Ndege ya abiria yaanguka katika uwanja wa ndege wa Wilson jijini Nairobi Kenya


HABARI ZA HIVI PUNDE
Ndege moja inayoendeshwa na kampuni ya Silverstone Air imeanguka katika uwanja wa ndege wa Wilson katika mji mkuu wa Nairobi nchini Kenya.
Walioshuhudia wanasema kwamba ndege hiyo ilipoteza mwelekeo wakati ilipokuwa ikipaa kuelekea Mombasa Ijumaa Alfajiri.
Picha kutoka eneo la mkasa zinaonyesha kwamba ndege hiyo ilianguka katika kichaka , ikigonga miti na kuvunja mojawapo ya mbawa zake kabla ya kuangukia ubavu mmoja.
Abiria mmoja ambaye alikuwa ameabiri ndege hiyo aliambia chombo cha habari cha Nation kwamba walikuwa bado hawajafika angani wakati rubani alipogundua matatizo.
Hakuna ripoti za moja kwa moja kuhusu majeruhi lakini abiria wengi walipatwa na mshtuko baada ya kunusurika kifo.
Kampuni ya ndege ya Silverstone , mamlaka ya ndege nchini Kenya KAA na uwanja wa ndege wa Wilson hazijatoa tamko lolote.
Vikosi vya kukabiliana na dharura katika uwanja huo wa ndege viliwaondosha abiria katika ndege hiyo na kuwakimbiza katika hospitali mbalimbali ili kufanyiwa vipimo.
Tutaendelea kukujuza kuhusu habari hiyo...

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA