Picha iliyochorwa kwa mashine yatolewa kumuonesha mtu aliyeanguka kutoka kwenye ndege


Picha ya mashine inayomuonyesha mwanaume huyo anayekisiwa kuwa na miaka 30Haki miliki ya pichaMET POLICE
Polisi wanatafuta msaada kumtambua mtu mmoja aliyeanguka jijini London kutoka kwenye Ndege akitokea Kenya.
Maafisa walitaarifiwa mnamo mwezi Juni, kuhusu kupatikana kwa mwili wa mtu huyo, anayeaminika kuwa na umri wa miaka 30.
Mwanaume huyo anadhaniwa kuwa alianguka kutoka kwenye sehemu ya mbele ya ndege iliyokuwa ikielekea uwanja wa ndege wa Heathrow.
Maafisa wa uchunguzi wametoa picha ya mashine ya inayomfanana mtu huyo.
Wachunguzi hao wamesema wanahisi mtu huyo ni raia wa Kenya lakini ''hawana uhakika''
MkobaHaki miliki ya pichaMET POLICE
Maafisa pia walitoa picha za mkoba ambao ulipatikana katika eneo la mbele la ndege, ndege ilipotua.
Mkoba huo ulikutwa na fedha kiasi za Kenya, na chapa ya MCA Polisi wameeleza.
Chupa mbili, jozi ya viatu,mfuko na sarafuHaki miliki ya pichaMET POLICE
Afisa wa polisi Paul Graves: ''tumefanyia uchunguzi tukio hili linalosikitisha''
''Mwanaume huyu ana familia mahali ambayo ingependa kufahamu mpendwa wao amepatwa na nini.
''Uchunguzi wetu umehusisha pia mawasiliano na mamlaka za Kenya, ambako ndege hiyo ilianzia safari yake, lakini mpaka sasa jitihada za kumtambua ziligonga mwamba.''
Mkanda wa mkoba ulikuwa na chapa za herufi MCA

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA