MADAI YA NDOA YA JIDE KUVUNJIKA, GARDNER AFUNGUKA


Na Ojuku Abraham na Gladness Mallya
HABARI kubwa ya mjini hivi sasa, hasa kwenye mitandao ya kijamii ni juu ya madai mazito ya kuvunjika kwa ndoa ya selebriti wawili Bongo, staa wa muziki wa Kizazi Kipya, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au ‘Jide’ na mtangazaji maarufu wa Radio Times FM, Gardner G. Habash, iliyofungwa Mei 14, 2005, Ijumaa linamaliza utata.
Staa wa muziki wa Kizazi Kipya, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au ‘Jide’ akiwa na  mumewe Gardner G. Habash wakati wa harusi yao.
KABLA
Kabla ya Gardner kufunguka, habari zilidai kwamba wawili hao walikuwa kwenye gogoro zito ambapo Gardner aliamua kuondoka katika nyumba waliyokuwa wakiishi pamoja iliyopo Kimara-Temboni, Dar.
Ilidaiwa kwamba baada ya kuondoka nyumbani eti Gardner alikwenda kukaa kwa mmoja wa ndugu zake.
Habari hizo za kwenye mitandao ambazo hazitaji chanzo cha kuvunjika kwa ndoa hiyo, zilidai watu wa karibu na familia hiyo walisema hiyo siyo mara ya kwanza kwa wawili hao kutengana, lakini mzozo wa safari hii unaweza ukawa wa moja kwa moja.
ACHA BWANA!
Ilidaiwa kwamba ni kutokana na kutemana huko, ndiyo maana Jide msanii anayetajwa kuwa ni miongoni mwa wenye mafanikio kimaisha Bongo, hakwenda Kituo cha Polisi Oysterbay, Dar kumwangalia mumewe ambaye aliwekwa korokoroni kufuatia kitendo chao cha kuwakimbia askari wa usalama barabarani akiwa na Ephraim Kibonde hivi karibuni.
Maselebriti, ‘Lady Jaydee’ au ‘Jide’ na Gardner G. Habash wakipata ukodaki kwenye Red kapeti.
MAFUMBO?
Ilisemekana kuwa hisia za kuachana huko zinachochewa pia na baadhi ya maandiko ambayo mwanamuziki huyo wa Kibao cha Yahaya, amekuwa akiyaweka katika akaunti zake za mitandao katika siku za hivi karibuni.
Ilielezwa kwamba katika akaunti yake ya Mtandao wa Istagram, Jide aliweka picha yake akiwa amesimama nje ya gari lake kisha akasindikiza kwa kuandika hivi: “Walking away from troubles”, maneno ambayo kwa tafsiri isiyo rasmi yanamaanisha kujiondoa kwenye matatizo.
BINTI MACHOZI?
Ilidaiwa kuwa kabla ya hapo, katika mitandao inaandikwa kuwa Jide pia aliweka picha yake akionekana kuwa na huzuni huku Binti Machozi akilengwalengwa na machozi na kusindikizia na maneno akiuliza: “Sijui nisemaje?”
IJUMAA MZIGONI
Kufuatia tetesi hizo, gazeti hili liliamua kuzifanyia kazi ili kupata ukweli.
GARDNER ANASEMAJE?
Mtu wa kwanza kupigiwa simu alikuwa ni Gardner ambaye aliipokea na kabla hajaelezwa chochote, alisema alikuwa katika sehemu ambayo asingeweza kuzungumza, hivyo angempigia mwandishi wetu baada ya robo saa.
JIDE VIPI?
Baada ya kukata simu, mwandishi wetu alimwendea hewani Jide na baada ya kuita kwa muda, simu yake ilipokelewa na Gardner akasema: “Mpigie baada ya robo saa.”
‘Lady Jaydee’ au ‘Jide’ akipozi.
DAKIKA 20 BAADAYE, GARDNER AFUNGUKA
Dakika ishirini baadaye, Gardner alimtumia ujumbe mfupi wa simu mwandishi wetu na kumweleza kuwa alikuwa Kituo cha Polisi Oysterbay, Kinondoni jijini Dar ambako aliitwa kwa ajili ya soo lao la kuwakimbia trafiki.
Baada ya kubadilishana maneno kadhaa, baadaye aliamua kupiga na mazungumzo kati yake na Ijumaa yalikuwa kama ifuatavyo;
Ijumaa: Ebwana hivi hizi habari kwenye mitandao juu ya kuvunjika kwa ndoa yako na Jide zimekaaje?
Gardner: Hamna kitu bwana, watu wanaunganisha tu vitu sijui kwa sababu gani.
Ijumaa: Sasa kama ni hivyo kwa nini Jide hakuja kukuona siku ile ulipolala polisi?
Gadner: Unaona sasa, wao wanajua hivyo, lakini siyo kweli, Jide alikuja usiku sana kwa sababu alikuwa anawaogopa mapaparazi.
Unajua Jide yeye huwa hapendi hayo mambo. Alikuja usiku sana, lakini hata hivyo polisi nao walimgombea sana kumpiga picha.
Ijumaa: Wanasema Jide kuna maneno amepost kwenye akaunti zake mitandaoni zinazoonyesha kuchoshwa na wewe, unasemaje?
Gardner: Si ndiyo kama hivyo nimekuambia, watu wanaungaunga tu vitu ambavyo hawavijui na sisi hata hatujui malengo yao.
Wakati ule uliponipigia simu mara ya kwanza nilikuwa naye kwenye gari ananipeleka pale polisi, lakini akapaki mbali kwa sababu hiyohiyo niliyokuambia kuogopa mapaparazi na si unakumbuka hata ulipompigia kwenye namba yake nilipokea mimi?
Ijumaa: Kwani upo naye hapo sasa hivi nimsalimie?
Gardner: Hapana tumeachana mimi niko kwenye usafiri mwingine naelekea kazini na yeye yupo kwenye misele mingine.
Ijumaa: Haya kaka basi poa.
Gardner: Poa kaka, mchana mwema.
HUKO NYUMA
Si mara ya kwanza kwa mastaa hao kudaiwa kutibuana kwani walisharipotiwa kutaka kutengana lakini mara nyingi huwa wanakaa chini na kuyamaliza kimyakimya.
JIUNGE NA GUIJI LA HABARI!

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA