moja linalolindwa sana ambalo pia linalindwa na vikosi vya Marekani, zikizingirwa na uwa mkubwa .
Mabomu hayo pia yana vifaa vya usalama na yanahitaji nambari ya kuingia ndani yake ili kuyatumia.
Masharti hayo yote yanalenga kuyalinda kutoka kwa kundi lolote la kigaidi ama jeshi lenye malengo maovu.
''Hatahivyo silaha hazipo salama iwapo kwa mfano serikali ya Uturuki itaamua kuziiba'', walisema wataalam.
Lewis sasa anaunga mkono Marekani kuyachukua mabomu hayo kutoka eneo la Incirlik.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia