Binti: Binamu Yangu Amenibaka na Kunipa Mimba
Mkazi
mmoja wa kijiji cha Mloe, mkoani Kilimanjaro aliyejulikana kwa jina
moja la Agustin (47) anadaiwa kumbaka na kumpa mimba binamu yake mwenye
umri wa miaka 16 (jina linahifadhiwa) aliyekuwa kidato cha pili katika
shule ya sekondari ya Okaoni Septemba mwaka jana huko Dakau, Kibosho.
Akielezea
tukio hilo, msichana huyo ambaye sasa amejifungua, alisema shangazi
yake ambaye hana msaidizi nyumbani kwake, alimpigia simu bibi yake
anayeishi naye, akimuomba yeye aende kumsaidia kufua nguo.
Alipokwenda, kwanza aliambiwa atoe mbolea katika zizi la ng’ombe lakini akiwa huko, binamu yake, ambaye ni mtoto wa mama yake mkubwa, alimfuata na kutaka kumbaka, kabla ya kufanikiwa kukimbia.
Alipokwenda, kwanza aliambiwa atoe mbolea katika zizi la ng’ombe lakini akiwa huko, binamu yake, ambaye ni mtoto wa mama yake mkubwa, alimfuata na kutaka kumbaka, kabla ya kufanikiwa kukimbia.
Alisema
alipomweleza shangazi yake kuhusu suala hilo, alimjibu kwa kilugha
akimwambia kuwa asimwambie upuuzi, kitu ambacho kilimuuma binti huyo
ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 15.
“Niliondoka
baada ya shangazi kunijibu hivyo. Nikiwa nafua nguo, Agustin aliniita
ndani, nikajua ananipa zingine ili nifue, lakini nilipoingia alinishika
mkono na kunivutia chumbani kwake, akaniambia ole wangu nikipiga kelele
au kumwambia mtu, atanifanyia kitu ambacho sitasahau, aliniziba mdomo,
akanivua ngua na kuanza kuniingilia,” alisema binti huyo.
“Nilisikia
maumivu makali sana, nikamwambia shangazi, lakini hakutaka
kunisikiliza, nikamweleza pia yeye mwenyewe Agustin kuwa nimeumia sana,
hakunijibu. Kesho yake aliniletea dawa nimeze, nikameza nikarudi kwa
bibi yangu. Baada ya miezi 6 nikasikia tumbo linauma, nikajua nina
minyoo nikamwambia shangazi akanipa dawa za minyoo, nikazimeza, hata
hivyo sikuona dalili za kupona.
“Nikamwambia
Agustin naumwa tumbo, akaniambia nioge anipeleke hospitali, nilipima
nikakutwa nina mimba ya miezi 5, alinichukua akanipeleka hospitali ya
Mawezi, akaongea na daktari mmoja akampa dawa, sikujua ni za nini
nilipotumia nilipatwa na kizunguzungu, kumbe zilikuwa ni za kutoa mimba,
pia alinipeleka Arusha Mianzini kwenda kutoa mimba kwenye dispensari
iliyoko huko, akapewa dawa anipe wakati tukiwa tumefika nyumbani.”
Baada
ya zoezi hilo kushindikana, msichana huyo alisema dada wa Agustin
aitwaye Aniseta alimpigia simu rafiki yake mmoja aishiye Dar akimuomba
aje Moshi kuna kazi anataka amsaidie.Inadaiwa kuwa rafiki huyo
anayetajwa kwa jina moja la Najma alitumiwa nauli ya shilingi laki moja
aende Moshi na alipofika, alimwambia kuwa kaka yake amempa mimba mtoto
wa ndugu yake hivyo wanataka wamtoroshe kumpeleka Dar akae mpaka
ajifungue kwani kule polisi na walimu wanamfuatilia ili wamfunge.
Najma
alipatikana na kukiri kwenda Moshi kumfuata binti huyo, lakini
alipofika naye Dar, rafiki yake alipigia simu na kumtaka amdhuru binti
huyo ili kupoteza ushahidi, jambo ambalo alilipinga licha ya wito wao wa
mara kwa mara.
Mwenyekiti
wa kijiji cha Mloe, Salutary Mushi naye alisema ni kweli Agustin ana
tabia ya kupenda kutoka na watoto wadogo, jambo ambalo limekuwa kero
kubwa mtaani hapo kwani huyu si mtoto wa kwanza kumharibia maisha,
akidai pia kuwahi kufanya hivyo kwa mtoto wa baba yake mkubwa.
Agustin
mwenyewe hakupatikana licha ya kuwepo habari za kuachiwa kutoka kituo
cha Polisi Moshi alikopelekwa kwa kosa hilo lililofunguliwa kwa faili
namba MS/RB3336/014.
Maoni
Chapisha Maoni