NDOA YA JIDE, GARDNER MAZITO YAIBUKA
Uzio wa nyumba ya Staa, ‘Lady Jaydee’ au ‘Jide’Gardner G Habash, ikiwa umezungukwa na nyasi.
Katika habari hiyo, ilielezwa kwamba mitandao mingi ya kijamii ndani
na nje ya Bongo ilipambwa na sakata la mastaa hao kudaiwa kutengana huku
Gardner akikanusha kwamba hakuna kitu kama hicho.Mara baada ya habari hiyo kwenda hewani, wikiendi iliyopita gazeti hili lilipokea simu nyingi zikianika undani wa kile wanachokijua.
“Gardner atuambie ukweli maana hata huku nyumbani (Kimara-Temboni, Dar) tuna zaidi ya miezi miwili hatuwaoni,” alisema mmoja wa wapiga simu hao.
Geti la nyumba hiyo likiwa na vumbi.
Ili kuthibitisha kilichosemwa, gazeti hili lilifika nyumbani kwa
mastaa hao na kushuhudia geti na nyumba vikiwa na mavumbi ya kutotumika
huku kukiwa hakuna hata alama za tairi za gari.Wanahabari wetu
walishinda eneo hilo bila wawili hao kurejea nyumbani ambapo kwa mujibu
wa majirani, Gardner alionekana akiingia nyumbani hapo akiwa na gari
aina ya Toyota Coaster la bendi yao ya Machozi na alipoondoka ndiyo
ikawa kimoja. “Ninyi angalieni mazingira. Ona maua na miti ilivyoweka vichaka na
pori. Ni vigumu kuamini kama staa mkubwa kama Jide anaishi kwenye
mazingira kama haya,” alisema mmoja wa majirani zao.Gazeti hili liliweka ‘patroo’ ya jirani huyo ambaye hadi tunakwenda mitamboni, wawili hao walikuwa hawaonekani nyumbani hapo.
Mbongo
Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ au ‘Jide’ na Mtangazaji wa
Radio Times FM, Gardner G Habash wakiwa katika picha ya pamoja.
Pamoja na yote hayo na ishara mbaya zinazoonekana juu ya wawili hao
ikidaiwa kila mmoja anaishi kivyake, bado Gardner amekuwa akisisitiza
hakuna chochote kinachoendelea na kwamba hajui anayeeneza habari hizo
ana lengo gani. Kwa upande wake Jide, wikiendi iliyopita alitupia mtandaoni picha ya kidole chenye pete ya ndoa huku akiombwa chondechonde na mashabiki wake aendelee kutetea ndoa yake
Maoni
Chapisha Maoni