PICHA 5 ZA MAZISHI YA MKE WA MSANII AFANDE SELE LEO MOROGORO
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Professor akiwa na Afande Sele Morogoro
Professor Jay amesafiri hadi mkoani Morogoro kwenda kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa mke wa msanii mwenzake Afande Sele.\
Kupitia Instagram, Professor ameshare picha akiwa kwenye mazishi na kuandika: Msibani Morogoro nyumbani kwao marehemu Asha au mama Tunda sasa hivi… tunajiandaa kwenda kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele saa kumi jioni ya leo, bwana alitoa bwana ametwaa, jina la bwana lihimidiwe….Amen
Jeneza la marehemu likiwa nje pamoja na watu mbalimbali waliojitokeza katika mazishi hayo
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Awali Afande Sele alisema kifo cha Mama Tunda kimetokana na uzembe wa madaktari. Mama Tunda alifariki baada ya kulazwa kutokana na kuugua Malaria. Akizungumza na Bongo5 leo, Afande alidai kuwa bila uzembe wa madaktari huenda malaria isingechukua uhai wa Mama Tunda.
Afande Sele akilia kwa uchungu
“Mama Tunda ametuachia pengo kubwa sana kwenye familia,” alisema Afande. “Amefariki jana saa tano usiku katika hospitali kubwa hapa Morogoro kutokana na uzembe wa madaktari. Walimpa matibabu akarudi nyumbani, sitaki kulizungumzia kiundani kwa sasa hivi kwa sababu tupo kwenye wakati mgumu. Huku mazishi yatafanyika kuanzia kama saa tisa hivi lakini bado hatutajua itakuwa wapi bado tupo kwenye mipango. Malaria ilimchukua sana, kwa familia na watoto kwetu ni msiba mkubwa sana, yaani ni huzuni sana,” aliongeza.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni