Kero la ufisadi lawaingiza mitaani Wakatoliki DRC


Wakatoliki waandamana DRC kupinga ufisadi
Wakristo wa kikatoliki katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wamefanya maandamano katika maeneo mbali mbali ya nchi hiyo kupinga ufisadi.
Maandamano hayo ambayo yameitishwa na Kamati ya Katoliki ya Walei ambao wamewataka raia wa kongo kwa ujumla kuingia mitaani kupiga ufisadi na ukosefu wahaki za kisheria.
Walei ambao ni wakristo wa kawaida katika jamuhuri ya kidemokrasi ya kongo wanaaminiwa kuwa ndio waliomshinikiza aliyekuwa rais wa nchi hiyo Joseph Kabila kuacha azma yake ya kugombea muhula wa tatu madarakani.
Hii ni mara ya kwanza kwa Kamati ya Walei kuitisha maandamani chini ya utawala wa rais wa sasa Felix Tshiseledi.

Unaweza pia kusoma pia:

Wameitisha maandamano hayo ya amani kufuatia kupotea kwa dola milioni 15 kutoka benki ya taifa ya DRC na kuwekwa katika benki ya biashara kabla ya kutoweka kabisa.
Licha ya kilio cha umma ambao uliwataka wahusika wachukuliwe hatua, iwe rais Tshisekedi wala mahakama hawajatoa maelezo ya kutosha kwa umma juu ya sakata hiyo.
Wakatoliki hao wanasema wanakataa mtindo wa kutotokomeza rushwa uliotawala tawala zilizopita.
Walei wa kikatoliki pia wamewatolea wito "Wale wanaosita kuchukua uamuzi unaofaa kwasababu mapambano dhidi ya matatizo haya ni swala letu sote ".
Katika taarifa yake CLC imewataka watu kuandamanaji "kutojihusisha na aina yoyote ya ghasia, kuchoma mataili, na kuweka vizuizi vya barabarani
Image captionKatika taarifa yake CLC imewataka watu kuandamanaji "kutojihusisha na aina yoyote ya ghasia, kuchoma mataili, na kuweka vizuizi vya barabarani
Awali Gavana wa mji wa Kinshasa Gentiny Ngobila , pamoja na kamati ya uratibu ya Walei (CLC) walikubaliana kusitisha maandamano hayo mjini Kinshasa ili kuzuwia, yasifanyika siku Oktoba 19 Jumamosi ambayo ni siku ya ilipofanyika operation Kin Bopeto
Hata hivyo maandamano hayo yaliendelea katika maeneo mengine ya nchi kama ilivyopangwa.
Akizungumza na BBC mmoja wa viongozi wa wakatoliki hao Isidore Ndaywele Nziem alisema kuwa wanakerwa na ufisadi uliokithiri, ukiukaji wa sheria kwa kutowaadhibu wahalifu na kudorora kwa mfumo mzima wa sheria nchini DRC .
Walei wa Kikatoliki wanamlaumu rais Felix Tchisekedi kutoshughulikia ufisadi wa dola milioni 15 zilizotowekaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWalei wa Kikatoliki wanamlaumu rais Felix Tchisekedi kwa kutotoa maelezo yoyote kuhusiana na ufisadi wa dola milioni 15 zilizotoweka
Kamati ya Walei wa Kikatoliki DRC (CLC) imevipongeza vyama vya kisiasa, makundi ya raia pia mashirika yasiyo ya kiserikali waliopaza sauti zao kuunga mkono maandamano hayo.
Katika taarifa yake CLC imewataka watu "kutojihusisha na aina yoyote ya ghasia, kuchoma magurudumu, na kuweka vizuizi vya barabarani, kutotumia lugha ya matusi, kutorusha mawe na vitu vingine au kufanya uporaji wowote wa mali".wakati wa maandamano hayo.
Wanasema wanataka kutumia kusanyiko hilo kama,"mfano wa kutumia uhuru kwa uwajibikaji ili kuijenga jamii ambayo ni bora kuishi ".
Akizungumza na BBC mmoja wa viongozi wa wakatoliki hao Isidore Ndaywele Nziem alisema kuwa wanakerwa na ufisadi uliokithiri, ukiukaji wa sheria kwa kutowaadhibu uhalifu na kudorora wa mfumo mziwa wa sheria nchini DRC .
Maaskofu wa kanisa katoliki DRC
Image captionMaaskofu wa kanisa katoliki DRC

Nguvu ya maandamano ya kanisa katoliki katika DRC

Si mara ya kwanza kwa Kanisa katoliki kuitisha maandamano katika jamuhuri ya kidemokrasi ya Kongo kupinga kile ambacho linaona kuwa hakifai kwa jamii ya Wakongomani.
Ufaransa inaamini kuwashinikizo la Walei wa kanisa katoliki walimshinikiza Joseph Kabila kuacha azma yake ya kugombea muhula wa tatuHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUfaransa inaamini kuwashinikizo la Walei wa kanisa katoliki walimshinikiza Joseph Kabila kuacha azma yake ya kugombea muhula wa tatu
Mwanzoni mwa mwaka jana Maaskofu wa Kanisa hilo nchini DRC waliitisha maandamano dhidi ya rais Joseph Kabila, kumshinikiza aondoke madarakani na kutangaza kuwa hatawania urais mwezi Desemba mwaka 2018. Maandamano hayo yalifanyika katika miji mbalimbali nchini humo.
Mwishoni mwa mwaka 2017 kanisa hilo nchini DRC pia liliitisha maandamano yaliyosababisha vifo vya waandamanaji saba baada ya makabiliano kati ya polisi na waandamanaji.
Polisi wa kupambana na ghasia walikabiliana na waumini wa Kanisa hilo waliokuwa wamemaliza ibada ya kuwaombea waumini waliouawa na kusababisha baadhi yao kujeruhiwa kwa hofu kuwa wangeandamana jijini Kinshasa.
Maaskofu wa Kanisa Katoliki wakati huo walisema, hawatachoka kushinikiza mabadiliko nchini DRC, na kumshinikiza rais Kabila ambaye alikuwa madarakani tangu mwaka 2001.
Ufaransa inaamini kuwa maandamano hayo na msukumo wa walei wa Kikatoliki ni mojawapo ya sababu zilizomsukuma Bwana Kabila kusitisha nia yake ya kugombea muhula wa tatu madarakani.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA