DIAMOND: Sitaoa Milele…!


Kutoka moyoni? Wakati bimkubwa Wema Isaac Sepetu akijiaminisha na kuhisi kuwa amepata mume ambaye ni baba bora, mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amefunguka kuwa kamwe hafikirii kuoa, Ijumaa lina cha kukuhabarisha.
Kauli hiyo ya Diamond inakuja wiki kadhaa baada ya Wema kuonekana na pete ya ndoa kidoleni kisha kukiri kuvishwa na ‘kichaa’ huyo wa Bongo Fleva ambaye amerejea kutoka Marekani alikotwaa Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki zilizokwenda kwa jina la African Muzik Magazine (AFRIMMA) 2014.
Staa Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa kwenye pozi lenye utata.
Staa Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa kwenye pozi lenye utata.

Hofu ya kuoa

Akizungumza na gazeti hili kwenye mahojiano maalum, Diamond alisema kuwa anahofia kuoa kwa madai kwamba akifanya hivyo anaweza kuanguka kimuziki kitu ambacho hataki kimtokee maishani mwake.
Kumbe!
Jamaa huyo ambaye siku hizi anajiita Dangote (jina la tajiri wa Nigeria, Aliko Dangote) alitiririka kuwa zamani alikuwa na wazo hilo la kuoa lakini akiwatazama wanamuziki wenzake waliooa mwisho wa siku, makali yao hupungua na wengine kupotea kabisa kwenye ramani ya muziki.

Bofya hapa kumsikia Diamond

“Unajua unaweza kuona kama vile nazungumza kitu cha utani lakini ndiyo ukweli wenyewe.
“Kuna wanamuziki wengi walikuwa kwenye peak (kileleni) lakini walipooa tu ‘kiki’ yao ilishuka ghafla katika muziki na wengine wamepotea kabisa.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na Mtangazaji wa Radio E-FM, Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na Mtangazaji wa Radio E-FM, Penniel Mungilwa ‘Penny’.
“Ukifuatilia kwa umakini wapo mastaa wengi duniani ambao umri umekwenda sana lakini hawajaoa. Hata hapa nyumbani kuna mifano hai. Nadhani hofu yao ni kuona kuwa wakifanya hivyo watashuka kimuziki,”alisema Diamond.

Ni kweli kamvisha pete Wema?

Alipoulizwa kama ni kweli amemvisha pete ya uchumba Wema, msanii huyo hakuwa tayari kufafanua kwa kigezo kwamba pete ni urembo kama urembo mwingine kwa mwanamke.

Nje ya boksi

Baada ya kusikia msimamo wa Diamond, gazeti hili lilijiongeza na kutoka nje ya boksi ambapo lilizungumza na baadhi ya wasanii waliooa na wasiooa ambapo walieleza mambo mazito.
Jackline Wolper
Jackline Wolper

Siri yafichuka

Katika mazungumzo yao kwa sharti la kutochorwa gazetini, wasanii hao walidai kwamba Diamond anahofia kupoteza kiki kwa warembo ambao wengi ndiyo mashabiki wake wanaoamini nao wanaweza kupata zali la kuolewa naye ndiyo maana humzingira na kumuomba namba ya simu kila anakokwenda.
Msururu wa mademu
Ilielezwa kwamba kwa kuwa jamaa huyo hupenda kuwa juu ndiyo maana alisharipotiwa kutoka na msururu wa wanawake mastaa ambao huchangia jina lake kuendelea kuwa juu.
Ilidaiwa kwamba wakati anatafuta namna ya kuchomoka kimuziki alidaiwa kutoka kimapenzi na warembo waliokuwa na majina madogo kama Rehema Fabian aliyepata umaarufu kupitia Shindano la Miss Kiswahili.
Jokate Mwegelo.
Jokate Mwegelo.
Ilisemekana kwamba baada ya hapo alidaiwa kuwa na msururu wa wanawake mastaa kama waigizaji Jacqueline Wolper Massawe na Aunt Ezekiel Grayson na Jokate Mwegelo.
Baadaye jamaa huyo alidaiwa kuruka na wasichana ambao hawakuwa na kiki hivyo aliwamwaga ndani ya muda mfupi kama Najma na Natasha.
Baadaye Diamond alitua kwa Wema hadi akafikia hatua ya kumvisha pete ya uchumba mwaka 2012 ndani ya Ukumbi wa New Maisha uliopo Masaki jijini Dar.
Kumbukumbu zinaonesha kwamba muda mfupi baada ya kumvisha Wema pete ya uchumba walimwagana ambapo Diamond alitua kwa Mtangazaji wa Radio E-FM, Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Irine Uwoya
Irine Uwoya
Diamond hakudumu na Penny kwa madai kwamba mrembo huyo hakuwa na kiki kama ilivyokuwa kwa Wema ambaye jina lake halijawahi kushuka tangu alipovaa Krauni ya Miss Tanzania 2006/07.
Ilisemekana kwamba hata tuzo zilipungua ndipo akampiga Penny chini na kurudi kwa Wema ambaye inasemekana ndiye anayemng’arisha.
Hawa wameoa, je, wameshuka?
Baadhi ya mastaa waliooa ni pamoja na Mohamed Ahmed ‘Z-Anto’, Nurdin Bilal ‘Shetta’, Amini Mwinyimkuu, Lawrence Marima ‘Marlaw’, Amani Temba ‘Mheshimiwa Temba’ na wengineo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA