Picha: Mama mzazi wa Sylvester Stallone 'Rambo' mwenye miaka 92 akifanya mazoezi ya kunyanyua vyuma


 Kama ulimuona Sylvester Stallone kwenye Expandables, bila shaka uliona umri wake ulivyo mkubwa huku akiendelea kutisha kama bado ni kijana mdogo. Sasa utamshangaa zaidi mama yake mzazi, Jackie mwenye miaka 92 anaeamini umri sio kikwazo.
Bibi huyo ameendelea kufanya mazoezi ya viungo licha ya kuwa na umri mkubwa na hata anapokuwa gym hubeba hadi vyuma vyenye uzito huku akisaidiwa kwa ukaribu na watu.

Bibi Jackie bado anavaa Mini-Skirt, na kupaka make up kama wanavyofanya wasichana warembo wenye umri mdogo.

“Hollywood wanahofia umri, lakini nadhani wazee ndio wanakuja. Nadhani umri wa mwanamke wa kati unarudi. Wote tungependa kufika kule, kufika kule kama mimi. Sio kwenye kiti cha kukusaidia kutembea, wala kuwa kwenye kitu maalum cha kutunzwa.” Amesema mama Rambo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA