Mfumo wa Vanishing Spray kutumika ligi ya Uingereza msimu ujao


Chama cha soka nchini Uingereza FA, kimeidhinisha matumizi ya Vanishing Spray, kuanzia msimu ujao wa ligi kuu ya soka nchini humo pamoja na michuano mingine iliyo chini ya chama hicho.
FA wamekubali matumizi ya Vanishing Spray, baada ya majadilino na chama cha waamuzi nchini Uingereza ambacho kimeafiki matumizi ya Spray hiyo ambayo mashabiki wengi walianza kuiona wakati wa fainali za kombe la dunia zilizofanyika nchini Brazil.
Tayari nchi kama Hispania pamoja na Italia zimeshathibitisha matumizi ya Vanishing Spray, hivyo Uingereza inakuwa nchi ya tatu barani Ulaya kukubali waamuzi kutumumia mfumo huo.
Mtendaji mkuu wa chama cha soka nchini Uingereza FA Richard Scudamore, amesema imewalazimu kupitisha Vanishing Spray, kwa lengo la kupiga hatua ambapo wanaamini malalamiko huenda yakapungua kutoka kwa wachezaji pamoja na mameneja ambao wamekua wakipingana na waamuzi inapotokea adhabu ndogo.

Kutokana na maazimio hayo, Uingereza wanakubali kusudio la pili kutoka shirikisho la soka duniani FIFA la kumaliza utata uwanjani baada ya kufanya hivyo wakati wakipitisha matumizi ya mfumo wa utambuzi wa mpira kuvuka mstari wa goli *Goal Line Tecknology* ambao ulianza kutumika kwenye ligi ya nchini humo msimu uliopita.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA