Ndege ya C-130: Mabaki yake yapatikana yakiolea katika maji Chile



Mabaki ya ndege ya C- 130 yakiolea karibu na eneo ambalo ndege hiyo ilitowekaHaki miliki ya picha
Image captionMabaki ya ndege yalipatikana yakiolea katika eneo ambalo ndege hiyo ilitoweka siku ya Jumatatu.
Maafisa wa Chile wanasema kwamba wamezuia mabaki yanayoaminika kutoka katika ndege ya kijeshi iliotoweka siku ya Jumatatu.
Wanasema kwamba mabaki hayo yalipatikana yakiolea kilomita 30 kutoka eneo ambalo ndege ya wanahewa wa Chile aina ya C-130 Hercules inayobeba mizigo ilikuwa na mawasiliano ya mwisho.
Vifusi hivyo vilipatikana katika maji yanayojulikana kama mkondo wa Drake.
Ndege hiyo ilikuwa imetoka mji wa kusini wa Chile wa Punta Arenas ikielekea katika kambi ya kijeshi ya Antarctica ambapo rais wa taifa hilo Eduardo Frei Montalva alikuwa.
Vifusi hivyo huenda vinatoka kutoka tangi la mafuta la ndege hiyo , kulingana na kamanda wa jeshi la wanahewa Eduardo Mosqueira ambaye alikuwa akizungumza na wanahabari siku ya Jumatano.
Bwana Mosqueira alisema kwamba jeshi la wanahewa litafanya uchunguzi kubaini iwapo mabaki hayo yalikuwa ni yale ya ndege hiyo.
Ramani ya picha iliotolea na anahewa wa Chile tarehe 10 Disemba 2019 ikionyesha mara ya mwisho ndege hiyo ya C-130 ilipokuwaHaki miliki ya picha
Image captionRamani ya picha iliotolea na anahewa wa Chile tarehe 10 Disemba 2019 ikionyesha mara ya mwisho ndege hiyo ilipokuwa
Ndege hiyo ilipoteza mawasiliano mwendo wa saa kumi na mbili za jioni siku ya Jumatatu muda mfupi baada ya kupaa kutoka mji wa Punta Arenas.
Jeshi la anahewa wa Chile lilitoa ramani ya njia iliofuata ndege hiyo na muda wake kwamba ilitarajia kutua mwendo wa saa moja na dakika 17 siku ya JUmatatu katika kambi hiyo ya Eduardo Frei Montalva.
Usakaji wa angani na baharini tayari umeanzishwa muda mfupi baada ya ndege hiyo kutoweka.
Argentina, Brazil, Uingereza na Uruguay zimetuma ndege kusaidia katika utafutaji wa ndege hiyo katika maji hayo ya barafu huku Marekani na Israel zikitoa picha za setlaiti.

Nani aliyekuwa ameabiri ndege hiyo?

Watatu kati ya abiria hao walikuwa wanajeshi wa Chile, raia wawili walioajiriwa na kampuni ya uhandisi na ujenzi Inproser waliokuwa wakielekea kufanya kazi katika kambi hiyo ya kijeshi, mwanafunzi mmoja na abiria 15 waliosalia walikuwa wanahewa kulingana na maafisa.
Ndege hiyo ya C- 130 hutumika kusafirisha watu na mizigo katika eneo la AntarcticaHaki miliki ya picha
Image captionNdege hiyo ya C- 130 hutumika kusafirisha watu na mizigo katika eneo la Antarctica
Ignacio Parada aliyekuwa akisomea uhandisi katika chuo kikuu cha Magallanesna alikuwa akielekea katika kambi ya Antarctic base kwa masomo ya kujipatia uzoefu.
Walimu wake walimtaja mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 24 kuwa ''mwanafunzi bora".
Alikuwa akipendelea kusomea kawi , kulingana na hotuba yake aliotoa kwa chuo hicho hivi karibuni.
Mfanyakazi wa Inproser Leonel Cabrera na Jacob Pizarro walikuwa wakielekea kufanya kazi katika kambi hiyo ya kijeshi.
Ndugu na jamaa za waathiriwa wamekuwa wakisubiri katika kambi ya wanahewa ya CerrilosHaki miliki ya picha
Image captionNdugu na jamaa za waathiriwa wamekuwa wakisubiri katika kambi ya wanahewa ya Cerrilos
Wanajeshi hao watatu waliokuwa wameabiri ndege hiyo siku ya Jumatatu walikuwa kanali Christian Astorquiza, Luteni kanali Oscar Saavedra na meja jenerali Daniel Ortiz.
Kulikuwa na mwanamke mmoja pekee katika ndege hiyo: Claudio Manzo mwenye umri wa miaka 37 ambaye alijiunga na wanahewa hao mwaka 2008 na alikuwa akipendelea kusafiri kwa ndege ili kufanya uchunguzi ardhini kwa lengo la kupata habari kutoka maeneo yalio mbali.
Pia miongoni mwa wale walikuwa wakisafiri ni Luis Jeremias Mancilla. Jeremia mwenye umri wa miaka 27 alikuwa ameajiriwa na jeshi kufanya kazi ya kuunganisha umeme katika kambi hiyo .
Nduguye mkubwa Luis ni sajenti katika jeshi hilo la wanahewa.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Ujerumani yanyakua Kombe la nne la Dunia