KWANINI WAKURDI WANAOGOPWA SANA ?
jeshi la Uturuki lililoingia kaskazini mashariki mwa Syria tarehe 9 Oktoba , kwa lengo la kubuni "eneo salama " liliwaondosha wanamgambo wa Kikurdi.
Wakosoaji wanahofia kwamba operesheni hiyo ilisababisha kumalizwa kwa Wakrdi nchini humo na kubuniwa kwa kundi la Islamic State (IS).
Lakini Wakurdi ni akina nani , na ni kwanini rais wa uturuki Recep Tayyip Erdogan anahisi haja ya "kuzuwia kubuniwa kwa ushoroba ugaidi " kwenye mpaka?.
Unaweza pia kusoma:
- Harmonise apigiwa debe na rais Magufuli
- Uturuki yadai kutotishika na vikwazo vya Marekani
- Tetesi za soka Ulaya Jumatano tarehe 16.10.2019
Wakurdi wanatoka wapi ?
Wakurdhi ni miongoni mwa wazawa wa maeneo tambalale ya milima ya Mesopotamian katika kile ambacho sasa ni eneo lililopo kusini -mashariki mwa Uturuki, kaskazini mashariki mwa Syria , kaskazini mwa Iraq na kusini -magharibi mwa Armenia.
Kati ya Wakurdi milioni 25 na 35 wanaishi katika maeneo ya milima , na hivyo kulifanya kabila kubwa zaidi katika eneo la mashariki ya kati .
Lakini Wakurdi hawajawahi kupata taifa lao la kudumu.
Leo wanaunda jamii ya kipekee inayoungana kutokana na asili yao , utamaduni na lugha , ingawa hawana lugha yao rasmi . Pia ni waumini wa dini tofauti , ingawa wengi wao n waunini wa madhehebu ya waislamu wa Sunni
Ni kwanini hawana taifa?
Katika miaka ya mwanzo ya karne ya 20th C, wakurdi wengi walianza kuangalia uwezekano wa kubuni eneo lao - ambalo lilinatakumbuliwa kama - "Kurdistan".
Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia na kushindwa kwa himaya ya Ottoman, washirika wa magharibi waliokuwa wameshinda, waliweka kipengele kwa ajili ya taifa la Wakurdi katika mkataba wa 1920 wa Sevres.
- Trump aionya Uturuki isithubutu kuwashambulia Wakurdi Syria
- Syria wamechukua karibu udhibiti wote wa mji wa Manbij
Maumaini hayo yalitoweka miaka mitatu baadae Swakati mkataba wa Lausanne, ambao uliweka mipaka ya Uturuki ya sasa , ulipoondoa kipengele kuhusu kuundwa kwa taifa la Kikurdi na hadhi ya walio wachache katika mataifa yao.
Zaidi ya mika 80 iliyofuatia , hatua yoyote ya Wakurdi ya kuunda taifa huru ilipingwa kwa ukatili.
Ni kwanini Uturuki inawaona Wakurdi kama tisho ?
Kuna uhasama mkubwa na muda mrefu baina ya taifa la Uturuki na Wakurdi wa nchi hiyo ambao ni asilimia kati ya 15% hadi 20% ya Waturuki.
Wakurdi walidhulumiwa kikatili katika mikono ya maafisa wa Uturuki kwa miaka mingi. Kujibu harakati za mageuzi ya kisasa katika miaka 1920 na 1930 , Wakurdi wengi waliwalipewa majina ya Kikurdi na mavazi ya suti yakapigwa marufuku na ikawa ni sheria kuzungumza lugha ya Kikurdi tu na hata kuwepo kwa utambulisho wa kabila la Kikurdi kukakataliwa wakapewa jina la watu ''wanaotoka katika mlima wa Uturuki''
Mnamo mwaka 1978, Abdullah Ocalan alianzisha kundi la PKK, ambacho kilitoa wito wa kuwepo kwa taifa huru ndani ya uturuki . Miaka sita baadae kikundi hicho kilianza mapigano , zaidi ya watu 40,000 na wengine mamia kadhaa wakasambaratishwa .
Katika miaka ya 1990 PKK walianza tena kudai uhuru , wakitaka zaidi kujitenga kiutamaduni na kisiasa, lakini wakaendela na mapigano. Mnamo mwaka 2013, makubaliano ya kusitisha mapigano yalifikiwa baada ya kufanyika kwa mazungumzo ya siri .
hata hivyo makubaliano hayo yalivunjika Julai 2015, baada ya mashambulio ya kujitolea muhanga ambayo ilidaiwa yalifanywa na IS kuwauwa wanaharakati vijana 33 katika mji unaokaliwa zaidi na Wakurdi wa Suruc, karibu na mpaka wa Syria. PKK walizishutumu mamlaka kwa kuhusika na wakawashambulia wanajeshi wa Uturuki na polisi.
Serikali ya Uturuki ilifanya mashambulio ya mara kwa mara katika kile ilichokiita "vita maalumu dhidi ya ugaidi " dhidi ya PKK na IS.
Tangu wakati huo , maelfu kadhaa ya watu - wakiwemo mamia ya raia wamekuwa wakiuawa katika makabiliano yanayoendelea kusini - mashariki mwa uturuki.
Uturuki iliimarisha uwepo wa vikosi vyake magharibi mwa Syria tangu Agosti 2016, wakati ilipotuma majeshi na vifaru kwenye mpaka na kuuteka mji muhimu wa Jarablus.
Hii ililizuwia kundi linaloongozwa na YPG la SDF kuchukua eneo lenyewe na kulihusisha na wakurdi.
Mnamo mwaka 2018, wanajeshi wa Uturuki na waasi wanaounga mkono serikali ya Syria waliwafukuza wapiganaji wa YPG kutoka eneo la Afrin. Makumi ya raia waliuawa na maelfu kwa maelfu wakayatoroka makazi yao.
Serikali ya Turkey inasema kuwa makundi ya Wakurdi wa Syria, YPG na PYD, ni matawi ya PKK, na yote yana lengo moja la kuchukua mamlaka kwa njia ya mapigano na ni makundi ya ugaidi ambayo hayanabudi kumalizwa
Ni nini wanachokitaka Wakurdi wa Syria ?
Wakurdi ni kati ya 7% na 10% ya Watu wa Syria . Kabla ya harakati za mageuzi dhidi ya rais President Bashar al-Assad zilianza mwaka 2011 wengi walikuwa wanaishi katika miji ya Damascus na Aleppo, na katika miji mingine mitatu iliyopo katika majimnbo ya Kobane, Afrin, na mji wa kaskazini-mashariki wa Qamishli.
Wakurdi wa Syria wamekuwa wakinyanyaswa kwa muda mrefu na kunyimwa haki zao za msingi . takriban Wakurdi 300,000 wamenyimwa uraia tangu miaka ya 1960 na ardhi ya Wakurdi iligawiwa upya kwa Waarabu katika jaribio la kuyafanya maeneo ya Wakurdi kuwa ya "Waarabu"
Wakati harakati zilipobadilika na kuwa vita vya kiraia , vyama vikuu vya kikurdi viliepuka wazi kuonyesha viko upande gani kisiasa.
Katikati ya mwaka -2012, vikosi vya serikali vilijiomndoa ili kuimarisha mapambano dhidi ya waasi kwingineko, na makundi ya Wakurdi yakachukua udhibiti.
Mwezi Januari 2014, vyama vya Kikurdi kikiwemo chama chenye ushawishi zaidi cha (PYD) - vilitangaza kuundwa kwa "utawala wa kujitegemea " katika majimbo matatu Afrin, Kobane na Jazira.
Mwezi Machi 2016, walitangaza azimio la kuanzishwa kwa "mfumo wa shirikisho " ambao ulijumuisha maeneo ya zaidi waarabu na Waturuki a yaliyokamatwa na IS.
Azimio hilo lilikataliwa na serikali ya Syria , upinzani wa Syria na Marekani .
Chama cha PYD kinasema hakitaki uhuru , lakini kinasisitiza kuwa makubaliano yoyote ya kisiasa ya kumaliza mzozo nchini Syria ni lazima yajumuishe hakikisho la kisheria kuhusu haki za Wakurdi na kuyatambua maeneo ya Wakurdi kama yanayojitawala.
Rais Assad ameapa kuirejesha "kila sehemu " ya ardhi ya Syria , iwe kwa njia ya mazungumzo au kwa nguvu za kijeshi . Serikali yake pia imekataa madai ya Wakurdi ya kujitawala , ikisema kwamba "hakuna mtu nchini Syria anayekubali kuzungumzia kuhusu uhuru au shirikisho".
Maoni
Chapisha Maoni