TRUMP AWATUSI DEMOCRATIC! SASA MAJI YAKO SHINGONI


TRump
Rais wa Marekani Donald Trump amekasirishwa na Democrats mara baada ya chama hicho kutangaza kupeleka nakala za ushaidi dhidi yake katika ikulu ya taifa hilo wiki hii.
Kamati inazitaka nakala hizo ili kuzihusisha na shutuma dhidi ya utawala wa Marekani na Ukraine , kesi ambayo sasa ndio muhimili wa madai dhidi ya rais.
Rais Trump amewashutumu viongozi wa Democratic kwa waongo na wanafanya uhaini mkubwa.
Democrats imetetea madai yao kwa kuangazia majadiliano ya simu kati ya rais wa Marekani na rais wa Ukraine.
Trump amesema nini?
Katika mkutano na waandishi wa habari, Trump alionyesha hasira yake wazi kwa mwenyekiti wa kamati ya kiintelijensia Adam Schiff, kwa kumtusi na kumtaka ajihuzuru wadhifa wake kwa sababu ni mtu wa hali ya chini na fedheha.
"Kiukweli, inabidi wamuangalie kama mtu aliyefanya kosa la uhaini" Trump aliongeza.
Trump alisema pia kuwa anaamini kuwa bwana Schiff alisaidiwa kuandika madai hayo na watu ambao hawakumpa ushaidi.
Rais ametaka mtoa taarifa za ukweli pekee ndio anapaswa kulindwa.
"Nchi hii inapaswa kuwabaini mtu huyo kwa sababu mtu huyo ni mpelelezi, kwa maoni yangu," Trump alisema.
Na kudai kuwa shutuma zote hazina ukweli na zinajumuisha uhalifu kwa watu wa Marekani, ingawa siku zote wataendelea kushirikiana na Congress .
Rais Trump aling'aka na swali aliloulizwa na mwandishi wa Reuters kuhusu vigezo vya mtu mhaini.
Kama mnavyoniona kuwa kiongozi niliyeshindwa, kuna watu ambao wanadhani kuwa mimi ni kiongozi mwerevu sana na labda nitaweza kutenda haki kisheria dhidi ya wahusika katika uchunguzi wa Urisi.
Mwandishi alimkatisha Trump kwa kumwambie apunguze jazba: "Usiwe mkali."
Awali rais Trump aliwatupia maneno makali wawakilishi wa Democratic ,Spika Bi. Nancy Pelosi na mwenyekiti wa kamati ya uchunguzi Adam Schiff, kupitia ukurasa wake wa Twitter na kudai kuwa Democrats inafuatilia upumbavu.
Trump alimwambia bi.Pelosi kuwa ingekuwa vyema kwa Bi.Pelosi kuupa kipaumbele mji wake wa San Francisco, ambao unatajwa kuwa mji maskini wenye watu wasiokuwa na makazi.
Presentational white space
House Intelligence Committee Chairman Adam Schiff (D-CA) joins Speaker of the House Nancy Pelosi to speak about Democratic legislative priorities and the impeachment inquiryHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMweyekiti wa kamati ya kiintelijensia,Adam Schiff and Spika Nancy Pelosi
Wabunge wa chama cha Democrats katika bunge la Congress wanasema kwamba simu hiyo iliofichuliwa ni thibitisho kwamba rais Trump alitoa shinikizo kwa taifa jingine kwa manufaa yake ya kibinafsi.

Ni shutuma gani inamkabili rais Trump

Shutuma dhidi ya rais Trump ambayo inaweza kumuondoa madarakani ,inakuja kufuatia mazungumzo ya simu kati ya rais Trump na kiongozi wa Ukraini rais Volodymyr Zelensky Julai 25.
Katika mazungumzo hayo ya simu, Trump alimshinikiza rais wa Ukraine kufanya uchunguzi wa kashfa za rushwa dhidi ya mpinzani wake Joe Biden na mtoto wake, ambaye anafanya kazi katika kiwanda cha gesi nchini Ukraini.
Hakuna ushaidi wowote mbaya ambao ulitolewa dhidi ya akina Biden.
Democrats wametaja kuwa rais Zelensky alifanya hivyo wakati huohuo ambao rais Trump aliamua kuondoa msaada wa kijeshi nchini Ukraini.
Wapinzani wa Trump wanasema kuwa Trump alikuwa anatafuta washirika ambao wangeweza kumsaidia katika uchaguzi wa urais kwa mwaka 2020 kwa ajili ya manufaa yake mwenyewe.
Presentational grey line
Athari za uchunguzi dhidi ya Trump
President Donald Trump addresses a joint news conference with Finland"s President Sauli Niinisto in the East Room of the White HouseHaki miliki ya pichaREUTERS
Uhalifu anaoshutumiwa nao Trump unaweza kumuondoa rais madarakani, na unapitia hatua mbili za mchakato wa kisiasa.
Kama kura za wawakilishi hazitatosha, basi bunge la seneti litalazimika kusimamia kesi hiyo.
Kura ya seneti inahitaji walau wingi wa theluthi mbili ya wingi - na inaweza kushindwa kwa sababuchama cha Trump kina maseneta wengi zaidi.
Ni marais wawili tu katika historia ya Marekani ambao ni Bill Clinton and Andrew Johnson ambao walikabiliana na kesi ya namna hiyo na hakuna kati yao ambaye alishtakiwa au kuondolewa madarakani.
Rais Nixon alijiondoa madarakani kabla ya kung'olewa na bunge.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA