Mfahamu Jyoti, mwanamke mfupi zaidi duniani 'Sentimita 60' anaepata deals kubwa Marekani


Unaweza kuwa mfupi kiasi cha kukufanya utamani kuongezeka, lakini ukiwaona wenzako wanavyopeta nalo basi utagundua unapaswa kumshukuru Mungu kwa umbo lolote ulilopewa.
Jyoti Amge, mwenye umri wa miaka 21, ndiye mwanamke mwenye kimo kifupi zaidi duniani akiwa na urefu wa inches 24 (sawa na urefu wa rula mbili za sentimita 32).

Jyoti ambaye ni mkazi wa Napur, India, aliingia rasmi katika kitabu cha Guinness mwaka 2011 kama mwanamke mfupi zaidi duniani aliye hai na tayari ameshapata deals kubwa kwa kimo chake.
Amewahi kushiriki katika makala maalum ya Body Shock: Two Foot High Teen na August 13, na mwaka huu alipata deal ya kuigiza katika ‘American Horror Story: Freak Show’.

Mwanamke huyo ambaye kimo chake kinatajwa kuwa kimetokana na tatizo la kutokua kawaida ‘achondroplasia’ anaendelea kupiga deals kubwa na amegeuka kuwa lulu kwa muonekano huo wa kipekee.

Jyoti akiwa amebebwa
  JustN

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA