AUNT EZEKIEL AFUMWA LIVE NA MUME WA MTU...AKIMBILIA KWA WEMA SEPETU


Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson akiwa na shost yake Wema Isaac Sepetu.

KAMA hakuwahi kutoa sadaka, huu ndiyo muda wake! Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson anadaiwa kukinukisha nyumbani kwa Wema Isaac Sepetu baada ya kunusurika kufumaniwa na mume wa mtu, Moses Peter Iyobo a.k.a Moze Iyobo ambaye ni densa wa Nasibu Abdul ‘Diamond’.
 Habari zisizokuwa na shaka zinadai kwamba tukio hilo lilijiri Jumapili iliyopita nyumbani kwa Wema, Kijitonyama, Dar ambapo Aunt alisababisha tafrani iliyosababishwa na mke wa mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina la Mwengi Ally.



Kwa mujibu wa mashuhuda wetu waliokuwa wakizungumza kwa kupokezana, Mwengi alidai kwamba Aunt amekuwa akitembea na mumewe huyo hivyo timbwili lilianzia nyumbani kwa Aunt, Mwananyamala A jijini Dar. 
Ilidaiwa kwamba, huku Aunt akiwa hajui hili wala lile, ghafla waliibuka wasichana saba na kumuanzishia mwigizaji huyo.Mashuhuda hao walidadavua kwamba katika kujinusuru na kipigo ambacho alihisi akiwa peke yake, angeumizwa Aunt alikimbilia  nyumbani kwa shoga yake, Wema.  SOMA ZAIDI>>

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA