HUYU ndo DEREVA TAX MWAMINIFU..ARUDISHA PESA ZAIDI ya TSH.BILIONI 2 ALIZO SAHAU MTEJA KWENYE GARI LAKE.
Dereva
mmoja wa taxi nchini Singapore amepongezwa na kusifiwa kwa uaminifu na
moyo wa imani baada ya kukabidhi kitita cha zaidi ya paundi 500, 000
sawa na mabilioni ya shilingi kilichokuwa kimesahaulika kwenye gari
yake.
Dereva
huyo Sia Ka Tian (pichani) mwenye umri wa miaka 70 na ambaye amekuwa
akiendesha taxi katika mji wa Singapore kwa zaidi ya miaka 30, alikuwa
amewashusha wapenzi wawili watalii kutoka Thailand waliokukwenda
kujivinjari nchini humo, baadae aligundua katika kiti cha gari kuna
mfuko mweusi ambao sio wa kweke.
Anasema
alipoufungua alikutana uso kwa uso na fedha nyingi zaidi ya dila
milioni moja za Singapore na papo hapo akaamua kuzipeleka katika ofisi
ya serikali inayohusika na vitu vilivyopotea na kuzisajili zikisubiri
atakayeulizia.
Katika
mahojiano na gazeti moja dereva huyo alipoulizwa kwa nini hakuingia
mitini
na fedha hizo, alijibu kuwa kwanza pesa sio muhimu kwangu, pili
pesa hizo sio za kwangu , akahoji kwanini nizichukue?
Inasemekana
kuwa wale wapenzi watalii walitoa taarifa ya kupotelewa na mzigo wao
katika kampuni inayomiliki taxi anayoendesha mzee Sia.
Haikuchukua muda taratibu zilifanyika kisha wakakabidhiwa kitita chao bila kupungua hata sumni.
Taarifa
zinasema dereva huyo amezawadiwa na kampuni yake ya taxi hizo na
atakabidhiwa tuzo ya heshima kwa uaminifu wake. Hata hivyo haijajulikana
kampuni hiyo itampa zawadi gani.
Maoni
Chapisha Maoni