Origino Komedi wamwagwa na MENEJA wao
KUNDI
maarufu la vichekesho ambalo kwa sasa ni kama halipo, limepata pigo
kubwa baada ya aliyekuwa meneja wao, mtangazaji nyota wa zamani wa
televisheni, Christina Mosha maarufu kama Seven, kuwamwaga na hivyo
kuachana nao.
Akizungumza
na mwandishi juzikati, Seven alisema ameachana nao baada ya mkataba
wake wa sasa kumzuia kufanya kazi na watu wengine zaidi ya walio chini
ya mwajiri wake mpya.
“Hivi
sasa niko na Sony, wao wananizuia kufanya kazi na wasanii ambao hawako
nao, hivyo baada ya mkataba wangu na wao kumalizika, nimeamua kuachana
nao.
“Mimi
ni mwakilishi wa Sony barani Afrika, ninashughulika na wasanii toka
nchi tofauti za Afrika, kama Senegal, Kenya na kwingineko kasoro Afrika
Kusini,” alisema.
Aliyekuwa
meneja wa kundi la Ze Comedi, mtangazaji nyota wa zamani wa
televisheni, Christina Mosha maarufu kama Seven akifafanua jambo.
Maoni
Chapisha Maoni