Safari hii ya kihistoria inaweza kubadili mawazo ya Kim Jong-un kufanya majaribio ya makombora
Raisi wa Korea kaskazini Kim Jong-un amepanda mlima mrefu kuliko yote nchini humo kwa kutumia farasi.
Hii si mara ya kwanza kwa kiongozi huyo kufanya hivyo kwani alishawahi kupanda kilele urefu wa 2,750m huku dhumuni likiwa ni kufanya matangazo muhimu.
Mlima huo ni mahali ambapo baba wa kiongozi huyo wa Korea kaskazini alizaliwa huku pia ni kati ya vivutio vya nchi hiyo.
Kitendo cha kiongozi huyo kupanda mlima wa Paektu ni kitendo kikubwa cha kihistoria.
Kiongozi huyo ametafakari hatua iyo ya kupanda mlima Paektu kama kuongoza nchi hiyo huku akisema inahitaji kuwa imara kama mlima huo.
Mara ya mwisho Kim Jong-un kupanda mlima Paektu kumeleta matokeo makubwa na mipango mikubwa iliyofanywa na kiongozi huyo juu ya nchi hiyo.
Inasemekana kuwa kiongozi huyo safari hii, anaweza kubalisha mawazo yake juu ya majaribio ya makombora ya masafa marefu pamoja na silaha za nyuklia.
Huku mazungumzo na utawala wa marekani umetulia na rais wa marekani Donald Trump amekuwa akitingwa na shughuli nyingine za kinyumbani na mambo ya kigeni.
Inawezekana Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini amepanda mlima huo kama mbinu ya kuelekea kukubaliana na mawazo ya uongozi wa Trump.
Marekani imetakiwa kuja na suluhisho juu ya kusitisha mpango mzima wa nyuklia korea kaskazini, mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka katika mji muu wa korea kaskazini.
Kim amekuwa akikumbana na vikwazo mbele yake kabla hajatatua mgogoro huo wa nukliya, lakini amefeli kuwashawishi Marekani.
- Korea Kaskazini yafanya majaribio mawili ya makombora
- Korea Kaskazini na Marekani zafufua mazungumzo ya nyuklia
- Trump akutana na Kim kwenye mkutano wa kihistoria
Mwanzoni mwa mwezi huu, maafisa wa korea kaskazini walikutana na maafisa wa Marekani nchini Sweden huku ikiwa ni mara ya kwanza tangu raisi wa Marekani Donald Trump na Bw Kim walipokutana katika eneo la mpaka wa kati wa Korea mwezi juni.
Huku marekani ikidai kuwa 'maamuzi mazuri na ya busara yalifanyika'.
Ikumbukwe kuwa kabla ya mazungumzo hayo Korea Kaskazini ilirusha aina mpya ya kombora huku ikiwa ni zoezi la 11 kwa mwaka huu.
Maoni
Chapisha Maoni