SONG JIANG, MHALIFU WA UCHINA ALIYEJIFICHA PANGONI KWA MIAKA 17 ANASWA HATIMAYE!
Pata kiungo
Facebook
X
Pinterest
Barua pepe
Programu Nyingine
Haki miliki ya pichaYONGSHAN POLICEImage captionBaada ya miaka 17 Song alibainiwa na ndege isiyokuwa na rubani (drone)
Polisi nchini Uchina wamemkamata mhalifu ambaye amekuwa akijificha kwa miaka 17, baada ya kutumia ndege zisizokuwa na rubani kubaini pango alimokuwa akijificha.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 63 ,kwa kwa majina Song Jiang amekuwa akitafutwa na polisi baada ya kutoroka jela ambapo alifungwa kwa kufanya biashara haramu ya kuwasafirisha wanawake na watoto, lakini aliweza kutoroka kutoka kwenye kambi ya jela mwaka 2002.
Amekuwa akiishi ndani ya pango dogo na kukata mawasiliano ya aina yoyote na binadamu kwa miaka mingi.
Polisi katika mji wa Yongshan walipokea taarifa kuhusu ni wapi alipo Song mwezi Septemba , kulingana na maelezo yao katika akaunti yao ya mtandao wa kijamii wa WeChat.
Taarifa hizo ziliwapeleka hadi katika eneo la milima iliyopo nyuma ya mji anakotoka katika jimbo la Yunnan lililopo kusini mashariki mwa Uchina.
Haki miliki ya pichaYONGSHAN POLICEImage captionNdege isiyokuwa na rubani ( Drone) ilibaini pango kwenye eneo la milima yenye mteremko mkali
Baada ya kushindwa kumpata katika msako wa kawaida , maafisa walituma ndege zisizokuwa na rubani za ziada ili kuwasaidia maafisa katika msako huo.
Hatimae ndege hizo zilibaini chuma chenye rangi ya kwenye eneo la mtelemko mkali pamoja na taka zilizokuwa kando ya makazi yaliyopo karibu na eneo hilo.
Haki miliki ya pichaYONGSHAN POLICEImage captionPando lilikuwa na ukubwa wa mita 2 za mraba
Ndipo polisi walipoamua kutembea kwa miguu hadi katika eneo hilo na kumpata song ndani ya pango dogo ambamo amekuwa akiishi kwa miaka.
Kwa mujibu wa polisi , mwanamme huyo amekuwa akiishi kwa kujificha binadamu kwa muda mrefu kiasi kwamba ilikuwa ni vigumu kwakekuwasiliana na maafisa usalama.
Tasnia ya filamu nchini huenda ikawa na mengi yanayofanyika nyuma ya pazia wakati wa majaribio ya kutafuta shots nzuri zenye uhalisia hasa kwenye scene za mapenzi! Lakini napata kigugumizi kikali kwa kile kilichoonekana kwenye video hii inayoaminika kuwa ni kipande cha filamu mpya inayotarajia kutoka iliyowakutanisha Rich na Irene Uwoya ambao wanaonekana wakibadilishana mate kwa kiss za uweli. Je, uhalisia huu kwenye filamu za Bongo unakubalika kimaadili? Bila shaka haukubaliki hapa kwetu Tanzania. Bado hatuko huko Hollywood na naamini kipande hicho kitatolewa. ASANTE KWA KUPATA HUDUMA ZETU,TUNAKUOMBA BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK
Haki miliki ya picha Image caption Vikosi vya muungano vya Syria (SDF) vinavyoongozwa na wapiganaji wa Kikurdi vinasema majasusi waliiba nguo za ndani za Abu Bakr al-Baghdadi ambayo ilitumiwa kufanya uchunguzi wa chembe chembe za vinasaba, DNA kabla auawe. Kamanda wa mwandamizi wa SDF Polat Can anadai kuwa wapelelezi wao walichangia kwa kiasi kikubwa juhudi za kupata maficho ya kiongozi wa kundi la Islamic State (IS) kabla ya oparesheni ya vikosi maalum vya Marekani nchini Syria. Serikali ya Tanzania yalaumiwa kuhusu wakimbizi wa Burundi Asili ya binaadamu wa leo 'yagunduliwa Botswana' Rais mstaafu Kenya atibiwa hospitalini, sio mara ya kwanza Baghdadi alijilipua na kujiua mwenyewe wakati wa oparesheni ya kumsaka. Marekani imepuuza jukumu la vikosi vya Kikurdi katika oparesheni hiyo. Akizungumzia oparesheni hiyo Oktoba 27, Rais wa Marekani Donald Trump alisema vikosi hivyo "vilisaidia" kutoa habari lakini akaongeza hawakufanya ''jukumu lolote ...
Mtindi unaorodheshwa kuwa miongoni mwa vyakula bora kutokana na kuwa na virutubisho vingi vya aina mbalimbali ambavyo vina faida nyingi katika mwili wa binadamu. Vikitajwa kwa uchache virutubisho hivyo, imethibitika kuwa mtindi ni chanzo kizuri cha ‘Calcium’, ‘Phosphorus’, ‘Riboflavin (vitamin B2), ‘Iodine’, ‘vitamin B12’, ‘Pantothenic acid (vitamin B5) ‘Zinc’, ‘Potassium’ na ‘Molybdenum’. Mbali ya virutubisho hivyo, ndani ya mtindi kuna ‘bakteria hai’ ambao ni muhimu kiafya katika mwili. HUREFUSHA MAISHA Utafiti unaonesha kuwa unywaji wa mtindi mara kwa mara, hasa katika kundi la wazee, uwezo wa mwili wa kupambana na magonjwa mbalimbali umeonesha kuongezeka na kufanya mfumo wa kinga ya mwili kuwa imara zaidi. Katika utafiti mmoja, walichaguliwa wazee 162 ambao walipewa utaratibu wa kunywa mtindi na maziwa zaidi ya mara 3 kwa wiki na kufuatiliwa maendeleo yao kwa muda wa miaka mitano. Baadaye utafiti huo ulionesha kuwa idadi ya vifo vya wazee hao ilipung...
Maoni
Chapisha Maoni