Shabiki wa Brazil auawa Kenya
Furaha ya mashabiki wawili wa
kombe la dunia iligeuka na kuwa matanga jumamosi usiku baada ya watu
wawili kupoteza maisha kufuatia ubishi kuhusiana na matokeo ya kombe la
dunia linaloendelea huko Brazil.
Shabiki wa kwanza aliuawa baada ya utani wa
shabiki ilizusha ubishiuliyosababishwa akadungwa kisu tumboni nje ya
baa moja katika mtaa wa Awendo iliyoko katika jimbo la Migori magharibi
mwa Kenya.Zaidi ya Saa nane baadaye yule aliyetoroka eneo la tukio naye alisakwa na umati wa watu waliokuwa wamejawa na hamaki na wakampiga hadi kufa kabla ya polisi kufika huko alikokuwa ametorokea.
Miili yote miwli imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya.
Maoni
Chapisha Maoni