MASANJA awavuruga WEMA na DIAMOND


COMEDIAN mwenye kofia ya uchungaji kwa sasa, Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ hivi karibuni aliwabomoa mastaa wapenzi Nasibu Abdul ‘Diamond’  na ubavu wake Wema Sepetu kwa kuwaandikia waraka mzito unaohusiana na maisha yao ya kila siku.
Katika waraka huo, aliouweka kwenye ukurasa wake wa Instagram, Masanja aliwataka wawili hao kujirekebisha mapungufu yao kama kweli wanapendana kwa dhati.
Akiuzungumzia waraka huo baada ya kuvutiwa waya na kachala wa Ijumaa, Masanja alisema hakuwa na nia mbaya kuwaandikia wapenzi hao kama watu watakavyojaribu kufikiria, bali alifanya hivyo kiroho safi na hivyo ni wajibu wao kuukubali au kuukataa.
“Sina maana hiki nilichokisema lazima wakichukue kama kilivyo, bali wao wenyewe wanapaswa kuangalia mara mbilimbili ushauri wangu kabla mambo hayajaharibika,” alisema.
Alimtaka Wema kutambua kuwa mume ndiyo kichwa cha nyumba, kwani kwa mujibu wa Diamond inaonekana binti huyo hamsikilizi mwenziye.
masanja
“Naamini kabisa kwa mujibu wa muongozo niliousoma kupitia maelezo ya Diamond kuwa hamsikilizagi, hivyo anatakiwa kuomba msamaha tena na tena, akubali kubadilika.”

WARAKA WENYEWE HUU HAPA

“Hili swala la Diamond na Wema nadhani Mungu amemhurumia mmoja wapo kati ya hao wawili, kama wangekuwa watu wa kuoana wangeshaoana muda mrefu, uchumba gani mrefu kama wanasomea udaktari? Rafiki yangu Nasibu kama kweli mlipendana kwa dhati hizo kasoro zinarekebishika, maana hakuna mwanadamu aliye sahihi kwani hata wewe Nasibu una mapungufu yako.
Mastaa Wema Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond’ wakiwa kwenye pozi la kimahaba
Mastaa Wema Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond’ wakiwa kwenye pozi la kimahaba
Na wewe dada yangu Wema lazima ujue mume ndiyo kichwa cha nyumba kwa maelezo hayo inaonyesha haumsikilizagi mwenzio, omba msamaha kila mara na pia ukubali kubadilika.
Mi sipendi mkiwa mnaongozana wote kwenye shoo ya usiku, mume anatakiwa aende kufanya kazi mke abaki nyumbani akirudi mwili umepoa hata ujauzito unaingia, sasa wote stejini mkirudi miili ya moto si mtazaa popompo jamanii!!!
Tupe maoni yako hapo Chini..!!

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA