PAKA MWEUSI AKATIZA UWANJANI CAMP NOU, WAKATI BARCA YAUA 3-0 LA LIGA


Mchezaji wa Barcelona, Lionel Messi akishangilia baada ya kufunga bao katika dakika ya 42 kipindi cha kwanza dhidi ya Elche usiku wa kuamkia leo.
Paka mweusi akiingia uwanjani na kusababisha mchezo kusimama wa muda.
Paka huyo akiondoka uwanjani.
Lionel Messi (mwenye mpira) akiwatoka wachezaji wa Elche.
BARCELONA imeanza vyema La Liga kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Elche Uwanja wa Camp Nou usiku wa kuamkia leo.
Katika mchezo huo, kiungo wa Barca, Javier Mascherano, alitolewa nje kwa kadi nyekundu kipindi cha kwanza, kocha mpya Luis Enrique akiiongoza timu kwa mara ya kwanza, alionyesha mwanzo mzuri.
Wafungaji wa timu ya Barca ni Lionel Messi dakika ya 42 na 64,  Munir El Haddadi Moham dakika ya 46.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA