HEBU MCHEKI NINJA HUYU TOKA JAPANI! UBUNIFU UNALIPA SAAAANA!


Eimi Haga became interested in ninjas by watching "Nintama Rantaro" on TV
Image captionEimi Haga alianza kuvutiwa kuangalia vipindi vya ninja tangu akiwa mtoto mdogo
Mwanafunzi mmoja wa Japani amefaulu mtihani wake kwa kiwango cha juu kwa kutumia mbinu za kihistoria za ninja - mara baada ya mwalimu wake kugundua kuwa aliandika insha yake kwa wino usioonekana.
Eimi Haga alitumia mbinu alizotumia ninja "aburidashi", kwa kutumia muda mwingi kutengeneza wino kwa maharage ya soya.
Maneno yake yalionekana wakati ambapo profesa wake alipoliunguza karatasi katika jiko la gesi.
"Ni kitu ambacho nilijifunza nikiwa mdogo," Bi. Haga aliiambia BBC. "Ninadhani kuwa hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kuja na wazo la aina hiyo."
Bi. Haga amekuwa akivutiwa na simulizi za 'ninja' katika vipindi vya televisheni tangu alipokuwa mtoto mdogo.
Baada ya kujiunga na chuo kikuu cha Mie nchini Japan, alichagua darasa la historia ya ninja na alitakiwa kuandika kuhusu makumbusho ya Ninja ya Igaryu aliyowahi kuyatembelea.
"Wakati profesa aliposema kuwa atatoa alama nzuri kwa mwanafunzi atakayekuja na ubunifu wa aina yake, nilijikita kuwa insha yangu lazima niiandike vizuri zaidi ya wengine," alisema mwanafunzi huyo.
"Nilifikiria kwa muda, na kuamua kuandika kuhusu wazo la ninja aburidashi."
The essay, showing the heated and unheated sections
Image captionInsha ikionesha sehemu iliyopata moto
Bi. Haga, 19, aliloweka maharage ya soya usiku mzima na baadae kuyasugua na kuyapondaponda kwenye nguo.
Alichanganya maharage na na maji na kusubiri kwa saa mbili kabla hajaanza kuweka umakini katika kuandika insha yake kwa kutumia brashi kwenye karatasi nyembamba ya jadi ijulikanayo kama"washi".
Kipindi ambacho maneno yalikuwa yamekauka yalikuwa hayaonekani.
Lakini profesa hakutupa karatasi kwenye takataka, kwa sababu kulikuwa na ujumbe ulioandikwa kawaida kuwa liweke karatasi kwenye moto."
Presentational grey line

Ninja ni nani?

  • Ni mtu shujaa na anatumia mbinu zake mwenyewe kupambana katika vita.
  • Ni utamaduni wa Japan ulioanza miaka mingi iliyopita
  • Ninja ni wataalamu wa kuwa na mbinu mbalimbali za kupigana
  • Ninja ilianza kuwa maarufu katika sinema za Marekani lakini ninja wanaotumika katika taswira za Hollywood inawatambulisha ndivyo sivyo.
Presentational grey line
Profesa, Yuji Yamada, aliiambia BBC kuwa alishangazwa sana na ubunifu huo wakati alipoiona insha hiyo.
"Niliona ripoti hiyo ikiwa imeandikwa kwa mfumo maalum lakini sikuwahi kuona ikiwa imeandikwa kwa maneno yasioonekana," alisema mwalimu.
"Kusema kweli nilikuwa nna wasiwasi kidogo kama maneno yataonekana vizuri, lakini nilipoanza kuliweka karatasi kwenye moto wa jiko la gesi nilipokuwa nyumbani , maneno yote yalionekana vizuri sana!!!"
"Sikufikiria mara mbili kumpa alama za juu kabisa kwa kazi aliyoifanya, sikusoma hata maelezo yote mpaka mwisho, nilidhani kuwa ni vyema kutounguza karatasi lote, ili kama waandishi wa habari wakitaka kuona na kupiga picha wawe na ushaidi".
Bi. Haga aliandika insha yake kwa mtiririko mzuri na wa kipekee.
" Niliamini kwamba profesa angeweza kutambua jitihada nilizotumia kuandika insha yenye ubunifu," alisema mwanafunzi huyo.
"Sikuwa na hofu ya kupata alama mbaya katika insha yangu - ingawa maudhui yenyewe yalikuwa hayana upekee wowote."

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA