RWANDA IMETISHA! NCHI YA KWANZA AFRICA KUTENGENEZA SIMU ZA SMARTPHONE, CHEKI HAPO CHINI.


Rwanda yatengeza simu aina ya smartphoneHaki miliki ya pichaIKULU YA RAIS RWANDA
Kampuni ya Mara nchin Rwanda imezindua simu mbili aina ya smartphone , ikitaja kuwa za kwanza 'kutengezwa barani Afrika' hatua inayopiga jeki maono yake ya kuwa bingwa wa maswala ya kiteknolojia katika eneo hili kulingan na chombo cha habari cha Reuters.
Simu hizo kwa jina Mar X na Mara Z zitatumia mfumo wa Google wa Android na kugharimu $ 190 na $ 130 matawalia.
Zitashindana na simu za kampuni ya Samsung , ambazo simu yake ilio bei rahisi zaidi ni $54 huku simu nyengine zisizo na nembo zikigharimu $37.
Kulingana na Reuters afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya Mara Ashish Thakkar amesema kwamba anawalenga wateja walio tayari kulipa zaidi kwa bidhaa za hali ya juu.
''Hii ni aina ya kwanza ya simu ya smartphone barani Afrika'', Thakar aliambia chombo cha habari cha Reuters baada ya kutembelea kampuni hiyo akiandamana na rais wa taifa hilo Paul Kagame.
''Kampuni hununua na kuunganisha vifaa vya simu nchini Misri, Ethopia , Algeria na Afrika Kusini'', alisema. Sisi ni wa kwanza kutengeza vifaa hivyo hapa Afrika.
''Tunatengeza bodi muhimu ya tarakilishi ya simu hizo { motherboards} mbali na bodi ndogo {sub Boards} za simu hizo wakati wa mchakato wote'', alinukuliwa na Reuters akisema kuna zaidi ya vipande 1000 kwa simu moja.
Baadhi ya simu hizo zikionyeshwaHaki miliki ya pichaIKULU YA RAIS RWANDA
Thakkar alisema kwamba kiwanda hicho kimegharimu dola milioni 24 kujenga na kinaweza kutengeza simu 1,200 kwa siku.
''Kampuni ya Mara inalenga kujipatia faida kutokana na makubaliano ya biashara huru katika bara hili, mwafaka unaolenga kujenga umoja wa mataifa 55 wa kibiashara ili kupiga jeki mauzo kote barani Afrika'' , alisema Thakkar.
Kulingana na Ruters Makubaliano hayo yanatarajiwa kuanza kutekelezwa mwezi Julai mwaka ujao , yakilenga kuunganisha takriban watu bilioni 1.3.
Lakini upo katika awamu za kwanza hivyobasi hakuna muda uliotolewa kufutilia mbali kodi.
Kagame amesema kwamba anatumai kwamba simu hizo zitaongeza utumizi wa simu aina ya smartphone miongoni mwa raia wa Rwanda ulio asilimia 15 kwa sasa.
''Raia wa Rwanda tayari wanatumia simu aina ya smartphone lakini tunataka wengi watumie. Uzinduzi wa simu za Mara zitawafanya raia wengi wa Rwanda kumiliki simu zaidi ya aina hizo'', alisema Kagame.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA